Ubunifu na Mitindo ya Mavazi

 1. Video content

  Video caption: Vigodoro: Kwa nini baadhi ya watu Tanzania hupendelea vazi la ndani 'linalokuza' makalio?

  Je, ni urembo ama kutokujiamini? Mwandishi wa BBC anazungumza na wauzaji, watumiaji na mwanasaikolojia juu ya vazi la ndani maarufu nchini Tanzania linalofahamika kama vigodoro.

 2. Video content

  Video caption: Mbunifu wa mitindo anavyotengeza nguo kutokana taka za plastiki

  Elisha Ofori Bamfo, mbunifu wa mitindo nchini Ghana amepata suluhisho ambalo linaweza kusaidia tu

 3. Mwanamke mwanamitindo anayezikubali mvi zake

  Katika msururu wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa Kiafrika, Mwandishi Mghana Elizabeth Ohene alitumia fursa ya janga la virusi vya corona kuunga mkono mwenendo wa urembo wa kisasa

  Soma Zaidi
  next
 4. Video content

  Video caption: Yasmine Agbantou, mwanamke aliyeamua kubuni mitindo nguo za wanawake wanene

  Mbunifu wa mitindo Yasmine Agbantou ni mwanamke anayetengeneza mitindo ya wanawake wanene baada ya kuchoshwa na ubunifu wa mitindo unaowalenga wanawake wembamba

 5. Lupita atembelea Serengeti kwa mara ya kwanza

  lupita

  Nyota wa Hollywood kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o ametembelea kwa mara ya kwanza mbuga ya wanyama ya Tanzania ya Serengeti, Aprili 5, 2021,.

  Mwanamitindo huyo muigizaji alipiga picha na kuiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na kuandika serengeti.

  Picha hiyo aliyojipiga mwenyewe yaani selfie inaonesha mazingira ya mbuga hiyo na kukiwa na tembo nyuma yake.

  View more on twitter

  Miezi michache iliyopita, kulitokea gumzo la kwanini Lupita hakupewa ubalozi wa utalii nchini Kenya na kupewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell.

  Lakini waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala alitetea uamuzi wa kumtaja mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kuwa balozi wa utalii kimataifa kwa nchi hiyo.

  Wakati wa hafla ya umma, Bwana Balala alisema anajua Wakenya wengi wameuliza kwanini muigizaji wa Hollywood Lupita Nyong'o hakuchaguliwa katika nafasi hiyo.

  Waziri akajibu kwamba wamekuwa wakimtafuta Bi. Nyong'o lakini hajapatikana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Muigizaji huyo wa Kenya ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar alipendekezwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii kuwa mtu sahihi wa kushikilia nafasi ya balozi wa utalii kimataifa kuwakilisha Kenya.

  Bwana Balala alisema Bi. Campbell amechukua nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba serikali inafanyia kazi namna ya kutumia ushawishi wake kutangaza utalii, kulingana na vyombo vya habari vya nchini Kenya.