Maandamano

 1. Blinken alaani ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa Sudan

  Anthony Blinken

  Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Anthony Blinken, amelaani ghasia dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia nchini Sudan na kusisitiza wito wa kutaka waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Abdalla Hamdok arejeshwe kazini.

  Siku ya Jumatano watu 15 waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya wakati vikosi vya usalama vilipofyatua risasi dhidi ya umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga mapinduzi ya mwezi uliopita.

  Katika mahojiano na BBC Bw Blinken, ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu aingie madarakani, alitaka wafungwa wa kisiasa waachiliwe na kusema viongozi wa kijeshi wanahitaji kusikiliza vilio vya watu wa Sudan.

  Mazishi ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika saa chache zijazo.

  Mapinduzi ya Sudan:Jeshi la Sudan lavunja serikali ya kiraia na kuwakamata viongozi

  Sudan: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 2. Jeshi lapelekwa katika shule Eswatini

  Wanajeshi walisambazwa katika maeneo ya mijini wakati wa ghasia mwezi wa Julai
  Image caption: Wanajeshi walisambazwa katika maeneo ya mijini wakati wa ghasia mwezi wa Julai

  Wanajeshi na polisi wamepelekwa katika shule zote katika Eswatini ambako wanafunzi wamekuwa wakifanya maandamano kwa muda wa wiki moja kudai mageuzi ya kisiasa.

  Shule za msingi na sekondari katika nchi hiyo pekee ya Kiafrika inayotawaliwa Kifalme zamani ikifahamika kama Swaziland, wamekuwa wakisusia kuingia madarasani na kufanya mgomo baridi kwa mwezi mzima uliopita.

  Hapo nyuma, maandamano ya wanaounga mkono demokrasia yalikuwa yakifanyika katika maeneo ya mijini, lakini katika kipindi cha mwaka hivi -maandamano hayo yamekuwa yakionekana miongoni mwa jamii za vijijini-ambako kwa kawaida wamekuwa walimuunga mkono Mfalme.

  Maafisa wa usalama wamekuwa wakionekana katika miji mikuu ya Eswatini-Mbabane na Manzini.

  Maafisa wanasema wamepelekwa kusaidia kuimarisha amani lakini wanafunzi waandamanaji wanaamini ni kuwatisha.

  Maandamano ya wanafunzi ya wiki hii ni ya hivi karibuni katika miezi ya hivi karibuni ya ghasia katika ufalme huo mdogo.

  Wanatoa wito wa hali bora za kusoma na elimu ya bure. Wanasema gharama ya elimu katika shule za taifa haipatikani kwa wengi-katika nchi ambazo karibu 25% ya watu wazima hawana ajira.

  Waandamanaji, ambao wamekuwa wakikusanywa na makundi ya wanafunzi, pia wanadai kuachiliwa kwa wabunge wawili waliokamatwa wakati wa maandamano ya kudai demokrasia mapema mwaka huu.

  Mfalme Mswati III aliwahi kuwashutumiwa na wanaharakati kwa kutumia ghasia kuwanyamazisha wapinzani wake wa kisiasa-baadhi wanaona kusambazwa kwa wanajeshi kama sehemu ya kutekeleza nia hiyo.

  Ufalme wa Eswatini ni mojawapo ya nchi masikini zaidi barani Afrika-wakosoaji wake wanamshutumu kwa kuishi maisha ya anasa huku watu wake wakikabiliwa na njaa kila siku.

  Wachambuzi wa siasa wanasema maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ni ishara ya kutaka mabadiliko nchini-kwamba watu wanaendelea kutofurahia utawala uliopo sasa madarakani.

 3. Habari za hivi pundeKesi ya Mbowe yaahirishwa Polisi watawanya wafuasi wake mahakamani

  Wafuasi wa Chadema nje ya mahakama ya kisutu
  Image caption: Wafuasi wa Chadema nje ya mahakama ya kisutu

  Polisi jijini Dar es Salam wamewatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

  Kesi hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa nia ya mtandao hata hivyo imeahirishwa kutokana na changamoto za kimawasiliano. Mbowe anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho asubuhi kuendelea na kesi hiyo.

  Awali wafuasi wa Chadema walionekana nje ya mahakama hiyo wakiwa na mabango yaynaosema: 'Mbowe sio gaidi’ na pia walikuwa wakipaaza sauti na kusema, ‘katiba mya sio ugaidi’.

  Hata hivyo polisi waliwatawanya wafuasi hao na baadhi yao kukamatwa.

  Video content

  Video caption: Polisi watawanya wafuasi wake mahakamani na kuwakamata wengine
  Waandamanaji
  Waandamanaji
  Waandamanaji

  Mawakili wa Mbowe wakiongozwa na Peter Kibatala , wapo mahakamani hapo lakini mteja wao ni mahabusi katika gereza la Ukonga.

  Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kufadhili vitendo vya kigaidi.

  Wakosoaji wa serikali ikiwemo Chadema pamoja na mashirika ya haki za kibinadamu wanaichukulia kesi hiyo ni ya kisiasa na kushinikiza serikali imwachie huru mwanasiasa huyo.

  Hata hivyo polisi wamekanusha madai hayo na kwamba wanasema wana ushahidi wa kutosha kwamba Mbowe alitenda makosa hayo na kutaka mahakama iachwe itekeleze wajibu wake.

  Soma zaidi:

 4. Uporaji Afrika Kusini: Lori za Msumbiji zachomwa moto

  mm

  Lori zinazomilikiwa na raia wa Msumbiji zimeporwa na kuchomwa moto na waandamanaji katika nchi jirani ya Afrika Kusini, chama cha wasafirishaji mizigo Msumbiji kinasema.

  Shirikisho la Chama cha Usafiri Barabarani (Fematro) linasema hakuna majeruhiwa au vifo vilivyoripotiwa miongoni mwa madereva.

  Kisa hicho kilitokea mjini Durban, mkoa wa KwaZulu-Natal, ana kwengineko mkoani Gauteng, alisema Constantino Jotamo, mkurugenzi wa Fematro director.

  "Tunatafuta maelezo zaidi kuhusu kile kilichotokea," alisema

  Madereva wanahofia hali huenda ikaendelea kuwa mbaya zaidi katika siku zijazo.

  "Siku chache zilizopita zimekuwa ngumu sana,” anasema Rui Muianga, dereva wa lori katika barbara ya Maputo-Johannesburg.

  Siku ya Jumanne, ni magari matatu pekee ya usafiri wa umma ziliondoka Msumbiji hadi Afrika Kusini

 5. Mwanahabari wa Chad atoweka baada ya kuangazia maandamano

  Mwanahabari mmoja nchini Chad ametoweka siku kadhaa baada ya kuangazia taarifa ya maandamano, kundi la kutetea haki za binadamu nchini humo limesema.

  Moïse Dabsene alikamatwa wakati wa maandamano ya tarehe 20 na kuachiliwa siku hiyo hiyo.

  Familia yake imenukuliwa na kundi la Chad CTDDH ikisema kwamba mara ya mwisho yeye kuonekana ilikuwa tarehe 25 Machi.

  Kundi hilo linasema hayuko katika kituo chochote cha polisi na kutoa wito aachiliwe huru ikiwa amekamatwa.

 6. Televisheni za Senegal zafungwa kwasababu ya kuangazia maandamano

  Wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Senegal walikabiliana na polisi
  Image caption: Wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Senegal walikabiliana na polisi

  Mamlaka nchini Senegal zimesitisha matangazo ya vituo viwili vya televisheni za kibinafsi baada ya kuzilaumu kwa kuangazia zaidi maandamano yaliyosababishwa na kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko.

  Vituo viwili vilivyoathirika na uamuzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Matangazo nchini humo ni Sen TV na Walf TV.

  Vituo hivyo vimeshutumiwa kwa upeperushaji wa picha zinazoonesha maandamano baada ya Bwana Sonko kukamatwa, Shirika la habari la AFP limeripoti.

  Siku ya Alhamisi, polisi walikabiliana na wafuasi wa Bw. Sonko mjini Bignona kusini mwa eneo la Casamance.

  Serikali imethibitisha kuwa mtu mmoja aliuawa siku ya katika ghasia za Alhamisi zilizotokana na kukamatwa na Bw. Sonko mjini Dakar mapema siku hiyo.

  Bw. Sonko amelaumiwa kwa kumbaka mwanamke mmoja katika saluni ambako alikwenda kusingwa.