Uhuru wa Kujieleza

 1. Mbowe: Siwezi kujipendekeza kwa rais Samia

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Mbowe

  Mwenyekiti wa chama upinzani cha (Chadema) nchini Tanzania, Freeman Mbowe amesema Tanzania isitarajie mabadiliko kutoka kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu kwani anatoka Chama Cha Mapinduzi ambacho kimeshika dola toka uhuru.

  Katika mahojiano ya mtandaoni Mbowe amesema anataka kuona haki na si vinginevyo kwani anachokitaka ni haki na uhuru wa watu kwani viko kwa mujibu wa sheria.

  ''Demokrasia haitakiwi kutolewa kama zawadi Demokrasia inapiganiwa Pamoja na maumivu tunayo yapata tuna amini hiyo ndio safari halisi ya kuitafuta demokrasia” , alisema.

  Mbowe anasema ni mapema sana kusema iwapo Tanzania ni salama sana kwa viongozi wa upinzani walioko ndani na nje ya nchi kwani bado viongozi wengi wa upinzani wanasota magerezani kwa kesi za kusingiziwa na wengine wamekimbia wakihofia usalama wao na serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana na hali hiyo.

  Pia anasema uhuru ambao umetolewa kama haki kwenye katiba bado umebinywa , akitoa mfano wa uhuru wa mikutano ya kisiasa, uhuru wa maandamano na hata vyombo habari kwani serikali inatumia sheria kuwanyima wananchi haki yao.

  Licha ya kauli za Rais Samia kuleta faraja na matuamaini, Bwana Mbowe anasema kuna haja ya mabadiliko ya kisheria ili haki itendeke kwa mujibu wa sheria na sio huruma ya rais.

  Mbowe anasema binafsi anatambua kauli njema za matumaini ambazo amezitoa Mama Samia na wanamheshimu kama mlezi na hata wanavyofanya siasa wana mipaka kwani wanamuheshimu kama mama.

 2. Uganda yataka YouTube kufunga vituo vinavyohusishwa na Bobi Wine

  Bobi Wine

  Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda imeandikia Google, jukwaa la kushirikisha video, kuomba ifunge vituo 14 vya YouTube vinavyodaiwa kuhusishwa na ghasia za mwezi uliopita ambazo zilisababisha zaidi ya watu 50 kufariki.

  Ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine mikuu kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais wa upinzani ambaye ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kwa kukiuka masharti ya kudhibiti ugonjwa corona.

  Baadhi ya vituo vya YouTube vinavyohusishwa na Bobi Wine ndivyo vinalengwa, lakini mkuu wa masuala ya sheria wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda ameambia kituo cha televisheni cha Bloomberg kwamba ni "bahati mbaya" tu.

  Katika barua yake kwa Google,Tume hiyo ilisema vituo hivyo vilitumiwa kuchochea vurugu na vinatangaza maudhui yanayokiuka sheria, Gazeti la Daily Monitor linaripoti.

  Raia wa Uganda wanajianda kushiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge Januari 14. Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu, inawania kuchaguliwa tena.

 3. Video content

  Video caption: Hali ya waandishi wa habari nchini Tanzania

  Tanzania kwa miaka mingi imekuwa katika ramani nzuri ya hasa kwenye uhuru wa kujieleza