Wadudu

 1. Video content

  Video caption: Kwanini watu wengi wanaogopa kula wadudu wakati zaidi ya watu bilioni mbili wanakula?

  Wadudu aina ya nyenje hupatikana kwa wingi sana baada ya miaka 17,Lakini kwanini hatuli kile ambacho watu wengine bilioni mbili wanakula duniani kote?

 2. Video content

  Video caption: Jinsi nzige wanavyotumiwa kwa faida nchini Kenya

  Shirika moja lisilo la kiserikali (NGO) nchini Kenya linatoa mafunzo kwa jamii ya kuwakamata nzige, ili kuwageuza kuwa chaula cha wanyama.

 3. Ipi siri ya mdudu ambaye hata akikanyagwa hawezi kufa?

  Mdudu jamii ya mbawakavu
  Image caption: Mdudu ambaye hawezi kuruka kukwepa ndege hatari lakini gamba lake ni silaha tosha

  Mdudu mdogo ambaye mwili wake umefinikwa kwa gamba gumu, anayesemakana kuwa hawezi kufa hata akikanyagwa.

  Wanasayansi wamebaini siri ya mdudu huyu kwamba uimara wake ni mara 39,000 zaidi ya uzito wake.

  Matokeo ya utafiti huu yanaweza kusaidia wajenzi wa nyumba kutengeneza nyenzo imara zaidi.

  Utafiti huo uliochapishwa na gazeti la Nature, unawezesha utengenezaji wa nyenzo imara", amesema kiongozi wa timu hiyo David Kisailus kutoka chuo kikuu cha California, Irvine.

  Nyama yake inayofunika mifupa ina viungio ambavyo vinafanya awe imara zaidi
  Image caption: Nyama yake inayofunika mifupa ina viungio ambavyo vinafanya awe imara zaidi

  Aina hii ya mdudu jamii ya mbawakawa ambaye pia anafahamika kama mbawakavu anapatikana Marekani na Mexico na anaishi chini ya gome la mti au chini ya miamba.

  Ndio mdudu mwenye nyama ngumu zaidi inayofunika mifupa.

  Mbawakavu huyu ambaye amepoteza uwezo wake wa kuruka mbali kama njia ya kuepuka hatari, amebadilika na kuwa na mabawa ya mbele ambayo yanazuia asife hata akikanyagwa na kitu na yamekuwa mwokozi wake dhidi ya ndege hatari.

 4. Video content

  Video caption: Masaibu ya nzige Kenya

  Wakulima katika baadhi ya Maeneo nchini Kenya wanahofia kuwa huenda wakakabiliwa na njaa na umaskini kutokana na uvamizi wa nzige. Anne Soy alishuhudia hali ilivyo Turkana

 5. Video content

  Video caption: Virusi vya corona: Niliishi na buibui 70 katika lockdown

  Tazama kando sasa kama unawaogopa buibui! Zookeeper Caitlin Henderson aliishi na 70 kati yao wakati mmoja wakati wa amri ya kutotoka nje nchini Australia.

 6. Na John Nene

  BBC News Swahili

  Vipepeo wa kike humtamani kipepeo huyu kutokana na madaha na uzuri alionao

  Je, una habari vipepeo ni kitega uchumi? Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya kwa muda mrefu sasa wamejikidhi kimaisha kupitia biashara hiyo ya vipepeo.

  Soma Zaidi
  next