Afrika Mashariki

 1. Video content

  Video caption: ‘Taka hizi zimetenganisha familia yangu’ - Jinsi ya kukabiliana na taka hatari Kampala

  Katika mji mkuu wa Uganda , Kampala taka zote za kila siku hazikusanywi.

 2. Raia Kenya na Ethiopia waliochanjwa miongoni mwa walioruhusiwa kuingia Uingereza

  Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri
  Image caption: Kenya yaondolewa kwenye orodha ya Uingereza ya vikwazo vya kusafiri

  Nchi nane leo (Jumatano, Septemba 22) zimeondolewa kwenye orodha ya zile zilizopigwa marufuku kuingia Uingereza wakati serikali ya nchi hiyo inapoanza kutekeleza mabadiliko kwenye mfumo wake wenye utata wa usafiri kimataifa.

  Misri na Kenya ni nchi za Afrika ambazo sasa, zitakuwa na wasafiri wanaoruhusiwa kuingia Uingereza.

  Habari hii imepokelewa kama afueni kubwa nchini Kenya ambapo tasnia ya utalii imepata hasara kubwa kufuatia vizuizi vya usafiri kama njia moja ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

  Uingereza ni ya nne yenye mchango mkubwa zaidi kwa watalii wanaotembelea nchi ya Kenya iliyopo Afrika Mashariki ambayo kwa sasa hivi iko katikati ya msimu wake wa kilele cha utalii ambao unamalizika na uhamiaji wa nyumbu kila mwaka.

  Furaha ya kukaribisha zaidi ya watalii 100 waliowasili katika uwanja wa ndege wa Mombasa, pwani ya Kenya, zimeshuhudiwa kwa mbwembwe na taadhima kuu.

  Wageni waliowasili wakiwa ni kutoka Romania – watalii wapya katika soko hilo nchini Kenya.

  "Tuna furaha kubwa sana kuwa hapa, na tutafurahia ujio wetu kabisa. Ni mara yetu ya kwanza. Watu waje kutembelea, wafurahie," mmoja wa watalii alisema.

  Idadi ya watalii nchini humo imepungua kwa zaidi ya theluthi mbili kutokana na janga la virusi vya corona na katika juhudi za kufufua sekta hiyo kwa hali na mali, sasa imegeukiwa soko la watalii kutoka Asia na Mashariki mwa Ulaya.

  Hata hivyo, watalii hawa wapya wanaokuja ni sehemu ndogo tu ya kile Kenya ilizoea kabla ya janga hilo.

  Sekta hiyo hadi sasa imepoteza mapato ya dola bilioni moja na nusu huku ajira milioni mbili zikitoweka - takwimu ambazo Waziri wa Utalii Najib Balala anasema zitachukua miaka kuimarika.

  "Idadi bado ni ndogo, lakini tumeona polepolea watalii wameanza kujiwekea nafasi zao za kuzuru Kenya majira ya joto. Haifurahishi lakini angalau ni ishara ya nia njema na kuonesha kwamba maisha yanarudi kama kawaida katika utalii, " amesema Waziri wa Utalii Najib Balala.

  Je dhana potofu kwamba chanjo ya corona ina sumaku ilitoka wapi?

 3. Paul Rosesabagina

  Paul Rusesabagina aliangaziwa kama mtu aliyetumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashawishi maafisa wa kijeshi kuwapa njia salama ya kuwatorosha karibu watu1,200 ambao walitafuta maficho katika Hôtel des Mille Collines, ambayo alikuwa meneja wake wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.

  Soma Zaidi
  next
 4. Hezron Mogambi

  Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Nairobi

  Rais Uhuru Kenyatta (Kushto) na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga

  Jopo lililojulikana kwa jina Building Bridges Initiative (BBI) lilipaswa kuangazia masuala tisa ikiwemo ukabila, ufisadi na ugatuzi - ikiwa ni miongoni mwa changamoto kuu tangu taifa kupata Uhuru mwaka wa 1963.

  Soma Zaidi
  next
 5. Video content

  Video caption: Fahamu maisha binafsi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

  Katika mahojiano maalum na BBC Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza upande wake wa Maisha binafsi na kiasi gani Maisha hayo yamebadilika tangu ashike madaraka.