Libya

 1. Wabunge nchini Libya waidhinisha kura ya kutokuwa na imani na serikali

  Bunge la Libya limepitisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

  Utawala - unaoongozwa na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah - uliwekwa madarakani mapema mwaka huu kama sehemu ya juhudi za kuleta amani zilizosimamiwa na Umoja wa mtaifa

  Serikali hiyo ilitazamiwa kutoa nafasi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Disemba.

  Lakini hali ya taharuki imeibuka baina ya kambi mbili hasimu baada ya spika wa bunge - ambalo makao yake yako mashariki mwa Libya - kuridhia sheria tata ya uchaguzi.

  Wengine waliona hatua hiyo ni ya kumpendelea kamanda wa makao ya mashariki, Jenerali Khalifa Haftar.

  Libya: Mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam yuko hai ataka kuongoza Libya

  Muammar Gaddafi :Miaka 10 baadaye Mwanawe Gaddafi anaweza kufaulu kuongoza Libya?

 2. Video content

  Video caption: Mamluki nchini Libya: 'Huu ni ufalme wa mlengaji shabaha wa Urursi'

  Tangu wakati huo, serikali mbili hasimu zimegawanya nchi hiyo kuwa magharibi na mashariki.

 3. ’’Kasri la angani’’ la Gaddafi latua nyumbani Libya baada ya muongo

  Libya Prime Minister/ Facebook

  Ndege ya kibinafsi ya kiongozi wa zamani wa Libya Hayati Muammar Gaddafi imetua katika mji mkuu wa Libya Tripoli baada ya karibu muongo mmoja ikiwa nchini Ufaransa, vimeripoti vyombo vya habari vya Libya na vya Kiarabu.

  Ndege hiyo kubwa, aina ya Airbus A340, ilipaa juu ya anga la Tripoli kabla ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Mitiga karibu na mji mkuu, iliripoti televisheni ya Arab Al Arabiya TV.

  Vyombo mbali mbali vya habari vilinukuu kauli za Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibah, ambaye alikuwa katika uwanja wa ndege kushuhudia ndege hiyo ikiwasili jana usiku.

  Amesema kuwa ukarabati wa ndege hiyo na taratibu nyingine vimekamilika, na serikali ya mpito imelipia gharama zilizohitajika kuirejesha Libya, ilitangaza ofisi ya Waziri mkuu kwenye ukurasa wake wa Facebook.

  Bw. Dbeibah alisema kwamba ndege nyingine 14 aina ya jet zilizosalia, 12 kati yake zimepangiwa kurejea Libya, huku serikali ikishughulikia kurejea kwa ndege mbili bora zaidi.

  Kulingana na televisheni ya Al Arabiya, jet ya Gaddafi, ambayo inafahamika pia kama "Kasri inayopaa", ilipaa kimo cha chini juu ya mji wa Tripoli na kuyazunguka maeneo kabla ya kutua ardhini.

  Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ndege hiyo, Bw Dbeibah alisema "watu wa Libya ndio watakaoamua hatma yake" na kama itatumiwa na maafisa au wengine, manufaa ya umma, kulingana na Al Arabiya.

  ndege

  Alisema kuwa kurejea kwa ndege hiyo maarufu nchini ni "hatua nzuri kwa Libya, usalama wake na utajiri", ilisema televisheni hiyo.

  Ndege hiyo ya kifahari, ilielezewa na baadhi kama "ndege ya Airbus yenye muonekano wa nyumba ya [James] Bond ndani ", ilivivutia vyombo vya habari vya kimataifa kwa miaka iliyopita.

  Gaddafi – ambaye aliiongoza Libya kwa miongo sita-na ambaye anafahamika kama kiongozi aliyekuwa na nguvu za mamlaka kibinafsi ambaye alionekana katika jukwaa la dunia kama mwenye mtindo wake wa uongozi, aliuawa katika mji wa nyumbani kwa wa Sirte mwezi Oktoba 2011 wakati wa mzozo ulioibuka kufuatia uasi mwezi Aprili mwaka huo.

  Mamlaka ya serikali mpya ya Libya, Serikali ya Umoja wa kitaifa(GNU) inayoongozwa na Bw Dbeibah, iliinga mamlakani baada ya kuchukua mamlaka kutoka kwa serikali iliyokuwa na makao yake mjini Tripoli na iliapishwa mwezi Machi kufuatia uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu katika mchakato uliodhaminiwa na Umaoja wa Mataifa.