Baraza la Usalama la UN

 1. Mzozo wa Tigray: Baraza la Usalama la UN lashindwa kukubaliana

  Mamia ya watu waliuawa mzozo ulipozuka mwezi Novemba
  Image caption: Mamia ya watu waliuawa mzozo ulipozuka mwezi Novemba

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kufikia tamko la pamoja kuhusu mzozo wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia, baada ya Urusi, China na India kuchukualia mgogoro huo kuwa suala la ndani.

  Wanadiplomasia walionukuliwa na shirika la habari la AFP wamesema nchi tatu za Afrika katika baraza hilo- Kenya, Niger na Tunisia - zimeunga mkono rasimu ya taarifa iliyoandikwa.

  Kamishena wa kutetea haki katika Umoja wa Mataifa katika awali alisema kulikuwa na ripoti za kusikitisha zinazoashitia huenda uhalifu wa kivita ulitekelezwa katika jimbo Tigray.

  Michelle Bachelet aliangazia visa vya unyanyasajji wa kijinsia, mauaji ya kiholela na uharibifu mkubwa ulifanywa katika eneo hilo.

  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki inataka kupewa idhini ya kuchunguza ripoti za ukatili uliotekelezwa na majeshi ya Ethiopia na Eritrea, wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front na vikosi vya jimbo la Amhara.

  Maelezo zaidi:

 2. Walinda amani wa UN Tigray 'wakataa kurudi nyumbani'

  Walinda usalama Ethiopia katika Umoja wa Mataifa walikuwa wabadilishwe
  Image caption: Walinda usalama 169 wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa walikuwa wabadilishwe

  Walinda usalama 15 wa Ethiopia nchini Sudan Kusini, kutoka eneo la Tigray, wamekataa kurudi Ethiopia siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la AFP inayomnukuu msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.

  Kikosi cha maafisa 169 wa Ethiopia kilikuwa kiondoke nchini Sudan Kusini.

  "Tunajaribu kutafuta maelezo, lakini nafahamishw akwamba karibu maafi 15 wa kikosi cha Ethiopia walikata kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Juba... wameomba kusalia huko," Bw. Dujarric alinukuliwa kusema katika mazungumzo na wanahabari.

  Mzozo ulizuka katika jimbo la Tigray mapema mwezi in Novemba mwka 2020 baada ya wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) kuvamia kabi ya majeshi ya muungano katika eneo hilo baada kufuatia tofauti kati yao na serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

  Maelfu ya watu waliripotiwa kuawa na wengine karibu milioni mbili kufurushwa makwao.

  Soma zaidi:

 3. UN kutekeleza mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia.

  Nyuklia

  Umoja wa Mataifa, Ijumaa itatekeleza mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.

  Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia unajumuisha ahadi ya kuacha kufanya utafiti, majaribio pamoja na utumiaji wa silaha hizo ambazo ni tishio.

  Mataifa yenye silaha za nyuklia hayakutia saini mkataba huo.

  Lakini wanaharakati wana imani kuwa hatua hiyo inaongeza shinikizo la kuachana na silaha za nyuklia na katibu wa umoja wa mataifa anaelezea hatua hiyo kama muhimu katika kufikia lengo la kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.