Mali

 1. Kiongozi wa mapinduzi ya Mali kuapishwa kuwa rais

  Kanali Assimi Goita

  Kanali Assimi Goïta leo anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Mali.

  Ni wiki mbili tangu amuondoe rais wa mpito na waziri mkuu katika mapinduzi - ya pili ndani ya miezi tisa.

  Wiki iliyopita, viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, Ecowas, waliungana na Muungana wa Afrika kufutilia mbali uanachama wa Mali, kutoa wito kwa serikali ya jeshi kuzingatia kipindi cha mpito cha miezi 18 kuelekea uchaguzi mkuu wa urais mwezi Februari.

  Ufaransa na nchi zingine za Magharibi zinataka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

  Mali ni kiungo ni muhimu katika uthabiti wa eneo la Sahel ambalo linakabiliwa na visa vya mara kwa mara vya uvamizi wa kijihadi.

  Maelezo zaidi:

 2. Kiongozi wa mapinduzi ya Mali ajitangaza rais

  MALI

  Kiongozi wa zamani wa Baraza la jeshi nchini Mali, Kanali Assimi Goïta, amejitangaza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya kuwavua madaraka rais wa mpito na waziri mkuu wa zamani.

  Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane sasa wameachiwa huru na jeshi.

  Walipelekwa katika kambi ya kijeshi usiku wa Jumatatu katika hatua ambayo iliifanya Mali kukabiliwa na mapinduzi ya pili ya kijeshi ndani ya miezi tisa.

  Hatua hiyo ilichochewa na mageuzi katika baraza la mawaziri ambapo maafisa wawili wa jeshi waliohusika na mapinduzi ya awali walipoteza kazi zao.

  Kanali Goïta alilalamika kwamba rais aliyeondolewa madarakani hakushauriana naye kuhusu baraza jipya la mawaziri .

  Hali ya taharuki imetanda nchini Mali hivi leo lakini kuna utulivu.

 3. Habari za hivi pundeBaraza la kijeshi nchini Mali lawaachia huru Rais na Waziri Mkuu

  Viongozi wa kijeshi nchini Mali walioipindua serikali wamewaachilia huru Rais wa mpito Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane.

  Waliachiwa huru saa saba usiku wa Alhamisi, Mwandishi wa BBC Noel Ebrin Brou anaripoti.

  Viongozi hao wawili wamekuwa wakizuiliwa katika kambi ya kijeshi tangu Jumatatu.

  Walilazimishwa kujiuzulu baada ya kuvuliwa madaraka na jeshi - mapinduzi ya pili katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika miezi tisa.

  Maelezo zaidi:

 4. Rais na Waziri Mkuu wa Mali wanaozuiliwa 'wajiuzulu'

  Rais wa mpito wa Mali na Mali Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wamejiuzulu rasmi, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

  Bwana Ndaw na Bwan Ouane wamekuwa wakizuiliwa tangu Jumatatu jioni katika kambi ya kijeshi nje ya mji mkuu, Bamako.

  Afisa aliyeongoza mapinduzi ya mwaka jana aliyekuwa makamu wa wa rais wa serikali ya mpito, Col Assimi Goïta, amewalaumu kwa kuzembea katika majukumu yao na kujaribu kuhujumu mchakato wa mpito ya nchi hiyo.

  Ripoti za kujiuzulu kwao zinajiri wakati wapatanishi wa Afrika Magharibi wamewasili nchi humo kujadili kupanga kuachiliwa kwao kutoka kambi ya kijeshi.

 5. Umoja wa Mataifa wataka kuachiwa mara moja kwa Rais wa Mali Bah Ndaw

  Rais Bah Ndaw (kati) anaripotowa kuzuiliwa na na wanajeshi wa Mali karibu na mji mkuu wa Bamako
  Image caption: Rais Bah Ndaw (kati) anaripotiwa kuzuiliwa na wanajeshi wa Mali karibu na mji mkuu wa Bamako

  Ujumbe amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umeagiza kuachiwa huru mara moja kwa Rais wa Mali Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, baada ya taarifa kuibuka kwamba wanazuiliwa na wanajeshi.

  Katika ujumbe wa Twitter ulioandikwa kwa Kifaransa, Minusma pia imetoa wito wa utulivu katika taifa hilo masikini la Afrika Magharibi.

  Kauli hiyo imetokana na ripoti kwamba Rais wa mpito Ndaw na Bw. Ouane walipelekwa na wanajeshi hadi kambi ya kijeshi ya Kati karibu na mji mkuu, Bamako.

  Hali ambayo ilizua wasi wasi wa kutokea kwa mapinduzi ya pili ndani ya mwaka mmoja nchini humo.

  Waziri wa Ulinzi Souleymane Doucouré pia ameripotiwa kuzuiliwa.

  Soma zaidi:

  Jumatatu jioni, Bw. Ouane aliliambia shirika la habari AFP kwa njia ya simu kwamba wanajeshi "walikuja kumchukua". Shirika hilo la habari baadaye ilisema mawasiliano ya simu baadaye yalikatizwa.

  Ripoti ya kuzuiliwa kwa viongozi hao ilikujua saa kadhaa baada ya serikali kufanya mabadiliko ambayo yalipelekea kuondolewa kwa maafisa wawili wa ngazi ya juu jeshini waliohusika katika mapinduzi ya mwaka jana.

  Kwa mara nyingine tena Mali inakabiliwa na hali ya msukosuko miezi tisatu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubakar Keïta.

  Anasema kwamba baadhi ya raia wengi Mali waliunga mkono kuondolewa kwa Bw. Keita- lakini ghadhabu zilipanda tena kutokana na ongezeko la ushawishi wa jeshi katika serikali ya mpito na mwendo wa kinyonga wa mageuzi yaliyoahidiwa.

  Mapinduzi ya mwaka 2012 yalifanya wanamgambo wa Kiislam kuteka maeneo ya kaskazini mwa Mali.

  Vikosi vya Ufaransa vilisaidia kukomboa maeneo hayo lakini mashambulio yaliendelea.

 6. Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

  Watoto

  Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

  Halima Cisse, 25, alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa, Waziri wa Mali Fanta Siby alisema katika taarifa. Alijifungua kupitia njia ya upasuaji.

  Bi Cisse amekuwa akitarajia kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

  Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao “wanaendelea vyema”. Wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

  Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu".

  Mimba ya Bi Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo – huku baadhi yao wakisafiri had Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu, shirika la habari la Reuters liliripoti.

  Msemaji wa wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.