Utafiti wa Kimatibabu

 1. Video content

  Video caption: ‘Kihisio’ kwenye ubongo kinachosababisha urefu wa binadamu, kwa mujibu wa utafiti

  Sasa Wanasayansi wanasema kwamba fumbo la wanadamu kuwa warefu na kufikia balehe mapema

 2. Madaktari wa Marekani wajaribu kupandikiza figo ya nguruwe kwa binadamu

  Nguruwe
  Image caption: Wataalam wanasema ni jaribio la hali ya juu zaidi katika uwanja huo hadi sasa.

  Madaktari nchini Marekani wanasema kuwa wamefanikiwa kumpa figo ya nguruwe mtu kwa njia ya upandikizaji katika hatua ambayo inaweza kusaidia kupunguza uhaba mkubwa wa viungo vya kupandikiza.

  Utaratibu uliofanywa katika Kituo cha afya ch NYU Langone mjini New York, Marekani ulihusisha utumiaji wa nguruwe ambaye jeni zake zilibadilishwa ili kuendana naya mwanadamu na cha kufurahisha ni kwamba haikukataliwa na kinga ya mwili wa binadamu.

  Mpokeaji alikuwa mgonjwa ambaye ubongo ulikua umekufa na dalili ya kupona ambaye familia yake ilikubali afanyiwe jaribio hilo kabla ya kutolewa kwenye mashine ya kumsadia kuishi, watafiti waliiambia Reuters.

  Kwa siku tatu figo hiyo mpya ilipandikizwa kwenye mishipa yake ya damu na kuwekwa nje ya mwili wake ili kuwawezesha watafiti kuifikia.

  Utafiti huo haujakaguliwa au kuchapishwa lakini kuna mipango ya kufanya hivyo inaendelea.

  Kutumia nguruwe kwa upandikizaji sio wazo jipya ikwani sehemu ya moyo wa nguruwe tayari hutumiwa sana kwa wanadamu.

  Na viungo vyao ni mechi nzuri kwa watu linapokuja suala la ukubwa.

  Upandikizaji figo unavyoweza kuokoa maisha

  Hiba aliachwa na figo moja baada ya kutapeliwa na wauza viungo vya binadamu Misri