Kilimo

 1. Video content

  Video caption: Mfuga nyuki anayehatarisha maisha yake

  Ericka Thompson ni mfuga nyuki anayewahudumia nyuki bila kuvaa vifaa kinga vyovyote.

 2. Video content

  Video caption: Wanawake wa zambia wanavyotumia baiskeli kurahisisha shughuli zao za kila siku

  Kama hauna gari na barabara ni mbovu sana basi inakua vigumu kupeleka bidhaa sokoni au kufika shuleni. Je baiskeli ni jibu ? Watu hawa wa Zambia wanahisi hivyo

 3. Rihana

  India imeshutumu ''raia wa kigeni'' na watu maarufu kwa ujumbe waliotoa mtandaoni baada ya mwanamuziki Rihanna, kutangaza kuwaunga mkono wakulima wanaoandamana, hali iliyosababisha suala hilo kutolewa macho na jumuia ya kimataifa.

  Soma Zaidi
  next
 4. Magufuli awataka wakulima wa taifa hilo kulisha dunia baada ya corona

  Rais Magufuli wa Tanzania.

  Rais wa Tanzania John Magufuli, amesihi wakulima nchini humo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula akibashiri uhaba wa chakula duniani baadaye mwaka huu kwasababu ya janga la virusi vya corona.

  Aliwataka wakulima kutumia vizuri fursa ya kupungua kwa uzalishaji kwa nchi ambazo huwa ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwasababu ya masharti ya afya yaliyowekwa kote duniani.

  "Mwaka huu kuna uwezekano wa kutokea kwa baa kubwa la jaa duniani kwasababu watu wengi wanazingatia hatua za kutotoka nje kujikinga dhidi ya corona, lakini hilo halistahili kutukatisha tamaa kwasababu hata sheria hizo zikiwekwa bado watahitaji kula, tutakuza mazao na kuyauza," amezungumza na wananchi kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba.

  Rais wa Tanzania amekuwa akikosolewa kwa kutozingatia sana ukubwa wa madhara ya janga la corona, na kusema mara kadhaa kwamba mgogoro wa afya umekuzwa na kukejeli wanaovaa barakoa.

  Mnamo mwezi Juni alitangaza kuwa nchi hiyo "haina virusi vya corona" kwasababu ya maombi ya wananchi.

  Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonesha wasiwasi wake juu ya mkakati wa serikali ya nchi hiyo katika kukabiliana na Covid-19.