Ukristo

 1. Illustration of William Gallagher

  Kwa wasikilizaji wake , William Neil "Doc" Gallagher alifahamika kama daktari wa pesa "Money Doctor" - mtu mwenye pesa ambaye alitangaza huduma zake kwenye radio ya Kikristo , iliyotangaza kote nchini Marekani kutoka kile kilichoitwa ukanda wa Biblia- 'Bible Belt' eneo lote la North Texas.

  Soma Zaidi
  next
 2. Video content

  Video caption: Tanzania:Utamaduni wa Kisukuma unaounganisha Ukristo na tamaduni asili

  Tamasha la utamaduni wa kisukuma Bulabo ambalo hufanyika kila mwaka nchini Tanzania huleta pamoja shughuli za utamaduni na zile za kikristo

 3. Mkenya ashtakiwa Uingereza kwa kuuza kile alichokiita dawa ya corona

  Askofu Wiseman anaendesha kanisa la Bishop Climate Ministries ambalo ni sehemu ya Kingdom Church
  Image caption: Askofu Wiseman anaendesha kanisa la Bishop Climate Ministries ambalo ni sehemu ya Kingdom Church

  Mhubiri mzaliwa wa Kenya anayeishi Uingereza amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kuuza kile alichokiita 'dawa' ya Covid-19.

  Askofu Irungu Wiseman wa kanisa la Bishop Climate aliuza chupa zenye mchanganyiko wa mafuta moja ikiwa ni pauni 91.

  Alishtakiwa katika mahakama moja mjini London kwa udanganyifu na makosa ya ukosefu wa utendaji haki katika biashara.

  Hata hivyo, alikanusha mashitaka hayo.

  Bwana Wiseman alitengeneza video na kuzisambaza mtandaoni akidai mafuta hayo ni tiba ya Covid-19.

  Hadi kufikia sasa, hakuna tiba ya Covid-19, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

  Bwana Wiseman anaendesha kanisa la Bishop Climate Ministries ambalo ni sehemu ya Kanisa la Kingdom Church lililoko London Kusini.

 4. Shepherd Bushiri

  Watu wanapiga makofi, wengine wanacheza densi na wengine wakirukaruka juu huku akiingia katika ukumbi , akiandamana na walinzi wake.

  Soma Zaidi
  next
 5. Reverend Paul Obayi holds an idol

  Muhubiri mmoja wa kanisa katoliki anaendesha jumba la makumbusho mashariki mwa Nigeria ili kuhifadhi sanamu na vifaa vingine vinavyochomwa na wahubiri wenzake wa kanisa la Pentecostal ambao wanaziona kama njia ya kuabudu sanamu.

  Soma Zaidi
  next
 6. TB Joshua kuzikwa 'kanisani'

  TB Joshua

  Kanisa la Mhubiri Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza siku na mahali atakapozikwa.

  Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN, lilisema Mhubiri TB Joshua atazikwa karibu na makao yake makuu mjini Lagos.

  Mhubiri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

  "Tunajiandaa kwa ibada ya kila wiki kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua." taarifa ilisema.

  TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

  TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.

  Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.

  TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Amerika Kusini.