Jacob Zuma

 1. Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

  Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa msamaha wa matibabu. Idara ya huduma za marekebisho nchini humo ilitoa taarifa muda mfupi uliopita ikithibitisha kuwa rais huyo wa zamani atamalizia kifungo chake nyumbani.

  Soma Zaidi
  next
 2. Zuma kuruhusiwa kutoka gerezani kuhudhuria kesi

  Rais wa zamani Zuma anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama

  Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ataruhusiwa kuondoka gerezani Jumanne wiki ijayo ili kuhudhurie mwenyewe katika kesi ya ufisafi.

  Uamuzi huu wa mahakama unakuja zaidi ya wiki moja baaada ya zaidi ya watu 300 kuawa wakati wa maandamano yaliyosababishwa na kukamatwa Zuma kwa kukiuaka agizo la mahakama katika kesi tofauti.

  Kua uwezekano wa kupelekwa kwa maafisa wengi wa usalama kwani wafuasi wa Zuma wanatarajiwa kukusanyika katika nje ya mahakama hiyo ya ufisadi katika mji wa Pietermaritzburg - ambao uliathiriwa vibaya na maandamano ya ghasia na uporaji.

  Hii itakuwa mara ya pili Zuma kuonekana hadharani tangu alipozuiliwa mwei uliopita.

  Wiki iliyopita aliruhusiwa kuhudhuria mazishi ya ndugu yake.

  Waendesha mashtaka walikuwa wamependekeza kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya kidijitali - wakitoa sababu za kiusalama.

  Lakini jaji ameridhia ombi la Zuma la kuodoka gerezani na kufika mwenyewe katika mahakama ya Pietermaritzburg.

  Washirika wa Zuma wameshtuhumiwa kwa kujaribu kuongoza ghasia dhidi ya serikali.

  Kesi hiyo inahusiana na makubaliano ya silaha ya miaka ya 1990, na madai kwamba Zuma alipokea hongo. Anakanusha mashtaka yote.

  Soma zaidi:

  Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye uongozi wake ulikumbwa na utata mwingi

 3. Habari za hivi pundeZuma akanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake

  Zuma

  Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekana mashtaka ya ufisadi mwanzoni mwa kesi yake katika mahakama ya Pietermaritzburg.

  Akionekana mdhaifu na kukiongea kwa utulivu, Jacob Zuma alisema NAPINGA makosa yote 18 ya ulaghai, ufisadi, ulaghai, ukwepaji wa kodi na utakatishaji fedha haramu.

  Mashtaka hayo yanahusiana na matukio ya zaidi ya miongo miwili - katika siku za mwanzo za demokrasia ya Afrika Kusini - pamoja na mpango mkubwa wa silaha wenye utata.

  Bwana Zuma na washirika wake wanasisitiza kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.

  Umati wa watu umekusanyika nje ya ukumbi wa mahakama huko Pietermaritzburg kuashiria kuwa Bwana Zuma bado ana umaarufumiongoni mwa wafuasi wake.

  Lakini sasa kuna ushahidi mkubwa wa ufisadi uliofanikiwa katika kipindi cha uongozi wa madarakani, na Waafrika Kusini wengi wanataka kuona haki ikitendeka.

  Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.

  Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.

  Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.

 4. Kesi ya rushwa dhidi Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

  Jacob Zuma

  Kesi ya ufisadi dhidi ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma inatarajiwa kuanza leo, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

  Kiongozi huyo ambaye wakati mmoja aliwahi kusherehekewa kwa mapambanodhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.

  Alidai kuwa mwathiriwa wa hujuma za kisiasa- na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa.

  Bwana Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.

  Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.

  Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.