Katoliki

 1. Tanzania 'kuchunguza wizi wa kikombe cha Ekaristi'

  Police are still investigating how the cup disappeared from the church
  Image caption: Polisi bado wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka kutoka kanisani

  Kikombe cha Ekaristi Takatifu kutoka kanisa moja la katoliki nchini Tanzania kimeibiwa, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

  Wizi wa kikombe hicho cha Ekaristi kilicho na thamani ya dola 2,150 ulitokea Jumapili iliyopita katika Parokia ya Mkoka, iliyopo mji Mkuu wa Dodoma.

  Polisi wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka katika majengo ya kanisa.

  Aidha hakuna kitu kingine kilichoibiwa kutoka kanisani humo.

  Na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kutokana na wizi huo, gazeti hilo limemnukuu mkuu wa usalama wa eneo hilo.

 2. Video content

  Video caption: Kanisa Katoliki Tanzania latahadharisha juu ya wimbi jipya la corona

  Kanisa Katoliki nchini Tanzania limetoa tahadhari juu ya wimbi jipya la maambukizi ya corona na kuwataka wananchi kuchukua hatua zote za kujikinga.