Barack Obama

 1. Nyanya yake Obama azikwa Magharibi mwa Kenya

  Obama na nyanayake Sara Obama

  Mama Sarah Obama, nyanya yake aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama amezikwa Magharibi mwa Kenya kulingana na utamaduni wa dini ya Kiislamu.

  Mama Sarah alifariki dunia siku ya Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mfupi kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa.

  Akiomboleza kifo chake Rais Obama alisema kwamba alikuwa "daraja la ukumbusho wa zamani" na ngano zake zilisaidia "kuziba pengo lililokuwepo".

  Gazeti la Daily Nation nchini Kenya liliweka video ya mazishi ya Mama Sarah Obama katika mtandao wa Twitter:

  View more on twitter

  Soma zaidi:

  Barack Obama amuomboleza nyanya yake Sarah Obama

  Mama Sarah Obama atakumbukwa vipi?

 2. Bibi yake Obama afariki Kenya

  Obama na Mama Sara

  Bibi wa Kambo wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama amefariki katika hospitali nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99, familia yake imenukuliwa na vyombo vya habari vya nchini humo

  Mama Sarah amekuwa mgonjwa kwa muda na amefariki alipokuwa akipokea matibabu.

  View more on twitter

  Familia yake inafanya mipango ya kufanya mazishi yake Jumatatu katika makaburi ya umma mjini, kulingana na ripoti.

  Rais Obama alikuwa akimuita Granny Sarah.

  Bi Obama alimtetea mjukuu wake wakati wa uchaguzi wa Marekani iliposemekana ni Muislamu na hakuzaliwa Marekani.

  Soma zaidi

 3. Marais Barack Obama, George W Bush na Bill Clinton wajitolea kupata chanjo ya corona

  Waliokuwa Marais wa Marekani

  Waliokuwa marais wa Marekani Barack Obama, George W. Bush na Bill Clinton wamejitolea kupewa chanjo ya ugonjwa wa corona kwa uwazi kabisa.

  Watatu hao ambao wawili ni wa chama cha Democrat na mmoja wa Republican wamesema kuwa watapata chanjo hiyo punde tu itakapoidhinishwa na wadhibiti wa maafisa wa afya.

  Hatua hiyo inakusudiwa kuimarisha imani ya raia juu ya usalama na ufanisi wa chanjo za virusi vya corona.

  Kura za maoni zinaonesha kuwa idadi kubwa ya watu hawana haraka ya kupata chanjo hiyo.

  Hadi kufikia sasa hakuna chanjo ambayo imeidhinishwa na Marekani lakini wadhibiti wa serikali wanaanza kufuatilia chanjo ya kampuni za kampuni za Pfizer na Moderna wiki zijazo.

  "Nawaahidi itakapoanza kupatikana kwa watu walio katika hatari kubwa, nitaipata," Bwana Obama amesema katika mahojiano ya radio Jumatano SiriusXM.

  "Huenda nikainywa kupitia televisheni au nichukuliwe video, ili watu wajue kwamba ninaamini sayansi."

 4. Barack Obama

  Barack Obama amemshutumu Donald Trump kwa kuchukulia urais kama "onyesho la kipindi cha televisheni ", katika hotuba aliotoa kwenye kongamano la Democrat.

  Soma Zaidi
  next