Maeneo ya Wapalestina

 1. Kiongozi mkuu wa kidini Gaza aonya dhidi ya kupinga chanjo ya Covid

  Gaza
  Image caption: Takriban asilimia 5 ya idadi ya watu Gaza wamepokea angalau dozi moja ya chanjo

  Kiongozi mkuu wa Gaza amewataka Wapalestina kupata chanjo haraka iwezekanavyo.

  Katika ujumbe wa video, Sheikh Hassan al-Lahhan anasema yeyote anayechelewe kupata chanjo ni “mwenye dhambi”na anaelezea mtu yeyote anayesambaza virusi hivyo bila kukusudia kama “wauwaji wa kutokusudia”.

  Kama kiongozi mkuu wa Kiislamu wa Gaza, Sheikh Hassan al-Lahhan anasimamia huduma ya maswala ya kidini katika eneo linaloongozwa na Hamas.

  Jaribio la kuhamasisha kuchukua chanjo linakuja wakati viwango vya wanaopata maambukizi ya Covid-19 ikianza kuongezeka tena huko Gaza, ambako mfumo wa afya umelemaa kutokana na vita vya miaka.

  Uwasilishaji wa chanjo kwa maeneo ya Palestina yaliyokaliwa umekuwa kwa mwendo wa polepole sana, lakini makundi ya kutoa misaada yanasema habari potofu na kusita kupata chanjo pia kumekuwa pingamizi.

  Huko Gaza zaidi ya watu 120,000 wamepokea angalau dozi moja - karibu asilimia 5 tu ya idadi ya watu katika Ukanda huo.