Nzige Afrika Mashariki

 1. Kifo cha Rais Magufuli: Marais 10 kumuaga hayati John Magufuli

  MAGU

  Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt.Hassan Abbas amethibitisha uwepo wa marais 10 katika shughuli za kuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri, uliopo mji mkuu wa Tanzania Dodoma.

  Marais hao ni kutoka Kenya, Zambia, Zimbabwe, Morocco, Namibia, Malawi ,Botswana , Afrika Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

  Kwa upande wa waliotuma wawakilishi ni Waziri Mkuu wa Rwanda, waziri wa mambo ya nje wa Angola, Makamu wa Rais wa Burundi pamoja na wawakili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuia ya Muungano wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, Mabalozi na kutoka Umoja wa Mataifa.

 2. Video content

  Video caption: Jinsi nzige wanavyotumiwa kwa faida nchini Kenya

  Shirika moja lisilo la kiserikali (NGO) nchini Kenya linatoa mafunzo kwa jamii ya kuwakamata nzige, ili kuwageuza kuwa chaula cha wanyama.

 3. Hofu baada ya nzige kuvamia mkoa wa Kilimanjaro

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Nzige
  Image caption: Wananchi wameonywa kutowakula nzige hao au kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyopuliziwa dawa

  Kundi la Nzige waharibifu wa jangwani limeingia wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro Kaskazini mwa Tanzania na kuibua hofu ya uharibifu wa mazao ya chakula.

  Wilaya hiyo inazalisha mazao mbali mbali ya chakula na kibiashara kama mahindi, mboga, maharage na mengineyo.

  Sio mara ya kwanza kwa uvamizi wa kuripotiwa katika wilaya ya Siha, siku za hizi karibuni.

  Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo kikosi cha wataalamu kinaendelea na kazi ya kuwanyunyizia dawa wakitumia ndege mkoani Arusha kwenye wilaya za Longido na Simanjiro ambapo waliripotiwa mwishoni mwajuma.

  Tayari Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda na jopo la wataalamu wameshafika mkoani Kilimanjaro kutathimini athari na kuweka mikakati ya kuwaangamiza wadudu hao ambao huzalia kwa wingi na kwa muda mfupi.

  Nzige

  Wilaya zilizoshambuliwa awali hazikuwa na hofu kubwa ya uharibifi wa mazao kwani makundi hayo yalishambulia zaidi maeneo ya malisho ya mifugo.

  Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema kazi ya kuwadhibiti bado inaendelea kwani wadudu hao waharibifu walivamia maeneo ya malisho na tayri asilimia kubwa ya eneo hilo limeshapuliziwa dawa ambayo kwa mujibu wa wataalamu matokeo yake huanza kuonekana ndani ya saaa 24 hadi 72.

  Wananchi wameendelea kuonywa kuwa waangalifu kutokula au kuokota nzige hao au kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyopuliziwa dawa, huku shule zikiendelea kufungwa kupisha zoezi hilo.

  Soma zaidi:

 4. Tanzania kutumia ndege mbili kupambana na nzige

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Nzige

  Serikali nchini Tanzania imetangaza kuanza kutumia ndege kunyunyizia dawa makundi ya nzige yaliyovamia wilaya ya Longido na Simanjiro wakitokea nchini Kenya.

  Taarifa za kuingia kwa wadudu hao waaribifu zilitolewa kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa na mkuu wa wilaya hiyo Frank Mwaisambe ambaye anasema ndege ya Shirika la Chakula Duniani FAO inayotokea Nairobi inatarajiwa kuanza kazi ya kunyunyuzia dawa leo.

  Ndege ya serikali ya Tanzania nayo itaungana nayo mara tu rubani wake atakaporejea kutoka Ethiopia alikokwenda kusaidia kupambana na nzige pia.

  Aidha mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa mpaka sasa hakujawa na madhara yoyote kwani eneo lililovamiwa kwa kiasi kikubwa ni pori lakini pia asilimia kubwa ya nzige hao bado ni wadogo.

  Mwaka jana makundi makubwa ya nzige yalivamia maeneo kadhaa nchini Kenya na Ethiopia na kuibua hofu ya kutokea kwa baa la njaa kutokana uharibifu mkubwa walioufanya.

  Maelezo zaidi:

  Namna nzige mmoja anavyosababisha baa

 5. Kenya 'kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya corona mwezi ujao'

  Kenya na Uingereza zakubaliana juu ya upatikanaji wa chanjo ya corona

  Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford mwezi ujao, kulingana na shirika la habari la Reuters.

  Waziri wa Afya Mutahi Kagwe nchini Kenya amesema kuwa chanjo hizo ziliagizwa kupitia mpango wa Umoja wa Afrika.

  Waziri wa mambo ya nje Uingereza, Dominic Raab, ambaye yuko nchini humo kwa ziara ya siku moja, amenukuliwa akisema Uingereza ilikuwa inasaidia Kenya kujitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo.

  View more on twitter

  "Ni wajibu wetu sio tu kimaadili, lakini ni kwa maslahi ya Uingereza kuona raia wa Kenya wakipata chanjo hiyo haraka iwezekanavyo kadri ya uwezo wetu," Bwana Raab amenukuliwa akisema.

  Kenya ina idadi ya watu takriban milioni 48, kulingana na takwimu ya idadi ya watu mwaka 2019. Na hadi kufikia sasa nchi hiyo imethibitisha maambukizi 99,308 ya virusi vya corona huku watu 1,130,707 wakifanyiwa vipimo vya virusi hivyo.

  Pia, watu 82,478 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo wa corona huku idadi ya vifo ikiwa 1,734.

 6. Ethiopia yaimarisha vita dhidi ya makundi ya nzige

  Nzige wamevamia nchi kadhaa za Afrika Mashariki
  Image caption: Nzige wamevamia nchi kadhaa za Afrika Mashariki

  Waziri wa Kilimo wa Ethiopia, Oumer Hussien, amesema ndege zaidi za kunyunyiza dawa zitapelekwa kukabiliana na makundi ya nzige wanaovamia mashamba nchini humo.

  Hii ni baada ya ndege za kupuliza dawa kuanguka mapema mwezi Oktoba na kurudisha nyuma jitihada za kupambana na wadudu hao waharibifu.

  Waziri amesema nzige katika maeneo manne wamepulizwa dawa kwasababu wamekuwa tishio kwa usalama wa chakula nchini Ethiopia.

  Amesema Wizara inaendeleza mchakato wa kubaini mashamba yaliyoathiriwa zaidi na uvamizi wa nzige ili kuwapa usaidizi wenye mashamba hayo.

  Nzige walionekana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki ambako wamesababisha uharibifu wa mimea.

  Wataalamu wametaja uvamizi wa sasa wa nzige kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 60.

 7. Vifurushi 21 vya msaada wa Jack Ma 'havikufika' Kenya

  Misaada kutoka kwa Jack Ma kwa ajili ya kukabiliana na corona
  Image caption: Misaada kutoka kwa Jack Ma kwa ajili ya kukabiliana na corona

  Mamlaka nchini Kenya imekiri kwamba mchango muhimu katika vita dhidi ya Covid-19 kutoka kwa bilionea wa China Jack Ma haikuwasili nchini.

  Naibu wa waziri wa uchukuzi wa, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya.

  Bwana Obure alisema hayo siku ya Alhamisi mbele ya kamati ya bunge ya afya japo hakudokeza ni vifaa vya aina gani vilikuwa ndani ya vifurushi hivyo.

  Aliongeza kuwa vifaa hivyo havikuwahi kuwawasili nchini kutoka Ethiopia ambako misaada ya Jack Ma katika eneo hilo ilitumwa kwa ajili ya kusambazwa katika nchi zingine.

  Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure.

  Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Jack Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha.

  Maelezo zaida:

  Je msaada wa Jack Ma Afrika una umuhimu gani katika kupambana na janga la corona?

 8. Waziri wa Afya Kenya Mutahi Kagwe

  Idadi ya wagonjwa wa virusi vya coroa nchini Kenya imeongezeka na kufikia 7,577 baada ya wagonjwa 389 wapya kuripotiwa. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema siku ya Jumamosi kwamba kati ya wagonjwa watatu ndio sio raia wa Kenya

  Soma Zaidi
  next