Ajali na Mikasa ya Ndege

 1. Watu 15 wamefariki kwenye ajali ya gari Mombasa

  Watu wapatao 15 wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea barabara ya Mombasa-Malindi nchini Kenya, maofisa wa serikali wameiambia BBC.

  Watu wengine ishirini wamejeruiwa katika ajali hiyo iliyotokea mapema asubuhi ya leo katika ajali hiyo iliyohusisha mabasi mawili.

  Madereva wa magari yote mawili wamefariki dunia hapo hapo.

  Mashaidi wa ajali hiyo wamesema sehemu ambayo ajali hiyo imetokea katika eneo lililokuwa katika ujenzi.

 2. Ndege aina ya Boeing 737 iliyosababisha ajali yaruhusiwa kuanza tena safari za abiria

  Vifusi kutoka kwa Ethiopian Airlines chapa 302 iliyotengenezwa na Boeing baada ya ajali ya pili nchini Ethiopia mwezi Machi 2019.

  Mkuu wa Mamlaka ya Safari za Anga Marekani (FAA), Steve Dickson, ametia saini agizo linaloruhusu ndege aina ya Boeing 737 kuanza tena safari zake kwa abiria.

  Bwana Dickson alisema ana uhakika wa asilimia 100 juu ya usalama wa ndege hizo ambazo zilipigwa marufuku kusafiri baada ya kutokea kwa ajali mbili za abiria nchini Indonesia na Ethiopia, na kusababisha vifo kwa watu 346.

  Uamuzi huo wa Mamlaka ya Safari za Anga Marekani (FAA), unamaanisha kuwa ndege hizo zinaweza kuanza tena safari za abiria kufikia mwisho wa mwaka huu.

  Mamlaka hiyo imetoa wito marubani kupewa mafunzo zaidi ili waweze kutumia kwa ubora wa juu kifaa kipya cha usalama kilichowekwa kwenye ndege aina ya Boeing 737.

  Aidha, wamiliki wa ndege ya Boeing wamefurahishwa na hatua ya FAA na kusema kuwa imejifunza kutokana na makosa yake yaliyotokea awali.

  Pia unaweza kusoma zaidi:

  Wakaguzi wagundua tatizo lingine katika ndege ya Boeing 737 Max

  Boeing yatangaza kuacha kuzalisha kwa muda ndege za 737 Max kuanzia Januari