Niger

 1. Jeshi la Nigeria 'liliwapiga risasi na kuwaua waandamanaji wa #EndSars': ripoti

  Nchi ilitikiswa na maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kwa wiki mbili Oktoba iliyopita
  Image caption: Nchi ilitikiswa na maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kwa wiki mbili Oktoba iliyopita

  Jopo la uchunguzi, lililoundwa na mamlaka nchini Nigeria kuchunguza tukio la waandamanaji kupigwa risasi mjini Lagos mnamo Oktoba 2020, limewasilisha ripoti juu ya kile kilichokea usiku huo.

  Toleo lililovuja la ripoti hiyo, iliyokabidhiwa kwa gavana wa jimbo hilo leo, inadai kuwa wanajeshi wa Nigeria waliwapiga risasi kimakusudi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye barabara ya Lekki Tollgate, kisha wakajaribu kuificha.

  Waandamanaji hao walikuwa wakiendesha kampeni dhidi ya ukatili wa polisi.

  Pia ilibaini kuwa baada ya jeshi hilo kurudi nyuma, askari polisi waliendelea na vurugu na kujaribu kufanya usafi katika eneo la tukio na kuweka miili kwenye lori na kutoa risasi.

  Baadhi ya matokeo yanalingana na ripoti za awali za Amnesty International, pamoja na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.

  Gavana wa Jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu, ambaye alianzisha jopo hilo, ameahidi "kutilia maanani" matokeo yake.

 2. Nigeria yasitisha huduma ya reli baada ya shambulio

  N

  Shirika la reli la Nigeria limesitisha kwa muda huduma za reli kutoka Abuja, kuelekea kaskazini magharibi mwa Kaduna baada ya watu wenye silaha kuwavamia abiria wa treni siku ya Jumatano.

  Watu walioshuhudia walisema washambuliaji hao walimlenga dereva wa treni ingawa hakuna majeruhi alireripotiwa mpaka sasa.

  Abiria mmoja aliiambia BBC kuwa walisikia mlio mkubwa kabla ya treni haijasimama kwa saa kadhaa.

  Mbunge wa zamani nchini humo, Senata Shehu Sani, aliandika kwenda tweeter kuwa treni ya pili na hivyo kulazimika kurudi Abuja siku ya Alhamisi baada ya mlipuko ulipotokea katika reli hiyo.

  Kampuni ya reli ya Nigeria ilisema huduma hizo zitarudi baada baada ya Ijumaa baada ya ukarabati..

 3. Ukusanyaji wa kodi ya mazishi Kusini mwa Nigeria

  People are complaining that the cost of burying their loved one has become a tax

  Kinyume na maeneo ya Kaskazini mwa nchi yanayokaliwa zaidi na Waislamu, maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ambakowanaishi zaidi Wakristo , familia huhangaika kuwazika wapendwa wao.

  Hii hutokana na kiasi cha pesa kinachotumiwa katika kile kinachosemekana kuwa ni kutekeleza taratibu za kitamaduni na kidini za mazishi.

  Lakini wakati huo huo baadhi wameanza kupaza sauti zao kupinga mtindo taratibu hizo ambazo ni ghali, wakisema kuwa viongozi wa kijamii na wa kidini wanashutumiwa kuwatoa pesa wafuasi wao kabla ya kuwaruhusu kuwazika wafu wao.

  BBC Igbo ilitembelea mji wa Ogidi uliopo Kusini Mashariki mwa Nigeria, ambapo ilipata fursa ya kuzungumza na Bw Uche Henry Modili, ambaye mke wake alifariki mwezi Machi.

  Kulingana na Bw Uche, "Wakati mtu anapofariki katika eneo hilo, anaulizwa 'Huu ni mwili wa nani?'

  "Chagua ni ; kanisa au'mama dunia',maneno ambayo hutumika kuelezea mazishi ya kitamaduni ya jamii.

  "Hapa ndipo tatizo lilipo, pande zote zinaweka pesa mbele kwa kuziomba familia kulipa kabla ya kuruhusiwa kumzika mfu wao.

  "Makundi ya kitamaduni hudai pesa kabla ya kuhudhuria mazishi, na kanisa linasisitiza kuwa garama ya mazishi ilipwe sawa na waimbaji wa kwaya ambao wanapaswa kuimba katika mazishi." Anasema Uche.

  Alisema kuwa Askofu Mkuu wa jimbo laEnugu, Rev .Emmanuel Chukwuma, alisema kuwa watu wanapaswa kulipia mahitaji ya kifedha ya kanisa wakati wa maisha yao.

  Je unajuwa ni kwa nini maiti hawazikwi kwa miezi au hata kwa miaka nchini Ghana?

 4. Mlipuko wa kipindupindu waua makumi ya watu Niger

  Mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na kutapika yaani kipindupindu umesababisha vifo vya watu 83 people nchi Niger, ambako mamlaka zimerekodi zadi ya visa 2,300 tangu Machi 13.

  Sita kati ya maeneo manane nchini Niger yameathiriwa na mlipuko huo, umeongezeka zaidi kutomana na mafuriko.

  Janga la kipindupindu lilitangazwa rasmi Agosti 9 na Waziri wa Afya Idi Illiassou Mainassara.

 5. 'Niliwaona malaika wakimbeba TB Joshua'

  TB Joshua

  Katika video iliyosambaa sana, mjumbe wa Mungu Nabii Paul alitabiri kwamba aliwaona malaika, waliomchukua nabii TB Joshua kutoka duniani.

  "Mungu alinionesha maono ya mwisho, nisikieni, nilisimama, na nikachukuliwa juu mbinguni, na madirisha ya mbingu yakafunguliwa kwa ajili yangu, na nikasimama kuangalia chini duniani ."

  Niliwaona malaika sita walitumwa chini kutoka mbinguni na kwenda duniani kumbeba nabii Joshua, kile nilichokiona nilikisema.

  Malaika watatu walimshika mkono wake wa kuume watatu wakamshika mkono wake wa kushoto, wakambeba juu nabii TB Joshua na kushikilia kikombe.

  Nabii Paul alisema alitazama mahala ambapo manabii walisimama, na wakageuka kulia , pia aliweza kuangaliakulia lakini hakuweza kuona sura ya aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha enzi.

  Nabii ME Paul pia alisikia sauti ya Mungu akiwaambia malaika kuchukua kikombe cha ndege kutoka kwa Nabii Joshua, na kukileta kwake.

  Kwa namna hiyo, nabii alipelekwa mahali sahihi.

  "Wakati mmoja hata niliwaona malaika wakuu wakiwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wakachukua kikombe kutoka kwa nabii TB Joshua, na kukipeleka mbele ya enzi ya Mungu.

  Alisema Bwana alikuwa na malaika hawa akamchukua mchungaji mahala panapofaa kwasababualikuwa amemaliza mwendo wake duniani.

 6. Nigeria: Watu kadhaa waliotoweka wahofiwa kufariki baada ya boti kuzama Nigeria

  Ramani

  Makumi ya watu wanahofiwa kufariki kaskazini mwa Nigeria baada ya boti iliyokuwa na abiria 200 kuvunjika mara mbili na kuzama mtoni, maafisa wanasema.

  Abiria wengi walikuwa wanawake na watoto waliokuwa wakisafiri kutoka jimbo la Niger kuelekea jimbo jirani la Kebbi.

  Watu 20 wameripotiwa kuokolewa, huku mamlaka ikilaumu ajali hiyo ya Jumatano ilisababishwa na uzito kupita kiasi.

  Wapiga mbizi na wafanyakazi wa dharura wamekuwa wakisaidia kuwaokoa wengine katika mto Niger, maafisa wa eneo hili waliiambia BBC.

  Rais Muhammadu Buhari ameelezea kusikitishwa na ajali hiyo ''mbaya", na kutuma rambirambi zake kwa jamaa za waathiriwa.

 7. Mji ambao wasioolewa wananyimwa kupangishwa nyumba

  Damilola Olushola anasema anaweza kulazimika kutafuta mume wa bandia ili kupata nyumba.

  Wanawake wasio na waume wanabaguliwa na wamiliki wa nyumba za kupangisha mjini Lagos, lakini hakuna changamoto inayokosa ufumbuzi.Soma zaidi

 8. Ubalozi wa Marekani wafungwa baada ya ufyatulianaji wa risasi

  Gari la vita la wanajeshi

  Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Niger, Niamey, umefungwa, huku kukiwa na ripoti za jaribio lililoshindwa la askari kufanya mapinduzi.

  "Ubalozi wa Marekani Niamey utafungwa Jumatano, Machi 31, 2021, kwa sababu ya milio ya risasi iliyosikika karibu na kitongoji chetu.

  Huduma za kibalozi zinasimamishwa hadi itakapotangazwa. Wafanyikazi wote wanahimizwa kukaa nyumbani, hadi hapo itakapotangazwa tena," ilisoma taarifa kwenye tovuti ya ubalozi.

  Milio mikali ya risasi ilisikika mapema leo asubuhi karibu na ikulu ya rais na katika vitongoji vingine vya Niamey.

  Ripoti zinasema hali hiyo sasa inadhibitiwa, chini ya masaa 48 kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule Mohamed Bazoum.

  Ikiwa atachukua madaraka itakuwa ni uhamisho wa kwanza wa kidemokrasia wa kupokezana madaraka nchini Niger.

 9. Mji mkuu wa Niger uko katika hali ya juu ya tahadhari, kulikoni?

  Niger is struggling to contain an Islamist insurgency.

  Milio mikali ya risasi imesikika karibu na eneo la makazi ya rais ambalo pia lina ofisi ya rais katika mji wa Niamey,Niger Jumatatno asubuhi.

  Milio hiyo ya risasi ilisikika karibu saa tisa usiku -03:00 (02:00 GMT), na ilidumu kwa karibu dakika 15, ikifuatiwa na milio ya risasi ya bunduki ndogo, wakazi walisema.

  Hali imesalia kuwa tete na mji huo kwa sasa umewekwa chini ya tahadhari ya hali ya juu.

  Ufyatulianaji risasi huo umejiri chini ya saa 48 kabla ya sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya mteule, Mohamed Bazoum.

  Serikali ya Niger haijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.

  Kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulio kutoka kwa makundi ya wanamgambo waliojihami huku taharuki za kisisasa zikikumba nchi hiyo kufuatia ushindi wa Bw. Bazoum katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi Februari.

  Mpinzani wake rais wa zamani Mahamane Ousmane, ambaye alishidwa katika duru ya pili ya uchaguzi, amepinga matokeo na kupuuza uamuzi wa mahakama wa kudumisha matokeo hayo.