Matumizi ya Mihadarati

 1. Morphine, Cocaine iliyofichwa katika vifungu vya nguo zanaswa JKIA,Kenya

  th

  Morphine na cocaine iliyofichwa kwenye vifungo vya kitenge vilinaswa Alhamisi katika uwanja wa ndege ya Jomo Kenyatta,JKIA nchini Kenya .

  Mkurugenzi wa DCI George Kinoti amesema kasha la dawa hizo za kulevya zilizofichwa katika vifurushi viwili zilinaswa kufuatia habari walizopokea awali.

  "Moja ya shehena ambazo zilikuwa zilipelekwa Australia kutoka Kenya zilitajwa kuwa pete za jadi za Kiafrika," alisema.

  Kinoti alisema mtu wa kawaida angechukulia jozi 168 za vipuli kuwa vipuli kama ilivyoripotiwa .

  "... lakini maafisa wa polisi waliokuwa makini waliona kuna zaidi ndani ya kifurushi hicho. Baada ya uchunguzi wa kina, waligundua podari ya manjano iliyofichwa kwa ujanja ndani ya mapambo," Kinoti alisema.

  View more on twitter

  Kinoti aliendelea kusema kuwa shehena ya pili ilikuwa imetajwa kuwa nguo 12 za vitenge na ilikuwa ikipelekwa Hong Kong.

  Wapelelezi wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya walifungua shehena na wakapata nguo 12 vifungo 199 zaidi vilivyotumiwa kuficha dawa hizo.

 2. Video content

  Video caption: Jinsi raia wa Mexico wanavyosaidika wakati wa Covid-19

  Makundi ya watu wanaouza madawa ya kulevya wasaidia familia maskini nchini Mexico