Muungano wa Ulaya - EU

 1. "Kemikali za milele " zipo katika bidhaa mbali mbali za nyumbani

  Hebu tazama katika bidhaa unazozitumia kila siku zinazokusaidia kurahisisha maisha yako ya kila siku... Je uliwahi kujiuliza ni kwanini vyakula havinati kwenye kikaango chako, na ni kwanini mafuta huwa hayagandi kwenye microwave, au ni kwanini maji hayawezi kupenya kwenye jaketi lako?.

  Soma Zaidi
  next
 2. Marekani na EU zalaani mashambulio ya angani Tigray

  The airstrike is believed to have left dozens killed and others injured
  Image caption: The airstrike is believed to have left dozens killed and others injured

  Muungano wa Ulaya na Marekani zimelaani mashambulio ya angani yanayosemekana kutekelezwa na vikosi vya anga vya Ethiopia, yaliyowajeruhi raia katika soko moja karibu na mji mkuu wa Jimbo la Tigray, Mekelle.

  EU imetaja tukio hilo kuwa la ''kutia wasiwasi" baada ya raia kulengwa na kuuawa "kimakusudi" .

  Jeshi la Ethiopia limepinga kulenga raia lakini limethibitisha oparesheni yake mpya dhidi ya Tigray People’s Liberation Front (TPLF), inafanywa kupitia mashambulio ya angani.

  Marekani imetoa wito wa kufanywa kwa uchunguzi huru na kuomba waathiriwa wapewe huduma za afya.

  Mzozo wa Tigray umekumbwa na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili.

  Shambulio la angani la Togoga linaaminiwa kusababisha vifo vya makumi ya yawtu na wengine kadhaa kujeruhiwa. Shirika la kimataifa la Malaba Mwekundu lemsema kuwa limesaidia kuwaondoa waliojeruhiwa.

  Kuna hofu ya kuongezeka kwa mapigano makali katika maeneo tofauti ya Tigray kati ya waasi na majeshi ya Ethiopia, yakisaidiwa na vikosi vya Eritrea, itasababisha kuzorota zaidi kwa mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo, kwani mashirika ya misaada sasa yanakabiliwa na vizuizi vipya kufikia mamilioni walioathiriwa na vita hivi.

  Kulingana na mashirika ya misaada, mamia ya maelfu ya watu, bado hawawezi kupatikana kwa sababu ya mzozo unaoendelea, hali inayowaweka katika hatari ya kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

 3. EU yafuta mpango wa kutuma waangalizi wa uchaguzi wa Ethiopia

  Umoja wa Ulaya EU, umefuta mpango wa kuwatuma waangalizi wake katika uchaguzi wa Ethiopia utakaofanyika mwezi Juni kwa "kutoafikiana kuhusu masuala kadhaa muhimu".

  Mwakilishi Mkuu wa Muungano huo Josep Borrell amesema viwango vinavyohitajika kama vile uhuru wa waangalizi na kuingiza nchini humo vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya usalama wao umezuiliwa.

  "Inasikitisha kwamba EU haujapewa hakikisho kuhusu kwamba watu wa Ethiopia watapata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo kwa njia ya kidemokrasia," aliandika katika taarifa iliyowekwa mtandaoni:

  View more on twitter

  EU imetoa wito kwa serikali ya Ethiopia kuendesha uchaguzi huru na wa haki.

  Muungano huo umesema utaunga mkono kwa bodi ya uchaguzi kwa euro milioni 20 ($24m; £17m).

  Ethiopia inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu Juni 5. Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na janga la corona.

  Jimbo la Tigray lilipuuza hatua ya serikali na kufanya uchaguzi wake.

 4. Tazama daraja la watembea kwa miguu lililo refu zaidi duniani

  Video content

  Video caption: Ilichukua miaka miwili kujenga daraja hili kwa gharama ya dola milioni 2.8
 5. Burundi yawapokea wawakilishi wa EU

  Ndayishimiye
  Image caption: Rais wa Burundi Everiste Ndayishimiye

  Burundi na Muungano wa Ulaya (EU) zimekubali kurejelea tena mashauriano kwa lengo la kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya kusitishwa miaka mitano iliyopita, ofisi ya rais imetangaza.

  Rais Evariste Ndayishimiye siku ya Jumatatu alikutana na wawakilishi wa EU nchini Burundi pamoja na mabalozi kutoka nchi za Ulaya.

  Pande hizo mbili "zilikubaliana kusahau yaliyopita na kuangazia siku zijazo kwa kujenga upya uhusiano wao", kwa mujibu wa afisi ya rais.

  Burundi ilikuwa imeilaumu EU kwa "kudhamini misukosuko" nchini humo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi Mei mwaka 2015. EU ilikatiza msaada wa bajeti kwa serikali kutoka na kile ilitaja kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

  Rais Pierre Nkurunziza alikuwa madarakani wakati huo. Alifariki mapema mwaka huo na nafasi yake kuchukuliwa na rais Ndayishimiye.

  Balozi wa EU mjini Bujumbura Claude Bochu ameweka picha ya mkutano huo katika Tweeter yake, na kusema kuwa ulifanyika katika "mazingira tulivu na ulikuwa wa kufana".

  View more on twitter