Nelson Mandela

 1. Afisa wa ANC aliyefurushwa chamani 'amsimamisha kazi' Rais Ramaphosa

  ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno
  Image caption: ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno

  Ace Magashule, katibu mkuu wa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini, ameJIBU hatua ya kutimuliwa kwake chamani kwa kumsimamisha kazi Rais Cyril Ramaphosa kama mkuu wa chama hicho.

  "Mimi pia, kwa kuzingatia mamlaka niliyopewa kama katibu mkuu wa ANC, na kwa kutii kikamilifu maazimio ya mkutano wa chama, namsimamisha kazi kwa muda rais wa ANC, Ndugu Cyril Ramaphosa, " Bw. Magashule alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

  Naibu katibu mkuu wa chama, Jessie Duarte, hata hivyo amesema Bw. Magashule hana mamlaka ya kumpatia rais barua ya kumsimamisha kazi na anaweza kufanya hivyo yeye binafsi bila uungwaji mkono wa chama.

  Bw. Magashule amesema atakata rufaa kupinga uamuzi wa kumfuza chamani "unaokiuka katiba" - na kusisitiza atasalia katika nafasi yake hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.

  ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno na kuonya wanachama wengine wanaokabiliwa na mashtaka ya ufisadi kwamba watafuata mkondo huo endapo hawatajiuzulu ndani muda wa mwezi mmoja.

  Bw. Magashule amepinga mashtaka ya ubadhirifu, ufisadi na utakatishaji fedha yanayomkabili.

  Soma zaidi:

 2. Nelson Mandela

  Leo ni siku ambayo Nelson Mandela anaadhimisha miaka 30 tangu alipoachiliwa kutoka gerezani wakati wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini. NI siku inayotumika kumuenzi na kutambua mafanikio yake.

  Soma Zaidi
  next