Yoweri Museveni

 1. Rais wa Uganda aonya polisi dhidi ya kutekeleza ukatili

  Polisi wa Uganda wameshtumiwa kwa ukatili
  Image caption: Polisi wa Uganda wameshtumiwa kwa ukatili

  Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameshutumu kile alichokitaja kuwa utovu wa nidhamu unaotekelezwa na vikosi vya usalama vinavyowatesa au kuwapiga raia wa Uganda wa kawaida.

  Bwana Museveni ameongeza kuwa vikosi vya usalama vinavyowatesa washukiwa ni wavivu na hawataki kufanya uchunguzi stahiki na kukusanya ushahidi wa kutosha unaohitajika.

  Wakati wa hotuba yake ya kitaifa iliyopeperushwa kupitia televisheni, picha za video za washukiwa waliokamatwa kwa kumpiga risasi Waziri wa Ujenzi Jenerali Katumba Wamala, ambao wanadaiwa kuteswa wakiwa kizuizini, zilichezwa.

  Rais alisema ukatili "utaharibu uhalali wetu" na kuongeza kuwa "hakuna mtu anayepaswa kumpiga raia yeyote wa Uganda. Matumizi ya "mateso" sio lazima na ni makosa".

  "Kwanini umpige mtu? Kwasababu wewe ni mvivu sana wa kuwahoji. Ni wahalifu lakini mateso ni makosa", rais alisema.

  Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine amemshutumu rais kwa kutokuwa mkweli katika matamshi yake juu ya ukatili unaotekelezwa na polisi.

  "Ninaweza kufikiria jinsi waathiriwa waliofanyiwa unyama chini ya uongozi wake wanavyohisi wakati wanamwona bila aibu yoyote akizungumza uongo, bila kujali kabisa matatizo yao. Kwa nyinyi nyote wahanga wa mateso, muliowekwa kizuizini kinyume cha sheria na waliotekwa nyara, ninaweza kuhakikishia kwamba kutakuwa na siku haki itatendeka", Bw. Kyagulanyi amenukuliwa na tovuti ya habari ya Nile Post akisema.

  Bwana Kyagulanyi amekuwa mwathirika wa ukatili unaotekelezwa na polisi mara kadhaa.

  Mnamo mwezi Januari, shirika la Human Rights Watch lililitoa wito kwa vikosi vya usalama vya Uganda kukomesha tabia ya matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi ambao ulighubikwa na vurugu na vitisho dhidi ya wapinzani.

 2. Uganda yarekodi viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya virusi vya corona

  Doses of Uganda's first batch of Covid vaccine are fast running out

  Uganda imeandikisha viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya virusi vya corona kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu janga la hilo lilipoanza.

  Watu 1,438 kati ya 8,478 waliambukizwa virusi kulingana na takwimu iliyotolewa na Wizara ya Afya siku ya Alhamisi. Vipimo vilifanywa tarehe 8 mwezi Juni.

  Nchini hiyo imekuwa ikikabiliwa na aina mpya ya virusi ambayo viligunduliwa kwanza nchini India, Uingereza, na Afrika Kusini ikiwemo kirusi kingine kilichogunduliwa China.

  Kuna wasi wasi visa vya maambukizi vinaendelea kuongezeka na hospitali huenda zikalemewa kwa kukosa vifaa tiba muhimu kama vile oksijeni.

  Shirika la ndege la kitaifa la Rwanda RwandAir limesitisha safari zake kwenda Uganda kutokana na ongezeko la maambukizi.

  Siku ya Jumatano, Milki ya Falme za Kiarabu zilisema kwamba wasafiri kutoka Uganda, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hawataruhusiwa kuingia nchini humo kuanzia Ijumaa hii.

  Zaidi ya watu 750,000 wamepewa chanjo ya corona nchini Uganda kufikia sasa.

  Nchi ilikuwa imepokea dozi 964,000 za chanjo ya AstraZeneca mnamo mwezi Machi, ambayo inaelekea kuisha.

 3. Rais Museveni ateua baraza jipya la mawaziri

  Yoweri Museveni
  Image caption: Rais Museveni awateua wanawake 10 katika baraza lake jipya la mawaziri.

  Rais wa Uganda Yoweri Museveni amefanya uteuzi wa baraza jipya la mawaziri 31 na manaibu waziri 50.

  Baraza hilo linajumuisha wanawake 10.

  Jessica Alupo, ambaye ni meja mstaafu wa jeshi, ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Ni mwanamke wa pili katika historia ya nchi hiyo kuteuliwa katika wadhifa huo. Alupo aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Elimu.

  Robinah Nabbanja, afisa wa ngazi ya juu wa chama tawala, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Alikuwa naibu waziri wa afya.

  Rebecca Kadaga, wakili na mwanasiasa wa zamani ambaye hadi uteuzi wake katika baraza la mawaziri alikuwa spika wa bunge amepewa wadhifa wa naibu waziri mkuu wa kwanza. Pia amepewa jukumu kusimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Baraza hilo la mawaziri pia linajumuisha maafisa wapya kutoka jeshini. Kamanda Mkuu wa sasa wa Majeshi, Jenerali David Muhoozi, ndiye naibu waziri wa mambo ya ndani. Jenerali eneral Muhoozi pia anawakilisha jeshi bungeni .

  Mmoja wa mawakili wa kibinafsi wa rais, Kiryowa Kiwanuka, ameteuliwa kuwa Mawanasheria Mkuu.

  Sam Kuteesa, ambaye amekuwa Waziri wa Uganda wa Mambo ya nje kwa muda mrefu, ameondolewa katika baraza la mawaziri.

  Jinsi Museveni alivyoitawala Uganda miaka 35

 4. Uganda yafunga shule siku 42 kudhibiti maambukizi ya Covid 19

  Nchi hiyo imekuwa ikiripoti ongezeko la maambukizi
  Image caption: Nchi hiyo imekuwa ikiripoti ongezeko la maambukizi

  Uganda imefunga shule zote pamoja na taasisi za elimu ya juu kwa siku 42 kufuatia wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona.

  Nchi hiyo ilifunga shule zote mwezi Machi 2020, na kuzifungua kwa awamu tangu mwezi Oktoba. Lakini wanafunzi wa shule za msingi na upili walikuwa hawajarejea wote shuleni.

  Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumapili, Rais Yoweri Museveni alisema waalimu wote sasa watahitajika kuchanjwa kabla ya kuruhusiwa kurejea kazini.

  Walikuwa wamejumuishwa katika kundi la kwanza la watu walioshtahili kuchanjwa wakati nchi hiyo ilipozindua kampeni ya chanjo ya corona mwezi Machi mwaka huu.

  Mikusanyiko yote ya kisiasa imesitishwa isipokuwa mikutano ya bunge na mahakama.

  Mikusanyiko ya umma pia imesitishwa kwa siku 42. Ni watu 20 watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi au mazishi.

  Usafiri wa umma na wa kibinafsi kutoka kutika wilayani kuingia jiji kuu la Kampala zitapigwa marufuku kuanzia tarehe 10 mwezi Juni. Magari ya kusafirisha mizigo hayataathiriwa na marufuku hiyo.

  Shughuli nyingi za kiuchumi zitaendelea kama kawaida lakini hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zitaimarishwa.

  Nchi hiyo imethibitisha ongezekola hali ya juu ya maambukizi ya corona katika wiki mbili zilizopita ikilinganishwa na miezi iliopita.

  Jumla ya watu 1,259 wamethibitishwa kuambukizwa, kiwango cha juu zaidi kurekodiwa tarehe 4 Juni tangu janga la corona lilipoatangazwa.

 5. Uganda kutenengeza chanjo ya Covid -19

  Isack Mumena

  BBC Swahili Kampala

  Mtu akidungwa chanjo

  Serikali ya Uganda imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Covid 19 kama mataifa mengine duniani.

  Mwaka jana Rais Yoweri Museveni alisema wanasayansi wa Uganda wanajaribu kufanya utafiti kuanza kutengeneza chanjo yao na tiba ya Covid-19 ambayo tayari iko kwenye majaribio.

  ''Ninafanya kazi na watu wangu kuanza kutoa chanjo yetu, sio kwamba tumekaa tu kusubiri watusaidie, tumechelewa lakini sasa tumeanza na chanjo yetu itakwenda kote duniani'' alisema Rais Museveni.

  Aliendelea kusema: ''Tutaanza kufanyia majaribio panya mwezi wa Juni kuona kama ina madhara na baadae mwezi wa Augosti tutafanyia majaribio nyani na kusubiri kudhibitishwa na WHO.''

  Museveni na mke wake

  Rais Museveni ametowa kauli hiyo wakati alipodungwa sindano ya chanjo ya Covid-19 ya Astra Zeneca pamoja na mkewe Janet Museveni, katika ikulu ya rais Nakasero mjini Kampala.

  Bw. Museveni aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata chanjo kwani haina madhara.

  Soma zaidi:

  Rais Museveni na mkewe Janet wapata chanjo ya Corona