Malawi

 1. Rais wa Malawi awafuta kazi waziri na mkuu wa watumishi

  President Lazarus Chakwera takes over energy ministry's functions

  Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amewafuta kazi waziri wa nishati na mkuu wake wa watumishi ambao wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi.

  Wawili hao na afisa mwingine mmoja - Enock Chihana, mshirika katika usimamizi wa Tonse Alliance – walikamatwa siku ya Jumatatu kwa madai ya kuhusika na zabuni ya mafuta ya nchi hiyo.

  Waliripotiwa kujaribu kushawishi jinsi kandarasi ya usambazaji wa mafuta itakavyotolewa.

  Nafasi ya waziri Newton Kambala haijajazwa baada ya kufutwa kwake.

  Majukumu ya wizara ya nishati yamehamishiwa ofisi ya rais.

  Mrithi wa mkuu wa watumishi wa umma Chris Chaima Banda pia hajatajwa wakati tangazo la kufutwa kwake lilipotolewa.

  Bw. Kambala na Bw. Banda hawajatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

 2. Malawi kuondoa hukumu ya kifo

  kunyongwa

  Mahakama kuu ya Malawi imeamua kuwa adhabu ya kifo ni kinyume cha katiba.

  Mahakama imesema kuwa hukumu ya kifo ipo kinyume na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu,

  Hii ikimaanisha kuwa adhabu kubwa zaidi itakayotolewa nchini Malawi itakuwa hukumu ya kifungo cha maisha.

  Tume ya haki za binadamu imeelezea uamuzi huo kuwa hayo ni maendeleo.

  Aidha ilibainika kuwa hakuna aliyenyongwa ncini humo tangu mwaka 1975.

  Malawi sasa imekuwa nchi ya 22 ukanda wa mataifa ya -Sahara kusitisha adhabu ya kifo.

 3. Kenya yasitisha safari za ndege za abiria kwenda India

  kenya

  Kenya imesitisha kwa muda safari za ndege za abiria wanaotoka India. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya Corona-kusini mwa Asia mwa taifa hilo.

  Katazo hilo litaanza Jumamosi na kudumu kwa muda wa wiki mbili.

  Lakini ndege za mizigo zitaendelea kufanya kazi .

  Mtu yeyote anayewasili kutoka India kabla ya hapo atapimwa virusi vya corona na wakikutwa na corona watalazimika kujitenga na kukaa karantini kwa gharama zao wenyewe.

  Kwa sasa India inakabiliwa na janga kubwa la virusi vya corona.

  Hospitali zimelemewa kwa kuwa na wagonjwa wengi na ripoti za watu kufariki mitaani zikiongezeka.

  Zaidi ya wagonjwa 350,000 wa virusi vya corona wameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita – na hii kuwa rekodi mpya ya dunia.

  Mataifa ya Afrika yanategemea kupata chanjo kutoka India kwa kutumiwa mpango wa Covax . Ingawa ongezeko la maambukizi limesababishwa kupiga marufuku usafirishaji wa chanjo hizo na kuangazia watu wake kwanza.

  Malawi imepiga marufuku pia wasafiri wanaotoka India, pamoja na Bangladesh, Brazil na Pakistan kutokana kusambaa kwa virusi vya corona katika hayo mataifa.

 4. Rais wa Malawi aomba muda kabla ya kutangaza baraza jipya la mawaziri

  Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameahirisha kutangaza baraza jimpya la mawaziri kwa mara nyingine tena, akisema anataka muda zaidi.

  Ofisi yake imesema kwamba imepokea ripoti ya kutathmini utenda kazi wa mawaziri kutoka kwa Makamu wa Rais Saulos Chilima siku ya Jumatano na haiwezi kufanya mabadiliko mara moja -kwani ripoti hiyo ni muhimu na rais anahitaji muda "kuipitia kwa makini".

  "Ikizingatiwa kuwa ripoti hiyo ni muhimu, raois anataka kuichanganua kwa makini, na shughuli hiyo itachukua siku zaidi kuliko ilivyotarajiwa," taarifa kutoka mkuu wa mawasiliano ya rais Brian Banda alisema.

  Siku ya Jumatatu rais aliwaambia Walamawi kwamba atafanyi amabadiliko baraza lake la mawaziri ndani ya saa 48.

  Lakini sasa ameomba kupewa muda zaidi, akisema atatangaza mawaziri wampya "tatakapokamilisha jukumu lake kwa mujibu wa katiba".

  Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo hata hivyo vimeonyesha picha ya rais na makamu wake iliyochapisha kwenye ukurasa wa Facebook wa Ikulu ya Malawi mnamo 19 Februari, na maelezo kwamba walikuwa wakitathmini utendaji wa Baraza la Mawaziri kwa pamoja.

  View more on facebook
 5. Kifo cha Rais Magufuli: Rais wa Malawi asema Magufuli alikuwa kiungo muhimu

  "Ni pigo kwa Afrika," asema Rais wa Malawi Lazarus Chakwera baada ya kupokea taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania John Magufuli, 61.

  "Rais Magufuli walikuwa ishara kuu ya ufufuo wa uchumi wa Afrika, na kifo chake ni pigo kubwa kwa bara hili," Bw. Chakwera aliongeza katika ujumbe wake wa Twitter.

  View more on twitter
 6. Nabii Bushiri milionea anayetafutwa na Afrika Kusini aachiwa huru Malawi

  Nabii Shepherd Bushiri ana wafuasi wengi barani Afrika

  Nabii milionea wa Malawi Shepherd Bushiri na mke wake wameachiwa bila masharti yoyote na mahakama moja mjini Lilongwe nchini Malawi baada ya kujisalimisha kwa polisi Jumatano.

  Afrika Kusini inataka ikabidhiwe wawili hao kwa kukiuka masharti ya dhamani nchini humo.

  Bushiri na mke wake wameshtakiwa nchini Afrika Kusini walikokuwa wanaishi kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na ulaghai.

  Hata hivyo wawili hao wamekanusha mashtaka hayo.

  Wakili wao, Wapona Kita, aliitaka mahakama iwaachilie wawili hao bila masharti yoyote akisema kuwa kukamatwa kwao ni kinyume na sheria.

  Mwendesha mashtaka aliomba mahakama kuruhusu polisi kuendelea kuwashikilia wanandoa hao kwa siku 30 zaidi ili kuwezesha Afrika Kusini kuwasilisha rasmi ombi lao la kutaka wakabidhiwe kwa nchi hiyo.

  Bwana Kita alisema ni kinyume cha sheria kumzuilia mtu wakati Afrika Kusini haijawasilisha ombi rasmi.

  Soma zaidi:

  Rais Cyril Ramaphosa anafuatilia kujua aliyemtorosha Nabii Bushiri milionea