Jamii

 1. Kwa jamaa walioachwa nyuma na wapendwa wao - hofu ya kuwatafuta jouhatsu wao - inaweza kuwaathiri vibaya.

  Kila mwaka baadhi ya watu huamua 'kutoweka' na kuanza upya maisha, ajira, nyumba na familia. Nchini Japan, kuna makapuni ambazo zinawasaidia wale wanotaka kutoweka na kupotea kabisa.

  Soma Zaidi
  next
 2. Afrika Kusini kutegua kitendawili cha mama anyedai kuzaa watoto 10

  Miguu ya mtoto mchanga

  Mamlaka nchini Afrika Kusini "zinakusanya taarifa" juu ya sakata inayoendelea kuhusu mwanamke wa Pretoria anayedaiwa kujifungua watoto 10, mtandao mmoja wa habari umeripoti.

  Hakuna shirika lolote la habari limefanikiwa kuthibitisha taarifa hiyo iliporipotiwa mara ya kwanza na mtandao wa habari wa Pretoria News wiki iliyopita.

  "Kuna masuala kadhaa muhimu yanastahili kushughulikiwa” kabla ya kuhutubia umma, Waziri wa Ustawi wa Jamii Lindiwe Zulu aliuambia mtandao wa habari wa TimesLive.

  ''Madai hayo ni ya kushangaza, lakini malipo na moshi hapakosi moto. Tunataka kuwajibikia suala hili iwezekanavyo. Tunawajimu wa kufahamisha watu kinachoendelea," alinukuliwa kusema.

  Pretoria News imesema haitabadili msimamo kurusu taarifa ya kwamba Gosiame Sithole alizaa watoto 10 tarehe 7 mwezi Juni.

  Pia imechapisha ripoti kwamba anayedaiwa kuwa baba hajawaona watoto hao wachanga.

  Independent Media, kampuni mama ya wavuti huo wa habari, imeshutumu mamlaka kwa habari ya kujificha ikidai kwamba walitaka "kuficha uzembe unaokumba sekta ya afya ambao uliwahusisha wanasiasa wakuu na wafanyikazi wa umma".

  View more on twitter

  Bi Zulu alikataa kuthibitisha au kukana kuwepo kwa watoto hao lakini akaongeza kuwa Rais Cyril Rampahosa ataarifiwa kwanza kabla ya matokeo ya uchunguzi kutolewa hadharani.

 3. Uganda yaharamisha utoaji watu kafara

  Mifupa
  Image caption: Mtu yeyote atakayekutwa na viungo vya binadamu atakabiliwa na kifungo cha maisha

  Bunge la Uganda imepitisha mswada wa kuharamisha kutoa watu kafara na kupendekeza kifungo cha maisha kwa wale watakaovunja sheria .

  Kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo sheri aya nchi hiyo haikuwa na sheria maalum ya kuangazia uhalifu wa kutoa watu kafara na badala yake kosa hilo lilikuwa likihukumiwa ka mauaji.

  Mswada huo pia unaharamisha mtu kupatikana na viungo vya mwili wa binadamu, utumizi wa vungo hivyo kwa dawa au kuuza kwa maslahi ya kibinafsi.

  Mtu atakayepatikana na hatia hiyo anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.

  Takwimu zinazoashiria ukubwa wa utowaji kafara wa watu unatofautiana katika maeneo tofauti nchini Uganda kwasababu visa hivyo haviripotiwi katika maeneo mengine ama hakuna hatua ya kisheria inayochukuliwa kikamilifu kuhusiana na uhalifu wa aina hiyo.

  Kulingana na utafiti wa mwaka 2014 uliofanywa na Tume ya kutetea haki nchini Uganda kuhusu utoaji kafara, watoto hususan wale walio na umri wa chini ya miaka sita umeshamiri sana

  Kulingana na mswada huo manusura wa utoaji kafara ya binadamu watapewa ushauri nasaha na kulipwa fidia.

  Mswada huo utakuwa sheria pale Rais atakapotia saini kuuidhinisha .

 4. Fahamu Kwanini wastaafu wengi Nigeria wananyimwa pensheni zao

  Video content

  Video caption: BBC Africa Eye : Kwanini wastaafu wengi Nigeria wananyimwa pensheni zao
 5. Basangiye irembo n'igikari, aha buri umwe arasohoka mu gikari

  Claudine Mukagahima na Faustin Munyanziza wanaishi nyumba moja iliyojengwa na 'Tume inayosimamia Umoja na Maridhiano', nyumba maalum mnamoishi familia mbili ; mmoja aliyetekeleza mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 huku jirani yake akiwa ni manusura wa mauaji hayo.

  Soma Zaidi
  next
 6. Video content

  Video caption: Tazama upasuaji wa kuongeza urefu wa miguu

  Upasuaji wa aina hiyo ulikuwa ukifanyiwa watu waliopata ajali