Paul Kagame

 1. Rwanda yaomba Tanzania walimu wa Kiswahili

  Rwanda iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi
  Image caption: Rwanda iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amemomba mwenzake wa Tanzania Swahili kuwapeleka walimu wa watakaosaidia kuimarisha juhudi za Rwanda kufunza lugha ya Kiswahili

  Katika karamu ya serikali Jumatatu usiku - kuashiria kumalizika kwa ziara ya siku mbili ya Rais Samia Suluhu - Rais Kagame alisema kuwa Rwanda tayari imeanzisha masomo ya Kiswahili shuleni.

  Mwaka 2017, Rwanda iliidhinisha Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza llakini lugha hizo zimechukua muda kushamiri kutokana na uhaba wa walimu.

  Kiswahili pia ni lugha rasmi ya Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo Rwanda ni nchi mwanachama.

  Mwezi uliopita, katika Siku ya Ushirikiano wa Afrika, Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliwataka Waafrika kujifunza Kiswahili ili kusaidia katika kuunganisha bara hilo.

 2. Kagame: Maneno ya Macron 'yana thamani kuliko kuomba msamaha'

  Kagame na Macron

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema maneno ya Rais Macron yalikuwa ‘kitu chenye thamani kuliko msamaha’’baada ya Rais wa Ufaransa kutoomba msamaha rasmi kwa Rwanda kuhusu jukumu la nchi hiyo katika mauaji ya kimbari.

  Katika hotuba aliyoitoa katika eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, Bw Macron aliomba msamaha kutoka kwa manusura, lakini hakuomba rasmi msamaha wa wazi kama ilivyotarajiwa.

  "Maneno yake yalikuwa kitu ambacho ni zaidi ya msamaha. Yalikuwa ukweli," Kagame alisema katika mkutano wa pamoja baadae.

  Egide Nkuranga, rais wa manusura wakuu' shirika la Ibuka, aliambia AFP amesikitika kwamba Macron "hakuomba msamaha kwa niaba ya nchi ya Ufaransa".

  Hatahivyo Bw. Nkuranga alisema Macron "alijaribu sana kuelezea mauaji ya kimbari najukumu la Ufaransa.Ni muhimu sana. Inaonesha kwamba anatuelewa.", AFP inaripoti.

 3. Rais Macron awasili Rwanda

  Rais Macron

  Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, katika juhudi za kufufua uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao ulisambaratika kwa zaidi ya miongo miwili.

  Wiki iliyopita katika mkutano wa kilele wa Paris kuhusu Afrika, Bwana Macron aliwaambia waandishi wa habari kwamba amekubaliana na Rais wa Rwanda Paul Kagame "kuanzisha ukurasa mpya wa mahusiano…"

  Wizara ya maswala ya kigeni ya Rwanda imetoa picha za kuwasili kwa Bwana Macron.

  Macron nchini Rwanda
  Macron Rwanda
 4. Rais Kagame kuwa wa kwanza kuleta kiwanda chanjo ya mRNA barani Afrika

  kAGAME

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema taifa lake litakuwa la kwanza kuleta chanjo ya mRNA barani Afrika wakati bara hilo likipambana na janga la virusi vya corona.

  “Rwanda inafanya kazi na washirika ili kuwa ya kwanza kutengeneza chanjo ya mRNA barani Afrika,” Kagame amesema katika mkutano wa kwenye mtandao wiki hii katika mkutano ulioitishwa na jopo huru la kukabiliana na janga la corona ingawa hakutoa ufafanuzi.

  Waziri wa afya wa Rwanda, Luteni Kanali Dkt.Tharcisse Mpunga ameliambia shirika la utangazaji la Rwanda kuwa mjadala huo ulikuwa ni wa kuleta kiwanda cha chanjo Rwanda.

  “Hii inaweza kuwa hatua kubwa kwa Rwanda na Afrika kupata chanjo …tunategemea kuwa punde mijadala hii itazaa matunda”, Dkt Mpunga salisema Alhamisi usiku.

  “Ikiwa kama Afrika bado inategemea chanjo kutoka mabara mengine , tutakuwa nyuma kwenye foleni mara zote panapokuwa na uhaba”, Bwana Kagame alisema hayo kwenye mjadala ulioongozwa na aliyekuwa rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf na waziri mkuu wa zamani wa New Zealand Helen Clark siku ya Jumanne.

  Mamlaka ya Rwanda haijatoa ufafanuzi ya namna kiwanda hicho kitawekwa Rwanda.

  Makampuni ya dawa ya Marekani na Ujerumani - Pfizer Inc. na BioNTech SE - walishirikiana kutengeneza chanjo ya mRNA vkukabiliana na Covid-19, kama Moderna Inc.

  Afrika ina viwanda vichache vya uzalishaji wa aina yeyote ya chanjo na vile vilivyopo vingi huwa vinaweka vifungashio na kusambaza - ila sio kutengeneza wenyewe.

  Chanjo ya mRNA inatofautiana na usambazaji wake na kuwa mshirika wa utengenezaji na RNA, au kemikali inayofahamika kama ribonucleic, kulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa. Pfizer Inc., pamoja na BioNTech SE, ilianzishwa na chanjo ya mRNA kupambana na Covid-19, wakati Moderna Inc.ilithibitishwa kuwa bora zaidi ya zile zilizotengenezwa na makampuni mengine yanayotumia namna nyingine ya utengenezaji.

  “Nilikuwa na fursa ya kufanya mawasiliano na makampuni kadhaa ya chanjo haswa nikilenga mjumbe wa teknolojia ya RNA iliyotumika kwenye Moderna na Pfizer,” Kagame alisema mwezi uliopita.

  “Tumekuwa tukishiriki katika mijadala na baadhi ya viongozi wengine barani kwetu lakini tunataka kujadilina zaidi kuhusu hili na wengine.”

  Mwezi Februari, Rwanda ilianza kutoa chanjo kwa wahudumu ambao wako kwenye hatari ya maambukizi wakati taifa hilo likiwa na idadi ndogo ya chanjo, baadhi wakiwa wamepata chanjo ya Pfizer-BioNTech.

  Zaidi ya watu 350,000 wamepata chanjo ya corona nchini humo, wizara ya afya imesema.

  Zaidi ya dozi milioni 17 za chanjo ya corona zimepelekwa Afrika ambayo ina watu bilioni 1.3 ambapo kiwango kilichotolewa ni chini ya 2% ya dozi milioni 780 zilizotolewa duniani , WHO imesema.

 5. Rais Paul Kagame azungumza na kaka wa Mahamat Idriss Déby

  Yves Bucyana

  BBC Swahili

  Kagame

  Rais Paul Kagame amempokea kwa mazungumzo Abdelkerim Déby Itno kama mjumbe maalum na mkuu wa ofisi ya rais wa Baraza la Jeshi la Mpito nchini Chad, kulingana na ofisi ya Rais wa Rwanda.

  Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo ya Jumatano jioni.

  Bwana Kagame anajulikana kama mmoja wa wale ambao walikuwa na uhusiano mzuri na makubaliano juu ya maswala yanayohusu bara la Afrika na Rais wa zamani wa Chad Idriss Déby Itno.

  Utawala wa kijeshi nchini Chad sasa unatishiwa na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa na Jumuiya ya Afrika kutaka wanajeshi warudishe madarakani kwa raia.

  Barala kuu la kijeshi linaloongoza Chad pia liko kwenye vita na vikundi vya waasi,ikiwa ilidaiwa kuwa Rais wa zamani Idriss Deby Itno alipigwa aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akipigana kwenye vita hivyo mwezi uliopita.

  Rais Kagame alipokea ujumbe wa Chad akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Vincent Biruta na Meja Jenerali Joseph Nzabamwita, mkuu wa idara ya ujasusi (NISS).

  Kwenye mitandao ya kijamii, wengine walisema kuwa kuonekana kwa Abdelkerim Idriss Déby kama balozi wa kaka yake mkubwa Jenerali Mahamat Idriss Déby ilikuwa ishara kwamba "familia ya Déby inaendelea kuimarisha utawala wake’’ Kabla na baada ya kifo cha mzee Déby, kuliripotiwa malumbano kati wanawe kuhusu atakayemrithi.

  Abdelkerim Idriss Déby, 29, alihitimu kutoka Chuo cha Jeshi cha Marekani (USMA) huko West Point mnamo 2015. Mnamo mwaka wa 2019 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa ikulu ya Rais wa Chad.

  Mnamo mwaka wa 2020, aliongoza ujumbe wa Chad uliokutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kujadili "kufungua" ubalozi wa Chad mjini Jerusalem.

 6. Kagame ataja 'unafiki' katika usambazaji wa chanjo ya corona

  Rais wa Rwanda Paul Kagame
  Image caption: Rais wa Rwanda Paul Kagame

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuna "unafiki" katika usambazaji wa chanjo ya Covid-19 duniani.

  Rais Kagame amesema hayo katika ujumbe wa Twitter baada ya Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, kusema kwamba mkataba ulioafikiwa kati ya mataifa tajiri na watengenezaji wa chanjo umefanya kuwa vigumu kwa shirika hilo kupata chanjo kwa ajili ya mpango wake wa Covax.

  View more on twitter

  Covax ni mpango wa kuhakikisha kuna usambazaji sawa wa chanjo ya Covid-19 katika nchi zote duniani.

  Mataifa tajiri yamekosolewa kwa kuhodhi chanjo na kufanya kuwa vigumu kwa nchi masikini kupata chanjo yoyote.

  Soma zaidi:

 7. Paul Rusesabagina

  Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema kukamatwa kwa mkosoaji wa chama tawala cha Rwanda RPF Paul Rusesababagina ni sawa na kulazimishwa kutoweka, ambao ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

  Soma Zaidi
  next