Wapenzi wa Jinsia Moja

 1. Kituo cha wapenzi wa jinsia moja chafungwa Accra Ghana

  Ghana still criminalises same-sex relations
  Image caption: Ghana haijahalalisha uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja

  Polisi nchini Ghana wamefunga kituo cha kuwahudumia wapenzi wa jinsia moja ambacho kilifunguliwa hivi karibuni katika mji mkuu wa Accra, kufuatia malalamishi ya umma.

  "Hatuwezi tena kufikia eneo letu salama na usalama wetu unatishiwa. tunomba mashirika ya kutetea haki za binadamu, na washirika wao kuangazia shambulio hili na uhalifu wa chuki tunaotendewa," Wanaharakati wa kutete haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Ghana walisema kwenye mtandao wa Twitter.

  View more on twitter

  Makundi ya kutetea haki, ikiwemo Muungano wa Haki sahihi za Kijinsia, Binadamu na Maadili ya Familia pamoja na Kongamano la Maaskofu wa katoliki Ghana (GCBC), yamekuwa yakishinikiza serikali kufunga kituo hicho.

  Kilifunguliwa kupitia hafla ya mchango wa fedha uliohudhuriwa na wanadiplomasia kadhaa wa Muungano wa Ulaya (EU) na wakigeni.

  Picha za kufunguliwa kwa kituo hicho zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimezua hisia mseto.

  Soma zaidi:

 2. Papa 'aashiria kuunga mkono' ndoa za watu wa jinsia moja

  Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kwamba anafikiria wapenzi wa jinsia wanastahili kuruhusiwa "kuoana".

  Maelezo zaidi:

  Papa Francis
  Image caption: Papa Francis