Olimpiki

 1. Mwanariadha wa Uganda afurushwa Japan

  Olimpiki

  Mnyanyuaji uzani wa Uganda aliyetoweka katika kambi ya Olimpiki magharibi mwa Japan Ijumaa iliyopita amerejea nyumbani saa chache kabla ya kuanza rasmi kwa michezo ya Olimpiki.

  Julius Ssekitoleko alirejeshwa nyumbani leo asubuhi na kuchukuliwa na polisi muda mfupi baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe.

  Mama yake mzazi, mke wake mjamzito na maafisa wengine wa serikali waliokuwa wamesafiri kumlaki hawakufanikiwa kumuona.

  Katika taarifa, Wazara ya Mambo ya Nje ilisema, "Serikali ya Uganda imejitolea kuendelea kumhudumia mwanariadha huyo ili kumsaidia atulie na kuendeleza kazi yake lakini pia kumsaidia kuelewa jinsi vitendo kama hivi vibaya havimuathiri yeye tu kama mwanariadha lakini pia wanariadha wengine katika sekta ya Michezo na taifa kwa ujumla. "

  Wakati alipotoweka katika chumba chake cha hoteli huko Izumisako mjini Osaka, Julius alikuwa hajatimiza viwango vya Olimpiki vilivyowekwa kimataifa alipofika Japan.

  Alitakiwa kurejea nyumbani Uganda katikati ya wiki hii.

  Aliacha kijikaratasi chenye ujumbe pamoja na mizigo yake akisema anataka kubaki Japan na kufanya kazi.

  Polisi wa Japan walimpata Julius katika mji wa Yokkaichi, maili 105 kutoka kambi wa wachezaji wa Olimpiki.

 2. El Moutawakel alipita mstari wa kumaliza mbio haraka mbele ya wenzake kiasi kwamba alidhani alikua amekosea kuanza mbio

  Kama wewe ni mwanamke wa Morocco na ndio umetimiza umri wa miaka 36, huenda ulikua karibu kupewa jina Nawal. Hii ni kwasababu ushindi wa Nawal El Moutawakel tarehe 8 Agosti 1984 katika michezo ya Olyimpiki mjini Los Angeles ulikuwa na maana kubwa sana kwa Mfalme wa Morocco Hassan II kiasi kwamba alitangaza kuwa watoto wote wa kike waliozaliwa siku hiyo waitwe jina lake. Hii ni hadithi yake...

  Soma Zaidi
  next
 3. Video content

  Video caption: Kipchoge aelezea ugumu wa kufanya mazoezi

  Corona yasababisha mwanaraidha wa kenya kufanya mazoezi peke yake.

 4. Video content

  Video caption: Eliud Kipchoge azungumzia vitabu anavyosoma akiwa nyumbani

  Bingwa wa michezo ya Olimpiki nchini kenya afanya mazoezi nyumbani kwake