UN

 1. Msako mkali dhidi ya jamii ya Tigray unaendelea Ethiopia- UN

  Demonstrators have been marching around the world to highlight the plight of Tigrayans

  Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu imesema takriban watu 1,000, wengi wao wakiwa kutoka kabila la Tigray, wamekamatwa tangu serikali ilipotangaza hali ya hatari tarehe 2 Novemba.

  Chini ya hali hiyo ya dharura ya miezi sita, serikali ina mamlaka makubwa ya kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini washukiwa bila kuwafungulia mashtaka, na kufanya upekuzi nyumbani bila vibali.

  Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alisema "takriban watu 1,000 wanaaminika kuzuiliwa kwa muda wa wiki moja au zaidi - huku ripoti zingine zikiweka idadi hiyo juu zaidi".

  Taarifa hiyo ilisema mazingira wanayozuiliwa ni mbaya na wafungwa wengi wanashikiliwa katika vituo vya polisi vilivyo na watu wengi.

  Wafanyakazi kumi wa ndani wa Umoja wa Mataifa ambao walikamatwa tarehe 9 Novemba bado wanazuiliwa.

  "Wengi wa wale wanaozuiliwa wanaripotiwa kuwa watu wa asili ya Tigray, wanaokamatwa mara kwa mara kwa tuhuma za kuhusishwa au kuunga mkono Tigray People's Liberation Front (TPLF)," UN ilisema.

  Katika siku za nyuma, polisi walisema kukamatwa huko hakukuwa na msukumo wa kikabila bali kulilenga wafuasi wa TPLF, ambayo imekuwa ikipambana na serikali kuu tangu mwaka uliopita na sasa wanatishia kuelekea mji mkuu.

  Mzozo wa Tigray, Ethiopia: Kwa nini ulimwengu mzima una wasiwasi na mzozo huu?

  Vita vya Ethiopia mwaka mmoja baadaye: Jinsi ya kumaliza mahangaiko

 2. Nusu ya madereva waliozuiliwa Ethiopia waachiwa huru - UN

  Millions of Ethiopians have been affected by the ongoing conflict

  Serikali ya he Ethiopia imewaachilia madereva wa misaada walio na mkataba wa Umoja wa Mataifa waliokamatwa wiki iliyopita, kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa.

  Katika kikao mjini New York, Farhan Haq alisema Jumatatu kwamba madereva 34 wameachiliwa lakini wengine 36 bado wanazuiliwa.

  Alitumai kuwa wafanyikazi waliosalia wa kandarasi na wafanyikazi 10 wa kitaifa wa UN waliokamatwa na mamlaka siku ya Ijumaa wataachiliwa.

  Kukamatwa kwao kwa wafanyikazi wa UN na wafanyikazi wa kandarasi kulifuatia tangazo la serikali ya shirikisho la hali ya hatari mapema mwezi huo.

  Kukamatwa kwa wafanyakazi wa UN na wafanyakazi wa kandarasi kunafuatia tangazo la hali ya hatari iliyowekwa na serikali mapema mwezi huu.

  Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wappiganaji waasi wa Tigray walitishia kuingia mji mkuu, Addis Ababa.

  Siku ya Jumatatu, msemaji wa UN pia alitangaza kutolewa kwa msaada wa dharura wa dola milioni 40 kwa Waethiopia.

  "Fedha hizi zitasaidia kuipiga jeki oparesheni za dharura katika maeneo yaliyoathiriwa na ghasia huko Tigray na kushughulikia mapema hali ya ukame kusini mwa Ethiopia," msemaji alielezea.

  Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao katika vita vya mwaka mzima kati ya mamlaka ya Ethiopia na wapiganaji waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).

  Mzozo wa Tigray: Kufufuka kwa uasi kunamaanisha nini kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia?

  Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray

  Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu

 3. Jeshi la DRC lashutumiwa na UN kumuua mwanaharakati

  Umoja wa mataifa unalishutumu jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kumpiga mwanaharakati wa haki za binadamu mpaka kufa.

  Cabral Yombo alifariki baada ya kupata majeraha ambayo yalisababishwa na mateso aliyopata kutoka kwa wanajeshi ambao walikuwa wanafuata maelekezo ya viongozi wa eneo hilo, Umoja wa mataifa ofisi ya haki za binadamu imeandika kwenye Twitter.

  Bwana Yombo aliandamana kupinga utozaji ushuru ambao uko kinyume na sheria uliowekwa na chifu Bakano wa mashariki mwa DRC.

  “Nina laani utesaji uliosababisha kifo cha bwana Cabral Yombo...wahusika lazima wawajibishwe”, mbunge wa eneo hilo Juvenal Munobo alinukuliwa na shirika la habari la Reuters.

  Jeshi na viongozi wa eneo hilo hawajajibu bado tuhuma hizo dhidi yao.

 4. UN yashangazwa na Ethiopia kwa kuwafukuza maafisa wake wakuu

  Mamilioni ya watu wamehama makazi yao kutokana na mapigano hayo
  Image caption: Mamilioni ya watu wamehama makazi yao kutokana na mapigano hayo

  Umoja wa Mataifa (UN) imeelezea kushtushwa kwake na hatua ya Ethiopia kuwafukuza nchini humo maafisa wake wakuu.

  Hii ni baada ya Ethiopia kuwapatia maafisa saba wakuu wa Umoja huo muda wa saa 72 kuondoka nchini humo "kwa kujihusisha na masuala yake ya ndani", kupitia ujumbe wa Tweeter kutoka kwa wizara ya mambo ya nje.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema UN inashirikiana na serikali "kwa matarajio kwamba "wafanyikazi walioathiriwa na hatua hiyo wanaweza "kuendelea na kazi yao muhimu".

  Maafisa hao ni pamoja na wakuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, Adele Khodr, na kaimu mkuu wa ofisi ya masuala ya binadamu Grant Leaity,UNOCHA.

  Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulieelezea wasiwasi wake kufuatia ya hatua ya kuwekwa kwa vizuizi vya misaada kufika eneo la Tigray linalokumbwa na mzozo.

  Inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tano kaskazini wanahitaji msaada wa kibinadamu.

 5. DRC: Mwandishi wa kibinafsi wa AFP bado anazuiliwa

  Kwa zaidi ya saa 24 sasa, mwandishi wa kibinafsi wa AFP nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jam Pierre Sosthène Kambidi, bado anasemekana kuzuiliwa katika gerza la kijeshi,tangu siku ya Jumatatu.

  Mwandishi huyo mpekuzi pia anachangia mada katika tuvuti ya Actualité.cd, chombo cha habari mtandaoni DRC.

  Chombo cha habari anachofanyia kazi, kiliandika kikinukuu chanzo kutoka mahakama ya kijeshi kwamba Pièrre Sosthene Kambidi anahojiwa kwa kuwa mtu wa kwanza kuwa na video inayoashiria kuua kwa wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa ambao walitekwa na wanaume waliojihami mnamo March 12, 2017, kati kati ya DRC.

  Raia wa Marekani Michael Sharp na Zaida Catalan, wa Uswidi walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa nchini DR- Congo. Walikuwa wakichunguza mazo katika eneo la Kasaï.

  Zaidi ya vikao 100 vya mahakama vimefanywa tangu kesi hiyo ilipoanza kusikizwa Juni 15, 2017 dhidi ya watu 30 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

  Mzozo wa DRC: Rais Felix Tshisekedi awateua wanajeshi kuwa magavana wa Ituri na Kivu Kaskazini

 6. Video content

  Video caption: Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumanne 21/08/2021

  Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumanne 21/08/2021 na Zuhura Yunus

 7. Rais wa Zambia alisifiwa kwa kusafiri na maafisa 'wachache'

  Rais wa Zambia alisifia timu yake ya kusafiri 'konda'

  Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekuwa akisifiwa mitandaoni kwa kusafirina “maafisa wachahche” kuhudhuria kikao cha 76 za mkutano wa baraza la kuu la umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani .

  Bwana Hichilema alisafiri kwa kutumia ndege ya Qatar Airways fkutoka mjini Lusaka, akiandamana na mawaziri wawili.

  “Kama nilivyoahidi kabala niingie madarakani, utahakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na kwa hivyo tumesafiri na timu konda ambayo inaundwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Fedha, Stanley Kakubo na Dk Situmbeko Musokotwane mtawaliwa, "alisema katika taarifa kabla ya kuondoka.

  "Huyu ni wa kwanza katika eneo ambalo [Rais wa Zimbabwe] Emmerson Mnangagwa na [Lazaro wa Malawi] Chakwera huchukua ndege zilizojaa watu wanaodandia safari", aliandika mwandishi wa habari wa Zimbabwe Hopewell Chin'ono.

  Mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii aliandika: "Afrika inainuka: Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameondoka Zambia kwenda Mkutano Mkuu wa UN, New York kwa kutumia ndege ya kibiashara".

  Rais wa Malawi mnamo Julai alikosolewa kwa kusafiri na familia yake kwa safari ya Uingereza lakini akasema kwamba walihitajika kwa hafla hiyo.

  Hakainde Hichilema: 'Mchunga ng'ombe' aliyeibuka kuwa rais wa Zambia

  Hakainde Hichilema:Tundu Lissu,Raila Odinga na Bobi Wine wanaweza kujifunza yapi kutoka kwake?

 8. Marekani yakaribisha uteuzi wa Obasanjo kuwa mwakilishi wa AU eneo la Upembe wa Afrika

  Obasanjo
  Image caption: Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo

  Marekani imeunga mkono uteuzi wa rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuwa Mawakilishi wa Muungano wa Afrika katika eneo la Upembe wa Afrika.

  Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema Marekani itatoa ushirikiano kuelekea majadiliano ya kumaliza mzozo nchini Ethiopia ambako maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya robo milioni kuishi katika mazingira ya njaa

  Uteuzi wa Olusegun Obasanjo unakuja katika kilele cha mzozo wa miezi 9 katika jimbo la Tigray ambapo Umoja wa Mataifa unasema uhalifu wa kivita umefanywa, na sasa maelfu wanaweza kufa na njaa.

  Utawala wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed uko chini ya shinikizo kujadiliana na Chama cha Tigray People’s Liberation Front, ambacho Ethiopia imetambua kama shirika la kigaidi.