Sanaa ya Kuigiza

 1. Muigizaji Will Smith akiri kuwa na 'muonekano mbaya zaidi'

  Will Smith

  Mwigizaji wa Marekani Will Smith amekiri kuwa na "muonekano mbaya zaidi" katika maisha yake baada ya kuweka picha yake akiwa bila shati katika mtandao wa Instagram.

  Will Smith, 52, anaonekana katika picha hiyo akiwa ameinua mikono kuashiria hajaridhishwa na jinsi alivyoongeza uzani wa mwili.

  Katika ujumbe alioandikia mashabiki wake milioni 53, Will alisema: "Naomba niwe muwazi kwenu nyote – muonekano wangu wa sasa ni mbaya zaidi katika maisha yangu."

  View more on instagram

  Baadhi yaa mashabiki wake walimpongeza kwa kuwa mjasiri kwani ni hatua moja ya kujikubali na kushughulikia changamoto inayomkabili.

  Muigizaji huyo aliyewahi kupunguza na kuongeza uzani wake wa mwili ili kuigiza katika vipindi tofauti ikiweo ile ya ‘Will Smith’-The Fresh Prince of Bel-Air iliyopata umaarufu mkubwa miaka ya 1990.

 2. Iraq yapiga marufuku maonyesho ya Televisheni ya ugaidi

  Kipindi cha Raslan

  Vipindi viwili vya televisheni ambavyo vimezua ghadhabu nchini Iraqi kwa kuwafanyia mzaha watu maarufu kwa kutumia vilipuzi bandia na kuiga visa vya utekaji vimesitishwa.

  Mmalaka ya mawasiliano imesema vipindi hivyo - Tony's Bullet na Raslan's Shooting - vimekiuka kanuni za mawasiliano.

  Kipindi kimoja cha Risasi ya Raslan, mwigizaji alizimia kwa hofu baada ya kufungwa vilipuzi bandia.

  Watazamaji walikosoa vipindi hivyo kwa kuendekeza ukatili hasa ikizingatiwa vitisho vya mara kwa mara kutokana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo nchini Iraq.

  Islamic State imetimuliwa katika ngome yake Iraq lakini kundi hilo limeendelea kuwashambulia raia na wanajeshi.

 3. hata zaidi bendera ya Afrika Mashariki kwa sababu Netflix ina zaidi ya watu milioni 203.7 wanaoiumia huduma hiyo kutazama filamu .

  Afrika mashariki imejaa nyota katika ulingo wa kimataifa kwa kuipeperusha bendera yao . Iwe ni katika michezo, sanaa na sayansi watu mbalimbali wameziletea sifa nchi za Afrika mashariki katika nyakati tofauti katika miaka ya hivi karibuni.

  Soma Zaidi
  next
 4. Video content

  Video caption: Beyoncé ashinda tuzo ya 28 katika tuzo za Grammy

  Mwanamuziki Beyoncé ajizolewa tuzo 28 katika tuzo ya Grammy mwaka huu.

 5. Muigizaji aibua gumzo Kenya baada kukutana na Rais Kenyatta

  Rais Kenyatta
  Image caption: Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

  Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Kenya wamekuwa wakitoa maoni mseto kuhusiana na kanda ya video inayomuonesha muigizaji Pascal Tokodi alivyokutana na Rais Uhuru Kenyatta bila kutarajia.

  Katika video hiyo iliyowekwa mtandaoni ni muigizaji huyo, anaonekana akipunguza mwendo wa gari na kumsalimia Rais Kenyatta - ambeye alikuwa akitembea karibu na makazi yake rasmi katika jiji kuu, Nairobi

  Inamuonesha rais akiwa bila walinzi.

  Muigizaji huyo "alitumia muda huo" kumuomba rais atazame kipindi maarufu cha televisheni, Selina, ambacho yeye ni mmoja wa waigizaji wake. Rais alimjibu ''Nimeona''.

  View more on twitter

  Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemkosoa muigizaji huyo, wakisema angelitumia muda huo vizuri.

  "Unakutana na RAIS akitembea peke yake na kile unachotaka akufanyie ni kutazama Selina kwenye Maisha Magic East? Vijana wa Kenya hawana sera na wanataka RAIS kuwapa nyadhifa serikalini wakati anafahamu fika hawawezi kujitetea kwa sekunde 10,"Abraham Mutai aliandika kwenye Twitter.

  Wengine walisema muigizaji huyo hakufany amakosa kunadi kipindi chake.

  "Pascal tokodi ni muigizaji mkuu wa kipindi cha selina, kipindi hicho kinamkimu kimaisha, alikutana na rais kwa chini ya sekunde 10....akamuomba atazame selina n akuungamkono kazi yake, kwa kweli hakufanya kosa lolote,"Chege Githinji aliandika.