Boko Haram

 1. Watekaji nyara wawachilia wanafunzi 27 Nigeria

  Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana
  Image caption: Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana

  Wanafuzi 27 waliokuwa wametekwa kutoka taasisi ya misitu katika Jimbo la Kaduna Kaskazini mwa Nigeria wameachiwa huru.

  Walikuwa miongoni mwa wanafunzi 39 waliyotekwa kutoka katika chumba zao za malazina genge la wahalifu waliokuwa wamejihami kwa silaha mwezi Machi.

  Mamlaka zinasema wahasiriwa walioachiwa huru siku ya Jumatano watafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baada ya kuzuiliwa kwa muda zaidi tangu visa vya utekaji dhidi ya wanafunzi kwa lengo la kuitisha kikombozi kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

  Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana nje ya bunge la taifa mjini Abuja kushinikiza mamlaka kuingilia kati suala hilo.

  Kiongozi mashuhuri wa Kiislamu ambaye amekuwa akiongoza juhudi za mazungumzo na magenge ya wahalifu wenye silaha Sheikh Ahmad Gumi ameiambia BBC kwamba yeye na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo waliingilia kati ili kuachiliwa kwa wanafunzi hao. Haijulikani ikiwa fidia ililipwa.

  Nigeria imeshuhudia ongezeko la visa vya utekaji nyara wanafunzi tangu mwezi Disemba huku hali ya usalama ikiendelea kudorora maeneo tofauti nchini.

  Zaidi ya wanafunzi 800 wametekwa huku baadhi yao wakiachiliwa huru baada ya kikombozi kulipwa.

 2. Watu 10 wafariki katika shambulio linashukiwa kuwa la Boko Haram

  Shambulio la siki ya Jumanne linaloshuiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram katika mji wa Maiduguri uliopo jimbo la Borno limesababisha vifo vya watu 10 na wengine 47 kujeruhiwa.

  Gavana wa jimbo hilo Babagana Zulum amesema washambuliaji walitumia guruneti iliyorushwa kwa kutumia roketi katika mji huo unaokaliwa na watu wengi, ikiwemo viwanja vya watoto kucheza. Alisema guruneti hizo zilirushwa kutoka viungani mwa mji huo.

  Picha zilizotolewa na mamlaka za jimbo hilo zinaonesha makumi ya watu waliojeruhiwa miongoni mwao watoto wakiwa hospitali.

  View more on twitter
 3. Video content

  Video caption: Mpiga picha anayehatarisha maisha yake kutengeneza makala ya wahanga wa Boko Haram

  Mpiga picha wa Nigeria Nelly Ating, ametengeneza makala ya wahanga wa Boko Haram tangu mwaka 2014.