Utalii

 1. Raia Kenya na Ethiopia waliochanjwa miongoni mwa walioruhusiwa kuingia Uingereza

  Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri
  Image caption: Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri

  Nchi nane leo (Jumatano, Septemba 22) zimeondolewa kwenye orodha ya zile zilizopigwa marufuku kuingia Uingereza wakati serikali ya nchi hiyo inapoanza kutekeleza mabadiliko kwenye mfumo wake wenye utata wa usafiri kimataifa.

  Misri na Kenya ni nchi za Afrika ambazo sasa, zitakuwa na wasafiri wanaoruhusiwa kuingia Uingereza.

  Habari hii imepokelewa kama afueni kubwa nchini Kenya ambapo tasnia ya utalii imepata hasara kubwa kufuatia vizuizi vya usafiri kama njia moja ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

  Uingereza ni ya nne yenye mchango mkubwa zaidi kwa watalii wanaotembelea nchi ya Kenya iliyopo Afrika Mashariki ambayo kwa sasa hivi iko katikati ya msimu wake wa kilele cha utalii ambao unamalizika na uhamiaji wa nyumbu kila mwaka.

  Furaha ya kukaribisha zaidi ya watalii 100 waliowasili katika uwanja wa ndege wa Mombasa, pwani ya Kenya, zimeshuhudiwa kwa mbwembwe na taadhima kuu.

  Wageni waliowasili wakiwa ni kutoka Romania – watalii wapya katika soko hilo nchini Kenya.

  "Tuna furaha kubwa sana kuwa hapa, na tutafurahia ujio wetu kabisa. Ni mara yetu ya kwanza. Watu waje kutembelea, wafurahie," mmoja wa watalii alisema.

  Idadi ya watalii nchini humo imepungua kwa zaidi ya theluthi mbili kutokana na janga la virusi vya corona na katika juhudi za kufufua sekta hiyo kwa hali na mali, sasa imegeukiwa soko la watalii kutoka Asia na Mashariki mwa Ulaya.

  Hata hivyo, watalii hawa wapya wanaokuja ni sehemu ndogo tu ya kile Kenya ilizoea kabla ya janga hilo.

  Sekta hiyo hadi sasa imepoteza mapato ya dola bilioni moja na nusu huku ajira milioni mbili zikitoweka - takwimu ambazo Waziri wa Utalii Najib Balala anasema zitachukua miaka kuimarika.

  "Idadi bado ni ndogo, lakini tumeona polepolea watalii wameanza kujiwekea nafasi zao za kuzuru Kenya majira ya joto. Haifurahishi lakini angalau ni ishara ya nia njema na kuonesha kwamba maisha yanarudi kama kawaida katika utalii, " amesema Waziri wa Utalii Najib Balala.

  Je dhana potofu kwamba chanjo ya corona ina sumaku ilitoka wapi?

 2. Video content

  Video caption: Ndovu waliotembea mwendo wa kilomita 500 waamua kujipa lepe ya usingizi

  Katika miezi ya hivi karibuni ndovu wa asili ya kiashia wameonekana wakitembea vijijini na mijini kusini magharibi mwa China , na kuwavutia watu wengi .

 3. Lupita atembelea Serengeti kwa mara ya kwanza

  lupita

  Nyota wa Hollywood kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o ametembelea kwa mara ya kwanza mbuga ya wanyama ya Tanzania ya Serengeti, Aprili 5, 2021,.

  Mwanamitindo huyo muigizaji alipiga picha na kuiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na kuandika serengeti.

  Picha hiyo aliyojipiga mwenyewe yaani selfie inaonesha mazingira ya mbuga hiyo na kukiwa na tembo nyuma yake.

  View more on twitter

  Miezi michache iliyopita, kulitokea gumzo la kwanini Lupita hakupewa ubalozi wa utalii nchini Kenya na kupewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell.

  Lakini waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala alitetea uamuzi wa kumtaja mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kuwa balozi wa utalii kimataifa kwa nchi hiyo.

  Wakati wa hafla ya umma, Bwana Balala alisema anajua Wakenya wengi wameuliza kwanini muigizaji wa Hollywood Lupita Nyong'o hakuchaguliwa katika nafasi hiyo.

  Waziri akajibu kwamba wamekuwa wakimtafuta Bi. Nyong'o lakini hajapatikana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Muigizaji huyo wa Kenya ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar alipendekezwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii kuwa mtu sahihi wa kushikilia nafasi ya balozi wa utalii kimataifa kuwakilisha Kenya.

  Bwana Balala alisema Bi. Campbell amechukua nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba serikali inafanyia kazi namna ya kutumia ushawishi wake kutangaza utalii, kulingana na vyombo vya habari vya nchini Kenya.

 4. Video content

  Video caption: Hifadhi ya Tanzania ya Serengeti yatangazwa kuwa bora duniani

  Hifadhi ya taifa ya Tanzania, Serengeti yatangazwa kuwa bora duniani

 5. Video content

  Video caption: Hatua kuchukuliwa kwa watakaoongoza watalii wasiovaa mavazi ya stara

  Hatua kuchukuliwa kwa watembeza watalii na wamiliki wa hoteli wasiosimamia marufuku hiyo