Uganda

 1. ADF/IS attacks

  Kati ya makundi yenye sifa mbaya zaidi yanayoendesha shughuli zao DRC ni lile la kutoka nchini Uganda la Allied Democratic Forces (ADF). Kundi hilo la kiislamu liliundwa miaka ya 1990 na mara nyingi lilihusika na mizozo ya ndani na taifa la Uganda.

  Soma Zaidi
  next
 2. Kenya kwenye hali ya tahadhari baada ya shambulio la Uganda

  Serikali ya kenya imetoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu

  Serikali nchini Kenya imesema maafisa wa usalama wameimarisha usalama kufuatia shambulio la milipuko miwili katika nchijirani ya Ugana siku ya Jumanne.

  Msemaji wa serikali Cyrus Oguna ametoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na kuripoti wahusika au mienendo yoyote ya kutiliwa shaka.

  Tahadhari hiyo inajiri siku chache baada ya wafungwa watatu waliopatikana na hatia kwa makosa yanayohusiana na ugaidi kutoroka katika gereza moja katika mji mkuu Nairobi.

  Washukiwa wengine watatu wa kujitoa mhanga waliuawa nchini Uganda katika maeneo mawili ya milipuko ambapo watu wengine watatu walifariki.

  Kundi la Islamic State limesema ndilo lililohusika na milipuko ya Uganda.

  Je, Kenya imelipia gharama ya juu kujiingiza katika vita dhidi ya ugaidi?

 3. Milipuko Uganda: Vitisho vya mabomu bado vinaendelea - polisi

  Msemaji wa polisi nchini Uganda amewataka raia wote wa Uganda kuwa makini.

  "Vitisho vya mabomu bado vinaendelea, haswa kutoka kwa washambuliaji wa kujitoa mhanga, Fred Enanga aliwaambia waandishi wa habari.

  "Tunaamini bado kuna wanachama zaidi wa makundi ya ugaidi wa ndani, haswa wale wa kitengo cha mabomu ya kujitoa mhanga ambacho kimebuniwa na ADF [Allied Democratic Forces]. Na hii inahitaji umakini wa jamii. Kwa kweli tunahitaji kuwa macho sana

  "Mbinu ya kushambulia kwa kutumia mabomu wanayotumia ndio mkakati wao ya hivi punde ya mashambulizi."

  Ramani