CCM

 1. Rais Samia awa rasmi mwenyekiti mpya wa CCM

  Aboubakar Famau

  BBC News, Dodoma

  CCM

  Rais Samia Suluhu Hassan amepata ushindi wa asilimia mia moja ya wapiga kura wote -avuka kigingi kingine cha Uongozi katika chama ambacho sehemu kubwa ya uongozi wake wa juu ni wanaume.

  Wajumbe 1862 ambao ni sawa na asilimia 99 ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi .

  CCM wamekutana hii leo jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa chama hicho na kumchagua rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyekiti wa Chama hicho.

  CCM

  Rais Samia anajaza nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi na hayati John Pombe Magufuli ambae alifariki tarehe 17 mwezi Machi mwaka huu.

  Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa chama hicho tawala kukutana baada ya kifo Dkt. Magufuli lakini pia ni kikao cha kwanza kwa Samia kuhudhuria kama rais wa Tanzania.

  MM

  Hii ni hatua ya kihistoria katika chama hicho kuongozwa na mwanamke katika nafasi yake ya juu kabisa.

  Wengi wanasubiri kwa hamu kuona ni mabadiliko gani atakayofanya mwenyekiti mpya baada ya kukabidhiwa mikoba ya kukuongoza Chama hicho kikongwe Afrika Mashariki kwa miaka mitano.

  Mabadiliko yanayotarajiwa hivi sasa ni zaidi katika safu ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

  Mbali na kupigwa kura ya mwenyekiti, pia kumekuwa na upigaji kura ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka nafasi mbili ambazo zilikuwa wazi.

 2. CCM kumchagua mwenyekiti mpya bila shamrashamra

  Aboubakar Famau

  BBC News, Dodoma

  SAMIA

  Maelfu ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM wamekutana jijini Dodoma hii leo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho.

  Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa chama hicho tawala kukutana baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Chama.

  CCM

  Mbali na mambo mengine yatakayofanyika, lakini ajenda kuu ya mkutano huo ni pamoja na kuchaguliwa cha mwenyekiti mpya wa Chama ambapo tayari maandalizi yanaonekana kukamilika kwa kumkabidhi rais Samia Suluhu Hassan nafasi hiyo ya juu kabisa katika chama.

  Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa nafasi hiyo kushikiliwa na mwanamke.

  Tofauti na miaka mengine, mkutano mkuu unakuwa na shamra shamra na vifijo, mara hii inaonekana itakuwa tofauti huku Chama hicho kikisema bado kinaomboleza kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania.

 3. Ezekiel Kamwaga

  Mchambuzi

  tz

  Samia amekabidhiwa Uenyekiti wa CCM miezi michache tu baada ya chama chake kuibuka na ushindi katika Uchaguzi Mkuu unaoelezwa kuwa "usiokuwa wa kidemokrasia' kuliko mwingine wowote katika historia ya chaguzi za vyama vingi hapa nchini.

  Soma Zaidi
  next
 4. Philip Mpango athibitishwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania

  Philip Mpango

  Rais Samia Suluhu Hassan amempendekeza Philip Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Maelezo zaidi

 5. Kifo cha Rais John Magufuli:CCM kufanya kikao maalum machi 20

  MAGU

  Wakuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanatarajia kufanya kikao maalumu Jumamosi Machi 20, kufuatia kifo cha mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

  Philip Mangula makamu mwenyekiti Tanzania bara na Mzee Ali Mohamed Shein makamu mwenyekiti Tanzania visiwani wamekubaliana kufanya kikao maalumu na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa Jumamosi katika ukumbi wa Lumumba jijini Dar es salaam.

  Aidha chama kitakuwa katika maombolezo kwa siku 21 sambamba na tangazo la serikali.

  Maelezo zaidi:

 6. Ezekiel Kamwaga

  Mchambuzi

  Aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinanana na rais John Pombe Magufuli

  Mwanzoni mwa mwaka huu, kulikuwa na wasiwasi kwenye duru za CCM kuhusu ni kwa namna gani chama hicho kikongwe zaidi nchini kitashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu ilhali kikiwa na viongozi wenye uzoefu mdogo wa siasa za ushindani.

  Soma Zaidi
  next