Masuala ya Polisi

 1. Kenya yachunguza kisa cha 'mtoto aliyefariki' polisi wakitekeleza amri ya kutotoka nje

  Police have put up roadblocks nationwide to enforce a curfew introduced to reduce coronavirus infections
  Image caption: Polisi wameweka vizuizi barabarani kote nchini kutekeleza amri ya kutotoka nje

  Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi nchini Kenya (IPOA), imeanza kuchunguza ripoti kwamba mtoto alifariki baada ya maafisa waliokuwa wakitekeleza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kama hatua ya kuzuia kuenezwa kwa virusi vya corona kukataa kufungulia gari lililokuwa likimpeleka hospitali.

  Mtoto huyo wa miezi minne aliyekuwa na tatizo la kupumua alikuwa akikimbizwa hospitali jumamosi iliyopita, babu yake aliambia gazeti la Nation.

  Madaktari walisema mtoto huyo alihitaji kupelekwa katika hospitali ya rufaa iliyokuwa umbali wa kilomita 25.

  Lakini maafisa waliokuwa katika kizuizi cha barabarani wanadaiwa kukataa kuwafungulia njia kwa sababu ya utekelezaji amri ya kutotoka nje iliyowekwa kuzuia maambukizi ya Covid 19.

  View more on facebook

  "Isingekuwa kizuizi hicho cha barabarani, maisha ya mjukuu wangu yangeweza kuokolewa," babu ya mtoto huyo, alisema kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Nation.

  Kenya imeweka amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri ili kuzuia kuongezeka kwa maambukizo ya virusi vya corona.

  Polisi haijajibu ombi la BBC la kupata kauli yao kuhusiana na suala hiyo.

  Mwezi uliopita, maelfu ya waendeshaji magari na abiria walikwama kwa masaa kadhaa katika trafiki katika mji mkuu, Nairobi, baada ya polisi kufunga barabara kuu jijini.

  Mamlaka zikosolewa sana lakini wanasisitiza kwamba utekelezaji mkali wa amri ya kutotoka nje ni muhimu kushughulikia kuongezeka kwa maambukizo.

 2. Idara ya polisi Kenya yatetea usajili wa makurutu wenye alama za chini

  Msemaji wa Idara ya Polisi nchini Kenya ametetea mchakato wa kusajili makurutu, akisema kwamba wale waliopata alama za juu katika mitihani ya kidato cha nne walikuwa na mahitaji yasiyoweza kutimizika.

  Aliongeza kwamba walikuwa wameweka angalizo kubwa katika taaluma zao na wenye uwezekano mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii ikilinganishwa na waliopata alama za chini, Charles Owino amezungumza na Citizen TV.

  Aliongeza:

  ‘’Tunakuwa na changamoto tunapoajiri kila afosa wa polisi mwenye alama ya C+ na kuendelea…wao hurejea shuleni, nba kuendelea na masoma na kupata shahada, wanaporejea wanasema ‘sasa hatutaki kuhudumu katika kiwango hichi'."

  View more on twitter

  Bwana Owino amesema kuwa kile cha muhimu ni kusajili "watu werevu", na kusema kuwa hilo haliwezi kutathminiwa kwa alama alizopata mtu pekee.

  "Unaingia na alama nzuri... na unakosa kufanya kazi yako, sio kisomo chako kitakachofanya kazi yako, lazima uwe mtu wa vitendo, na ni lazima uhakikishe unapandishwa cheo kihalali," Bwana Owino amesema.

  Idara ya polisi mara nyingi huwa inaorodheshwa kama taasisi yenye ufisadi zaidi katika serikali, maafisa wake wakishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kuingilia haki za watu.

 3. Video content

  Video caption: Polisi awanunulia washukiwa wa wezi chakula cha Krismasi

  Afisa wa polisi nchini Marekani alieitwa kukamata familia inayoshukiwa kuiba ndani ya duka la jumla, badala yake awanunulia chakula cha Krismasi.