Tunisia

 1. Mhakama yawafunga wabunge wawili wa Tunisia

  Wabunge wawili wa Tunisia wamefungwa jela na mahakama ya kijeshi huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo.

  Wabunge hao wawili ni wa chama cha Karama.

  Wabunge watano wamefungwa kufikia sasa tangu mwezi Julai wakati Rais Kais Saied alipoingia madarakani.

  Nidal Saudi alituhumiwa kumtukana afisa wa usalama wa uwanja wa ndege miezi kadhaa iliyopita.

  Mbunge mwingine Saif Eddine Makhlouf, alituhumiwa kwa kuwatishia majaji na kuwatuhumu kwa kuhusika na mapinduzi wakati alipozuiliwa nafasi ya kumwakilisha Bw. Saudi kama wakili wake.

  Bwana Makhlouf amekuwa mkosoaji wa rais.

  Mnamo mwezi Julai, Rais Saied alifanya mabadiliko serikalini, kusitisha bunge na kuchukua udhibiti wa nchi.

  Wapinzani wake walimshtaki kwa kufanya mapinduzi lakini hatua yake ilipokelewa vyema na raia wa Tunisia.

  Utawala wa Zine al-Abidine Ben Ali Tunisia, anakumbukwa vipi?

 2. Rappa wa Tunisia Swagg Man afungwa jela kwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha

  Swagg Man is known for his facial tattoos

  Msanii Swagg Man, wa Tunisia-Ufaransaamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha .

  Alikamatwa nchini Tunisia mwaka 2019 kwa tuhuma za kuhamisha fedha katika akaunti ya benki ya Uswizi.

  Swagg Man, ambaye jina lake halisi ni Iteb Zaibet, alikuwa ameweka ujumbe katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa anachangisha fedha za kujenga Msikiti, makao ya watoto mayatima na hoteli.

  Lakini kulingana na mtandao wa habari wa Le Courier de Atlas, alilaumiwa kwa kutumia mradi huo kama kisingizio cha kufanya ubadhirifu wa fedha.

 3. Mamia ya vijana wadogo wakamatwa wakati maandamano yakiendelea Tunisia

  Vikosi vya usalama Tunis vyatumia mabomu ya risasi kutawanya waandamanaji

  Polisi nchini Tunisia wamewakamata watu zaidi ya 600 katika maandamano yenye vurugu yalioingia siku ya nne.

  Siku ya Jumatatu, vijana wengi waliokuwa wameandamana walikusanyika tena katikati ya mji wa Tunis, wakirushia polisi mawe na mabomu ya petroli.

  Vikosi vya usalama vilijibu kwa kurusha mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

  Tunisia inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na theluthi moja ya vijana nchini humo hawana kazi.

  Mgogoro wa kiuchumi umeendelea kuzorota kwasababu ya janga la corona.

  Maandamano ya hivi karibuni yanafanyika ikiwa ni miaka 10 tangu kutokea kwa mapinduzi nchini Tunisia yaliodai demokrasia na kusababisha vuguvugu la maandamano katika mataifa ya Kiarabu.

  Hatahivyo, matumaini kuwa maandamano haya yataleta ajira yamefifia.

  Nje ya mji wa Tunis, kumeripotiwa ghasia Jumatatu katika miji ya Kasserine, Gafsa, Sousse na Monastir.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema idadi kubwa ya waliokamatwa tangu kutokea kwa maandamano hayo Ijumaa, ni wenye umri mdogo ambao wamekamatwa kwa makosa ya kusababisha uharibifu na uporaji.

  Khaled Hayouni alisema maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa.

  "Hilo halina uhusiano wowote na maandamano yanayoruhusiwa kisheria na kikatiba," Bwana Hayouni amesema. "Maandamano yanafanyika mchana... bila kutokea kwa vitendo vyovyote vya kiuhalifu ."

 4. Video content

  Video caption: Maandamano ya George Floyd yasambaa hadi Uarabuni

  Maandamano ya George Floyd yasambaa hadi Uarabuni

 5. Video content

  Video caption: Mwanafunzi wa uhandisi asaidia kuunda Barakoa,Tunisia

  Mwanafunzi wa uhandisi ,Taha Grach asaidia Tunisia kwa kutengeza barakoa za muundo wa 3D

 6. Video content

  Video caption: Muigizaji atishiwa maisha yake kwa sababu ya kudansi

  Nermine Sfar muigizaji kutoka nchini Tunisia amesema amepokea vitisho dhidi ya maisha yake kutoka kwa kundi la jihadi baada ya kuanza kupeperusha video za moja kwa moja akicheza