Muziki

 1. Kanye West abadilisha jina lake kuwa Ye

  Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.
  Image caption: Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

  Msanii wa Marekani aliyekua akijulikana kama Kanye West sasa itajulikana rasmi kama wewe tu.

  Jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la rappa huyo kubadilisha jina, afisa mawasiliano katika Mahakama Kuu ya Los Angeles alithibitisha.

  Nyota huyo wa miaka 44-aliwasilisha ombi hilo mwezi Agosti, akitoa "sababu za kibinafsi."

  Rapa huyo, anayejulikana sana kwa vibao kama vile Gold Digger na Stronger, alikua akitumia Ye kama jina la utani na mnamo 2018 alilitumia kama jina la albamu.

  Muda mfupi baada ya kutolewa kwa albamu hiyo, alitweet: "Kujulikana rasmi kama Kanye West. Mimi ni YE."

  Sasa amelifanya rasmi na jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

  Ijapokua jina la Ye tayari lilikua likitumia kwenye Twitter, akaunti yake ya Instagram na wavuti yake bado inatumia jina lake la zamani kufikia Jumanne.

  "Ninaamini 'Ye' ni neno linalotumiwa sana katika Biblia, na katika Biblia linamaanisha wewe. Kwa hivyo mimi ni wewe, mimi ni nyinyi, yaani ni sisi," alisema katika mahojiano ya 2018 na mtangazaji wa redio Big Boy.

  Wasnii wengine waliobadilisha jina ni Prince, Snoop Dogg na Sean Love Combs, wengine wao mara kadhaa.

  Kim Kardashian West azungumzia matatizo ya akili ya Kanye West

  Je Umma unapaswa kumhukumu Kanye west kwa afya yake ya akili?

 2. Msanii wa Nigeria Tiwa Savage afichua njama ya utapeli kupitia video ya ngono

  Tiwa Savage anasema ana wasiwasi juu ya athari ya video hiyo kwa mtoto wake
  Image caption: Tiwa Savage anasema ana wasiwasi juu ya athari ya video hiyo kwa mtoto wake

  Nyota wa muziki wa Nigeria Tiwa Savage amefichua kuwa anatapeliwa kwa kutumia kanda ya video ya ngono lakini hatalipa.

  Anasema video hiyo iliwekwa kwa bahati mbaya katika mtandao wa Snapchat na mpenzi wake ambaye aliifuta baadaye alipogundua kilichotokea lakini tayari ilikwa imepakuliwa na mhuni ambaye amekuwa akimfuatilia msanii huyo.

  Anasema mara ya kwanza aliangua kilio alipoona video hiyo akihofia jinsi itakavyopokelewa

  Savage, 41, ni mmoja wa wasani tajika duniani wa miondoko ya Afrobeats na amesainiwa katika lebo ya Universal Music Group.

  Alipata umaarufu kutokana na muziki wake kama vile Kele Kele na Eminado na alikuwa mmoja wa wasani waliosajiliwa katika lebo ya muziki ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy nchini Nigeria, ambako anafahamika kama First Lady.

  "Sitaiita video ya ngono lakini ni video inayonihusu mimi na mpenzi wangu wa sasa ," alimwambia mtangazaji Angie Martinez wa kituo cha redio cha Power 105.1 mjini New York.

  Alifichua kwamba tukio hilo lilitokea mwezi uliopita na kwamba mtu huyo alijaribu kumtapeli lakini hakuwa tayari kusalitiwa na mtu yeyote "kwa kufanya jambo ambalo ni la kawaida".

 3. Video content

  Video caption: ‘’Niliacha shule ili nitilie mkazo katika utayarishaji wa muziki’’

  ‘’Niliacha shule ili nitilie mkazo katika utayarishaji wa muziki’’

 4. Video content

  Video caption: Ifahamu bendi hii ya wanawake pekee Tanzania

  Bendi ya wanawake huwa ni nadra sana kuskika kutokana na dhana kwamba wanawake hawawezi kushirikiana.

 5. Video content

  Video caption: "Ninacheza vyombo vyote bendi yangu ya muziki ya Ireland"

  Caitríona Lagan ana uwezo wa kucheza ala tano za muziki kwa wakati mmoja