Familia

 1. Kiongozi wa 'familia kubwa zaidi duniani' afariki nchini India

  Ziona Chana

  Mwanamume wa miaka 76- anayeamiiwa kuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani amefariki katika jimbo la Mizoram, nchini India.

  Ziona Chana, mkuu wa dhehebu la kidini ambalo linaunga mkono ndoa ya wake wengi, alifariki Jumapili, na kuwaacha wake 38, watoto 89 na wajukuu 36.

  Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Waziri Mkuu Kiongozi wa jimbo la Mizoram, Zoramthanga,ambaye alitoa salamu zake za rambi rambi katika mtandao wa Twitter "kwa masikitiko makubwa ".

  View more on twitter

  Chana aliripotiwa kuugua ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu

  Madaktari waliiambia shirika la habari la PTI kwamba hali ya Chana ilikuwa mbaya zaidi nyumbani kwake katika kijiji cha, Baktawng Tlangnuam. Alilazwa hospitali Jumapili jioni ambako alithibitishwa kufariki alipofikishwa.

  Ni vigumu kubainisha ikiwa kweli Chana alikuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani kwa kuwa kuna wengine ambao wamedai taji hilo.

  Pia ni vigumu kukadiria ukubwa wa familia ya Chana. Ripoti moja ilidai alikuwa na wake 39, watoto 94, wajukuu 22 na kitukuu mmoja, ambao kwa jumla ni watu 181.

  Wakati ripoti kadhaa za habari nchini humo zimemtaja kuwa anashikilia "rekodi ya ulimwengu" kwa familia kubwa kama hiyo, haijulikani ni rekodi gani ya ulimwengu.

  Imeripotiwa pia kuwa familia hiyo imeangaziwa mara mbili kwenye kipindi maarufu cha Ripley's Amini au la.

 2. Video content

  Video caption: Je sera ya mtoto mmoja inaweza kukoma katika zama za kizazi kipya China?

  Je sera ya mtoto mmoja inaweza kukoma katika zama za kizazi kipya China?