Mitandao ya Kijamii

 1. Video content

  Video caption: "Ninacheza vyombo vyote bendi yangu ya muziki ya Ireland"

  Caitríona Lagan ana uwezo wa kucheza ala tano za muziki kwa wakati mmoja

 2. Video content

  Video caption: Meghan Ghimifre: Msichana asiye na mikono anayehamasisha wengine Tiktok

  Anasema kwamba ‘anafurijika’ watu wanapomwambia kuwa video zake zinawapa motisha.

 3. Mkuu wa Twitter aweka bendera ya Nigeria mtandaoni- Kunani

  Mkuu wa Twitter

  Mkuu wa Twitter Jack Dorsey ameweka ujumbe wenye picha ya bendera ya Nigeria mtandaoni katika hatua ambayo vyombo vya habari nchini humo vinaashiria ni kuunga mkono maandamano ya Jumamosi dhidi ya uongozi mbaya na kulalamikia kufingiwa kwa Twitter.

  Ujumbe wa Bw. Dorsey umewavutia Wanageria wengi wanaotumia mtandao wa VPN kufikia programu hiyo tumishi.

  Twitter inajadiliana na serikali ya baada ya kupigwa marufuku nchini humo tarehe 5 mwezi Juni.

  Marufuku hiyo ilifuatia hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari lakini ofisi yake imesema hatua hiyo haihusiani kivyovyote na suala hilo.

  Raia wa Nigeria siku ya Jumamosi waliandamana kulalamikia uongozi mbaya, ukosefu wa demokrasia na kupigwa marufuku kwa Twitter.

  Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji na kuwakamata baadhi yao,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

  Maandamano ya Jumamosi ni ya kwanza tangu maandamano ya #EndSARS ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanywa kwa wiki kadhaa.

  Soma zaidi:

  Serikali hufanikiwa vipi kufunga au kubana mtandao?

 4. Nigeria yataka wenye mitandao ya kijamii kupata vibali vya ndani

  Nigerian authorities suspended Twitter five days ago

  Kampuni za mitandao ya kijamii ambazo zinataka kuendesha shughuli zao nchini Nigeria sasa zitahitajika kujisajili nchini humo na kupewa leseni na tume ya utangazaji.

  Waziri wa mawasiliano,Lai Mohammed, ametoa tangazo hilo kufuatia hatua ya serikali kupiga Twitter marufuki siku tano iliyopita.

  Mtandao huo wa kijamii ulifuta ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria zake lakini ofisi ya rais imepinga madai kwamba marufuku hiyo ilikuwa hatua ya kilipiza kisasi.

  Baadhi ya vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Nigeria vimepuuza amri ya kufunga akaunti zao za Twitter na kuamua kufikia mtandao huo kupitia mtandao wa VPN.

 5. Nigeria 'yajadiliana na Twitter' baada ya marufuku

  Twitter

  Nigeria imesema inajadiliana na Twitter,baada ya kuufungia mtandao huo wa kijamii wikendi iliyopita.

  Baada ya kukutana na wanadiplomasia, Waziri wa Mambo ya nje wa wa Nigeria Geoffrey Onyeama amesema serikali inafuatilia jinsi mazungumzo yanavyoendelea kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya ziada.

  Katika hatua ya hivi punde dhidi ya Twitter, mamalaka imeagiza vyombo vyote vya habari kujiondoa katika mtandao huo.

  Wanadiplomasia wa Magahribi wamekosoa marufuku hiyo wakisema uhuru wa kijieleza ni sehemu muhimu ya democrasia.

  Serikali ya Nigeria imechukua hatua ya kufungia mtandao huo baada ya Twitter kuondoa ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari wa kutishia kundi linalotaka kujitenga.

  BBC ilizungumza na Gbenga Sesan wa Mpango wa Paradigm, ambao unatoa fursa za kidijitali kwa vijana kote Afrika, ambaye anasema marufuku ya serikali imefeli.

  Maelezi zaidi: