VVU/Ukimwi

 1. Marekani inazingatia kusambaza dawa za kupunguza makali ya Ukimwi zilizokwama Kenya

  Dawa za kupunguza makali ya Ukimwi

  Marekani inapania kupeleka dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ambazo zimekwama katika bandari ya Kenya katika nchi zingine zinazohitaji, ubalozi wake nchini Kenya unaesema.

  Dawa hizo ziliwasili nchini Kenya mwezi Januari na zimekwama katika bandari ya Mombasa kutokana na mzozo unaoendelea wa kodi na vibali.

  Ubalozi wa Marekani umesema unahofia muda wa mwisho wa matumizi ya dawa hizo,na huenda ikawa rahisi kupeleka dawa hizo katika nchi nyingine kutumika.

  Serikali ya Kenya iliondolea ushuru dawa hizo lakini afisa wa mamlaka uya ukusanyaji kodi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema kwambabaadhi ya makontena bado zinasubiri kibali kutoka kwa shiriki la dawa.

  Afisa kutoka shirika la madawa anasema kibali kipya kinahitajika kuombwakwani ya awali inasema mpokeaji ni Shirika la Kenya la usambazaji madawa.

  Mfadhili, USAid,imepatia kampuni ya kibinafsi kusambaza dawa hiyo wakati serikali inataka shirika lake la usamazaji dawa kusimamia mpango huo.

  Zaidi ya watu milioni 1.5 wanaoishi na virusi HIV wanahitaji dawa hizo na zimekuwa zikitolewa kwa mgao katika vituo vya afya ili kikidhi mahitaji hayo kwa muda.

 2. Tahadhari yatolewa dhidi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi Kenya

  kenya

  Zaidi ya pakti 24,000 za dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi zilizosambazwa katika majimbo 31 ​​nchini Kenya zina athari kubwa kwa wale wanaozitumia.

  Wanaharakati wa maswali ya HIV wanasema matumizi ya dawa hizo zenye thamani ya bilioni shilingi 1.2 yalisitishwa nchini humo mwaka 2019.

  "Kwa nini serikali inacheza na maisha ya watu? Tumewaambia mara nyingi sana kwamba dawa hizi hazifanyi kazi kwa sababu madhara ambayo yamehusishwa nayo. " Nelson Otuoma, mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watu wanaoishi na VVU aliiambia BBC kwa simu.

  Dawa iliyosimamishwa ni ile ya Zidovudine / Lamivudine / Nevirapine. Dawa hizi ni miongoni mwa dawa zilizotolewa kama msaada kwa nchi kutoka kwa mfumo wa ule Global Fund na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Usaidizi wa Virusi vya HIV (PEPFAR).

  “Tumeshangazwa sana kwamba dawa hizi zilikuwa bado kwenye ghala kwa miezi. Walituambia kuwa zilikuwa zimeshaharibiwa.” Otuoma aliongeza.

  Kwa kawaida, dawa ya Nevirapine, utolewa kama dawa moja au kama mchanganyiko wa kipimo cha dawa tatu.

  Madhara ya dawa hii kwa kawaida ni maumivu ya tumbo, upele, uchovu, maumivu ya kichwa, kutapika na maumivu ya misuli, ambayo huenda baada ya mwezi mmoja.

  Nevirapine imehusishwa pia na uharibifu wa ini kwa watu wengine. Nchi nyingi zimesitisha matumizi yake kwa watu wanaishi na HIV.

  Shirika la Afya duniani WHO limesema kwamba matibabu ya msingi wa Nevirapine yalikuwa yameonesha kiwango kikubwa cha kutopunguza makali ya virusi vya ukimwi mwilini,

  Mwaka wa 2015, shirika hilo lilipendekeza nchi kutumia dawa ijulikanayo kama Dolutegravir kama tiba mbadala ya laini ya kwanza kwa watu wazima na vijana.

 3. Mwanamke mwenye ukimwi anayewasaidia wengine 'kufa kifo kizuri'

  Thembi Nkambule

  Thembi Nkambule amekuwa akiwahudumia mamia ya watu wanaofariki kutokana na Ukimwi Eswatini - nchi ambayo mtu mmoja kati ya wanne ana HIV. Haya ndio mambo aliyojifunza juu ya maana ya "kifo kizuri".

  Soma zaidi