Sudan

 1. Waandamanaji wa Sudan wakubali kuanza tena usafirishaji wa mafuta

  Protesters from the Beja community blocked two crucial oil pipelines

  Serikali ya mpito ya Sudan imefikia makubaliano na waandamanaji ambao walifunga mabomba mawili muhimu ya usafirishaji mafuta mashariki mwa nchi na kukatiza usambazaji wa mafuta ndani na nje ya nchi.

  Waandamanaji hao kutoka jamii ya Beja ambayo imekuwa ikiandamana kwa wiki kadhaa, ilikuwa imeiziba bomba linalosafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini na nyingine ambayo inashughulikia mafuta ambayo hayajasafishwa kuingia Sudan.

  Jamii hiyo ilikuwa imekasirika kwa kuachwa nje ya mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya serikali na makundi kadhaa ya waasi mwaka jana kama sehemu ya mabadiliko ya muda mrefu kutoka kwa utawala wa kijeshi hadi utawala wa raia nchini.

  Ujumbe kutoka mamlaka ya mpito siku ya Jumapili ulifanya mazungumzo na waandamanaji.

  Hatua hiyo ilifuatiwa na makubaliano ya muda na wazee wa jamii ya Beja kuruhusu usafirishaji wa mafuta kupitia bandari ya Bashayer, kituo kikuu karibu na Bandari ya Sudan ambako shughuli ya usafirishaji wa nje ya Sudan Kusini hufanyika.

  Wazee wa jamii ya Beja wamesema wanahitaji wiki moja, baada ya makubaliano hayo ya muda, ili kujadili zaidi suala hilo.

 2. Sudan: Wanajeshi wa Ethiopia 'walirudishwa nyuma' baada ya kujaribu kuingia al-Fashaga

  Wakuu wa jeshi la Sudan wameapa kushikilia eneo hilo linalozozaniwa (picha ya maktaba)
  Image caption: Wakuu wa jeshi la Sudan wameapa kushikilia eneo hilo linalozozaniwa (picha ya maktaba)

  Sudan inasema imezima jaribio la majeshi ya Ethiopia "kuingia" katika himaya yake.

  Mkuu wa majeshi ya Sudan, Jeneral Abdel Fattah al-Burhan, amesema hii inaonesha jinsi majeshi inavyolinda nchi hiyo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka wiki iliyopita.

  Katika taarifa yake, Sudan ilisema tukio hilo lilifanyikakatika wilaya ya Umm Barakit.

  Jeshi la Ethiopia halijajibu ombi la BBC la kutoa maoni.

  Lakini kituo cha Habari cha al- Jazeera kinanukuu serikali ya Ethiopia ikisema:"Tunakanusha harakati za vikosi vyetu kwenye mpaka wa Sudan au kuingia kwao katika eneo lolote."

  Umm Barakit liko katika eneo la mpakani la al-Fashaga linalozozaniwa, ambako hali ya taharuki imeonezeka.

  Ramani

  Kwa miongo kadhaa, raia wa Ethiopia wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo katika ardhi hiyo yenye rotuba inayodaiwa na Sudan.

  Uhusiano kati ya Sudan na Ethiopia umezorota zaidi tangu Ethiopia ilipoanza kujaza maji katika bwawa iliyojenga katika Mto Nile na vita kuzuka katika eneo lake la Tigray.

  Katika miezi ya hivi karibuni, mapigano yameripotiwa mara kadhaa katika eneo la al-Fashaga.

  Kwanini Ethiopia, Sudani wanapambania al-Fashaga?

  Bwawa la mto Nile:Maji ya mto huu yanatishia kuleta vita kati ya Misri,Ethiopia na Sudan

 3. Mapinduzi yaliyotibuka Sudan: Serikali yawalaumu wandani wa Bashir

  Kiongozi wa Sudan

  Sudan inasema watu walio na uhusiano na Rais Omar al-Bashir aliyeng'olewa madarakani wamehusika na jaribio la mapinduzi lililotibuka Jumanne.

  Msemaji wa serikali alilaumu "nguvu za giza" akiongeza kuwa wale waliohusika wamekamatwa.

  Bashir, ambaye amekuwa madarakani kwa miongo mitatu aling'olewa uongozini miaka miwili iliyopita.

  Utawala wa sasa- unaojumuisha jeshi, wawakilisha wa kijeshi na makundi ya waandamanaji - ulibuniwa kama sehemu ya makubaliano ya ugawanaji mamlaka.

  Wapangaji wa mapinduzi walijaribu kuchukua jengo la utangazaji la shirika la habari la serikali, Shirika la habari la AFP linaripoti.

  Ripoti za awali kutoka mji mkuu wa Khartoum ana mji ulio karibi wa Omdurman izilielezea shughuli nyingi za kijeshi katika kanda ya mto Nile na daraja kuu la kuvuka mto Nile lilikuwa limefungwa.

  Barabara ya kuelekea Khartoum na bandarini pia imefungwa.

  "Haturudi nyuma... kuna watu wanajaribu kuturudisha nyuma," alisema Waziri wa Habari Hamza Baloul katika taarifa iliyosomwa katika televisheni ya kitaifa TV, ikilaumu "mabaki" ya utawala wa zamani kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi ya Jumanne.

  Sudan: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 4. Habari za hivi pundeJaribio la mapinduzi Sudan latibuka-Mamlaka

  TL

  Serikali ya Sudan inasema kumekuwa na jaribio la mapinduzi lililotibuka katika nchi hiyo na hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti.

  "Kumekuwa na jaribio la mapinduzi lililoshindwa, watu wanapaswa kukabiliana nalo, "Shirika la habari la AFP linanukuu ripoti zikisema.

  Kulikuwa na jaribio la kuchukua jengo ambalo lina vyombo vya habari vya serikali, Shirka la habari la AFP linasema likiashiria chanzo cha serikali.

  Msemaji wa serikali amesema shughuli ya kuwahoji wanaoshukiwa kuwa nyuma ya jaribio hilo la mapinduzi itaanza muda mfupi ujao.

  Msemaji huyo aliyenukuliwa na mashirika ya habari ya kimataifa anasema wapangaji wa mapinduzi walijaribu kuchukua udhibiti wa redio ya Serikali huko Omdurman, ng'ambo ya mto Nile kutoka mji mkuu Khartoum.

  Maandamano yalikuwa yamepangwa kufanyika mjini Khartoum leo na wanajeshi walikuwa wametumwa kushika doria mitaani wakati mapinduzi hayo yalipojaribiwa.

  Serikali ya mpito ya Sudan ambayo imekuwepo tangu 2019 imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kuleta mageuzi ya kiuchumi na kisiasa licha ya madai yanayokinzana kutoka kwa maeneo ya kihafidhina na yale huria.

  Sudan: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 5. Sudan yaidhinisha kwa kauli moja mswada wa kujiunga na mahakama ya ICC

  Sudan iliahidi haki kwa wahanga wa uhalifu uliofanywa Darfur wakati wa utawala wa Bashir
  Image caption: Sudan iliahidi haki kwa wahanga wa uhalifu uliofanywa Darfur wakati wa utawala wa Bashir

  Baraza la mawaziri la mpito la Sudan limepitisha kwa kauli moja muswada ambao utaiandalia njia ya kujiunga na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ameandika katika ujumbe wa Twitter Jumanne.

  Rasimu hiyo imeidhinishwa kwa maandalizi ya mkutano wa pamoja kati ya Baraza Kuu la Uongozi na baraza la mawaziri ili kuipitisha kuwa sheria.

  "Haki na uwajibikaji ni uti wa mgongo wa Sudan mpya, ambayo imejitolea kwa sheria ambayo sote tunataka kuijenga," Bwana Hamdok alisema.

  Hatua hii imesongeza Sudan karibu na kuwakabidhi washukiwa wa ICC wanaotafutwa kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari katika eneo la magharibi mwa Darfur, akiwemo Rais wa zamani Omar al-Bashir.

 6. Miili zaidi yapatikana ikielea kwenye mto wa mpaka wa Ethiopia na Sudan

  Mto huo unatiririka kutoka eneo la Tigray lililokumbwa na mzozo nchini Ethiopia
  Image caption: Mto huo unatiririka kutoka eneo la Tigray lililokumbwa na mzozo nchini Ethiopia

  Daktari katika mji wa mpakani wa Sudan ambako maiti kadhaa zilipatikana zikielea juu ya mto anasema ameona miili zaidi ikielea juu ya maji.

  Dkt. Tewodros Tefera anasema binafsi ameona miili 12 inayofikisha 30 jumla ya maiti zilizoopolewa majini siku chache zilizopita katika mto Setit (ambao pia unafahamika kama Tekeze).

  Eneo hilo linakaribia mpaka wa Sudan-Ethiopia, na mto huo unapitia eneo la Tigray nchini Ethiopia ambako kumekuwa na mapigano ya miezi kadhaa.

  BBC imeona kanda ya video ya moja ya miili iliyopatikana asubuhi.

  Soma zaidi:

 7. Miili kadhaa yapatikana ikielea mtoni katika mpaka wa Tigray-Sudan

  Jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia limekumbwa na mapigano tangu Novemba
  Image caption: Jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethipia limekumbwa na mapigano tangu mwezi Novemba

  Makumi ya miili imepatikana katika mto unaoashiria mpaka kati ya Ethiopia na Sudan, wakaazi wa upande wa Sudan wameripoti.

  Baadhi ya miili ilikuwa na majeraha ya risasi na mikono kufungwa.

  Mto Setit unaofahamika Ethiopia kama Tekeze unapitia eneo la Tigray linalokumbwa na mzozo kaskazini mwa Ethiopia ambako vikosi vya serikali na washirika wake wanapigana na waasi wa Tigray.

  Mhudumu wa afya ambaye alitorokea nchini Sudan ameiambia shirika la Habari la Reuters kwamba alikizika miili 10 katika wiki moja iliyopita. Anasema miili mingine 28 iliopolewa, ikiwemo saba siku ya Jumatatu.

  Shirika la habari la AP limemnukuu afisa wa Sudan akisema mamlaka katika mkoa wa Kassala ilikuwa imepata miili 50, inayodaiwa kuwa ya watu wanaotoroka vita.

  Serikali ya Ethiopia haijatoa tamko rasmi kuhusiana na miili hiyo. Akaunti ya Twitter inayoendeshwa na serikali hapo jana iilisema kampeini ya "propaganda" kuhusu "mauaji feki" huko Humera – ambako mto Tekeze unapitia- "imefufuliwa tena kwa kutumia picha za uwongo zinazoonesha picha za kikatili”.

  Mapigano katika eneo la Tigray yalianza mwezi Novemba kati ya utawala wa jimbo hilo Tigray People's Liberation Front (TPLF), na serikali ya muungano.

  Vita hivyo vya miezi minane vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu huku maelfu ya watu wakikabiliwa ha hali ya njaa.

 8. Kiongozi wa Sudan aonya juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kutetea mageuzi

  Abdalla Hamdok alikua waziri mkuu mnamo Agosti 2019
  Image caption: Abdalla Hamdok alikua waziri mkuu mnamo Agosti 2019

  Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, ameonya kwamba nchi hiyo huenda ikatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuwaelekezea kidole cha lawama wandani wa karibu wa utawala uliopita.

  Amesema marekebisho ambayo amekuwa akitekeleza yalilenga kuboresha uchumi

  Kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta imesababisha maandamano kote nchini.

  "Kuzorota kwa hali ya usalama kunahusishwa sana na mgawanyiko uliokumba masuala yaliyofikiwa wakati wa mapinduzi, ambayo yaliacha ombwe linalotumiwa na maadui zake na wafuasi wa serikali ya zamani'', Bw. Hamdok alinukuliwa na shirika la Reuters.

  Sudan imepongezwa kwa mageuzi yake ya kiuchumi tangu rais wa zamani Omar al-Bashir alipong’olewa madarakani mwaka 2019.

  Hata hivyo kumekuwa na upungufu wa chakula unaohusishwa na mizozo ya muda mrefu na majanga ya asili kama ukame na njaa.