Ukame

 1. Ukame wa Madagascar: Watu wanakula 'mchanga uliochanganywa na ukwaju'

  Zao zinalopandwa kwa wingi Madagascar limekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua

  Raia wa kusini mwa Madagascar wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju kwasababu ya kiangazi ambacho kimeharibu zao linalotegemewa na wenyeji, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

  "Tunauita udongo wenye kuhimili kiangazi kwasababu unaruhusu ukwaju kukua na kutusaidia kukabiliana na kiangazi," AFP imemnukuu mkulima wa eneo Doday Fandilava Noelisona.

  "Siku hizi hatutafuti tena chakula bali tunatafuta mbinu za kupata kitu chochote cha kushikilia tumbo."

  Matunda ya dungusi ambayo watu huyategemea yamekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua.

  Aidha, shirika la AFP limemnukuu mkulima mwingine, Avianay Idamy, ambaye anasema amegeukia uuzaji wa makaa kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia yake angalau waweze kula muhogo mara moja tu kwa siku.

  Shirika la chakula dunia- WFP, linasema watu milioni 1.5 kusini mwa Madagascar wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

 2. Video content

  Video caption: Virusi vya corona: Tutaweza vipi kulinda bayoanuwai wakati wa corona?

  Wakati huu wa virusi vya corona bayoanuwai na mazingira kwa ujumla vimeathirika. Lakini je bayoanuwai inaweza kulindwa vipi wakati wa corona?. Wataalamu wanaeleza