Vyombo vya Habari

 1. Mwanamke na Mwafrika kwa kwanza kuongoza WTO aitwa "Bibi" na gazeti la Uswizi

  Ngozi Okonjo-Iweala,
  Image caption: Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala

  Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala, amekaribisha uamuzi wa mdhibiti wa vyombo vya habari wa Uswizi ambao ulipata kichwa cha habari kinachomfafanua kama "bibi" baada ya uteuzi wake kuongoza bodi hiyo yenye kuegemea ubaguzi wa kijinsia.

  Gazeti la Aargauer Zeitung lilikuwa na kichwa cha habari kinachosoma: "Bibi huyu atakuwa mkuu wa WTO", baada ya Bi Okongo-Iweala kuteuliwa mnamo mwezi Machi.

  Gazeti hilo liliomba msamaha baada ya kukososlewa vikali kutokana na kichwa chake cha habari na kusemekana kwamba kilikuwa "kisichofaa".

  Bi. Okonjo-Iweala, Mnigeria-Mmarekani, ni mchumi msomi wa chuo kikuu cha Harvard na anayeheshimika.

  Bi. Okonjo-Iweala, 67, ndiye Mwafrika na mwanamke wa kwanza kuongoza WTO.

  Alituma ujumbe Alhamisi kwamba Baraza la Wanahabari la Uswisi lilikuwa sawa kupaza sauti juu ya ubaguzi wa kijinsia.

  Katika uamuzi wake Jumanne, mdhibiti wa vyombo vya habari alisema kuwa wameshindwa kubaini ikiwa kuna upendeleo wa ubaguzi wa rangi.

  "Hata hivyo, ... ni dhahiri kwamba ikiwa hii ingemhusu waziri wa zamani wa fedha na waziri wa mambo ya nje mwanamume katika nchi ya watu milioni 200, kichwa cha habari 'Babu awa mkurugenzi mkuu wa WTO'hakingeweza kutumika", tovuti ya habari ya Barron iliripoti.

  Ngozi Okonjo-Iweala kuweka historia ya mwanamke na mwafrika wa kwanza kuongoza WTO

 2. Video content

  Video caption: 'Tutazingatia kuwa na sheria isiyokwaza ya upatikanaji na usambazaji habari'

  Baraza la habari Tanzania: 'Tutazingatia kuwa na sheria isiyokwaza ya upatikanaji na usambazaji habari'

 3. Rais Samia ataka uhuru wa vyombo vya habari uheshimiwe

  ikulu

  Rais wa Tanzania Bi.Samia Suluhu Hassan amesema ni muhimu kusimamia vyombo vya habari vya ndani.

  Rais Samia amesema "nasikia kuna vyombo vya habari vilivyofungiwa fungiwa na TV za mikono, vifungulieni na vifuate sheria na muongozo wa serikali".

  Aliongeza kusisitiza kuwa ;"Tusiwape mdomo wa kusema kuwa tunaminya uhuru wa vyombo habari."

  Aidha Rais Samia amesema wahakikishe kuwa kila atakayepewa ruhusa ya kuendesha chombo cha habari anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi kuwa kosa ili adhabu yake ilingane na adhabu inayotolewa.

  "Tusifungie tu kibabe, wafungulieni lakini hakikisha wanafuata miongozo ya serikali".

 4. Wafanyakazi wa Gazeti la Tanzania mashakani kwa 'kumuomboleza' rais mpya

  Uongozi wa gazeti la Daily News linalaomilikiwa na serikali limetangaza kuwasimamisha kazi maafisa wakuu wa kitengo cha matangazo kufuatia tukio ambapo gazeti hilo liliweka tangazo la ‘kuomboleza’ kifo cha Rais Samia Suluhu Hasaan.

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matangazo Anitha K Shayo na Msimamizi wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja Rajab Juma Mohammed wamesiimamishwa kazi mara moja ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo,Taarifa ilisema.

  Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya gazeti hilo kuomba msamaha kuhusiana na "dosari" iliyojitokeza katika tangazo ''linaloomboleza'' kifo cha Rais Mpya.

  Katika msamaha wake Mhariri Mkuu wa gazeti la Daily News alisema lengo la ujumbe huo lilikuwa "kumpongeza" Rais Samia baada ya kuchukua hatamu ya uongozi kutoka kwa mtangulizi wake John Magufuli ambaye alifari wiki chache zilizopita.

  Tangazo la gazeti

  Nakala ya tangazo hilo imechapishwa mtandaoni:

  View more on twitter
 5. 'Hatuchukii wanaotupa changamoto na kutukosoa kwa staha'

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Rais John Magufuli
  Image caption: Rais wa Tanzania John Magufuli

  Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amesema serikali yake haiogopi kupewa changamoto wala kukosolewa kama kukoselewa kwa staha.

  Akizindua studio za vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano serikali yake imeruhusu vyombo vingi zaidi vya habari kuliko wakati mwingine wowote tangu taifa hilo lipate uhuru.

  Amesema mwaka 2015, Tanzania ilikuwa na vituo vya radio 106 na televisheni 25 lakini hadi kufikia mwezi februari 2021 kuna jumla ya vituo vya redio 193, televisheni 46, magazeti 247,televisheni za mtandao 443 na redio za mtandao 23.

  Licha ongezeko hilo Rais Magufuli, amewataka waandishi wa habari kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa kwanza na kufanya kazi kwa kuzingatia haki hasa kwa yule ambaye habari inamhusu.

  Pia ameongeza kumekuwa na habari nyingi za uzushi nyingine zikizushia watu vifo wakiwemo viongozi na watu mashuhuri.

  ''Yako mambo ya ajabu yanatokea kwenye baadhi ya mataifa na kamwe huwezi kuyaona kwenye vyombo vya habari. Sasa sisi tumekuwa wepesi kwa sababu ya uhuru huu kila kitu hata kile ambacho hakifai kina andikwa'' alisema Bw. Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli amewataka watendaji wa serikali kuwa wepesi kwenye kutoa taarifa kwasababu ziko baadhi ya Wizara na Taasisi za umma ambako waandishi wakienda kufuata taarifa habari zinafichwa bila sababu ya msingi.

  Rais Magufuli amekuwa akilaumiwa kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

  Pia unaweza kusoma:

 6. Video content

  Video caption: Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumanne 06/10/2020

  Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumanne 06/10/2020 Na Wazir Khamsin