Zambia

 1. Mwanamuziki wa Zambia ajitoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumpinga mtandaoni

  Slapdee

  Mwanamuziki maarufu wa Zambia Slapdee amejiondoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumkosoa kwa kufanya maonesho ya muziki kwa chama kilichokuwa madarakani.

  Chama hicho cha Patriotic Front kilishindwa uchaguzi na hivyo kundoka madarakani mwezi Agosti.

  Slapde, ambaye jina lake halisi ni Mwila Musonda, awali alitetea maamuzi yake ya kufanya maonesho kwa ajili ya maofisa kama biashara lakini inaoneka iliathiri muziki wake.

  Kufuatiwa kuchaguliwa Afrimma kushiriki kuwania tuzo, Wazambia walihamasisha watu watu mtandaoni kumpigia kura mwanamuziki wa Afrika Kusini Cassper Nyovest katika kipengele alichokuwa anawania cha mwanamuziki bora wa kiume kusini mwa Afrika ambapo kulikuwa na mshiriki wa Zimbabwe Jah Prayzah naTha Dogg kutoka Namibia na wengine.

  Kampeni za kumpinga Slapdee na kumuunga mkono Cassper Nyovest zilizua gumzo mtandaoni.

  Mwanamuziki wa Afrika kusini aliandika kwenye twitter "kwanini anazungumziwa Zambia?" alafu akasema "Ni sawa Zambia, hii ni biashara tu"

 2. Rais wa Zambia akanusha mazungumzo ya haki ya wapenzi wa jinsia moja Marekani

  Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alimkaribisha Rais Hakainde Hichilema katika Ikulu ya White Housewiki iliyopita
  Image caption: Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alimkaribisha Rais Hakainde Hichilema katika Ikulu ya White House wiki iliyopita.

  Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekanusha kufshiriki mazungumzo juu ya haki ya wapenzi wa jinsia moja wakati alipohudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.

  Uhusiano wa jinsia moja umepigwa marufuku nchini Zambia, ambako sheria za enzi za ukoloni wa Uingereza juu ya mapenzi ya jinsia moja bado zinatumika.

  Rais Hichilema alitoa tamko hilo siku ya Alhamisi wakati wa hotuba yake kwa taifa iliyorushwa moja kwa moja kutoka mji mkuu, Lusaka baada ya kuombwa kuweka wazi aliyoangazia katika ziara yake.

  "Hatukuenda huko kuzungumzia haki ya wapenzi wa jinsia moja. Hili ni jambo ambalo nataka kusema kwa msisitizo, "alinukuliwa akisema na gazeti la Zambia Daily Mail.

  Aliongeza kuwa katiba ya Zambia ilikua wazi kuhusiana na masuala yanayohusu haki ya wapenzi wa jinsia moja, ilisema ripoti ya tovuti ya Lusaka Times

  Marekani ilimuita nyumbani balozi wake nchini Zambia mnamo Disemba 2019 kati kati ya mzozo wa kidplomasia ulisababishwa na kauli ya balozi huyo baada ya kufungwa jela kwa wapenzi wa jinsia moja.

  Serikali ya Zambia ilimshtumu kwa kujaribu kuingilia sera zake.

 3. Rais wa Zambia alisifiwa kwa kusafiri na maafisa 'wachache'

  Rais wa Zambia alisifia timu yake ya kusafiri 'konda'

  Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekuwa akisifiwa mitandaoni kwa kusafirina “maafisa wachahche” kuhudhuria kikao cha 76 za mkutano wa baraza la kuu la umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani .

  Bwana Hichilema alisafiri kwa kutumia ndege ya Qatar Airways fkutoka mjini Lusaka, akiandamana na mawaziri wawili.

  “Kama nilivyoahidi kabala niingie madarakani, utahakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na kwa hivyo tumesafiri na timu konda ambayo inaundwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Fedha, Stanley Kakubo na Dk Situmbeko Musokotwane mtawaliwa, "alisema katika taarifa kabla ya kuondoka.

  "Huyu ni wa kwanza katika eneo ambalo [Rais wa Zimbabwe] Emmerson Mnangagwa na [Lazaro wa Malawi] Chakwera huchukua ndege zilizojaa watu wanaodandia safari", aliandika mwandishi wa habari wa Zimbabwe Hopewell Chin'ono.

  Mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii aliandika: "Afrika inainuka: Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameondoka Zambia kwenda Mkutano Mkuu wa UN, New York kwa kutumia ndege ya kibiashara".

  Rais wa Malawi mnamo Julai alikosolewa kwa kusafiri na familia yake kwa safari ya Uingereza lakini akasema kwamba walihitajika kwa hafla hiyo.

  Hakainde Hichilema: 'Mchunga ng'ombe' aliyeibuka kuwa rais wa Zambia

  Hakainde Hichilema:Tundu Lissu,Raila Odinga na Bobi Wine wanaweza kujifunza yapi kutoka kwake?

 4. HH

  Rais mteule wa Zambia kutoka chama cha upinzani cha UPND, Hakainde Hichilema, katika hotuba yake mara baada ya kutangazwa kumshinda rais Edgar Lungu, alisema kabla ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika wiki hii, aliwahi kuwekwa ndani mara 15.

  Soma Zaidi
  next
 5. Raila Odinga ampongeza rais mteule wa Zambia

  Odinga

  Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Rais Amolo Odinga amempongeza Raila Odinga ampongeza rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema.Katika ujumbe wake wa pongezi alioutuma kwenye ukurasa wa Facebook, Bw Raila amesema ’’ Ninachukua fursa hii kumpongeza rafiki Hakainde Hichilema

  ''Nachukua fursa hii muhimu kumpongeza rafiki yangu Hakainde Hichilema, Chama cha United Party of National Development (UPND) cha Zambia kwa ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais. ailsema , Raila.

  View more on twitter

  Wakati kukiwa changamoto ya kipindi kisicho cha kawaida cha afya ya umma, watu wa Zambia wameifanya Afrika ya kujivunia kufanya uchaguzi wa mafanikio.

  Uchaguzi wa huru, haki, wa kuaminika na kuthibitishwa kila mara huwezesha kuwepo kwa utashi wa watu.

  Ni tumaini langu kwamba uchaguzi huu utaimarisha maisha ya kidemokrasia ya Wazambia, kuleta maendeleao zaidi na kuwakumbusha Waafrika wenzenu popote walipo kwamba hakuna lisilowezekana. Nawatakia baraka zote katika siku na miaka ijayo.

  Soma zaidi:

  Hakainde Hichilema: Mfahamu mfanyabiashara tajiri aliyeshinda uchaguzi wa urais Zambia

 6. Habari za hivi pundeUchaguzi Zambia: Rais Edgar Lungu akubali kushindwa

  Rais wa Zambia wa sasa Edgar Lungu amekubali kushindwa moja kwa moja katika runinga. “Nachukua furasa hii kumpongeza ndugu yangu Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa kuwa rais wa saba wa Zambia”

  Bwana Lungu hapo awali alikuwa amedokeza kwamba atapinga matokeo ya uchaguzi baada ya kushutumu upinzani kwa ulaghai.

 7. Viongozi wa upinzani Afrika wapongeza ushindi wa uchaguzi wa urais Zambia

  Hakainde Hichilema ashinda urais Zambia baada ya kujaribu kwa mara ya sita
  Image caption: Hakainde Hichilema ashinda urais Zambia baada ya kujaribu kwa mara ya sita

  Viongozi mbali mbali wa upinzani katika nchi za Afrika wamempongeza rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema.

  Bwana Hichilema Jumatatu amethibitishwa mshindi katika uchaguzi wa urais, kwa kupata kura 2,810,777 dhidi ya Edgar Lungu aliyepo madarakani aliyepata kura 1,814,201.

  Ilikuwa jaribio lake la sita kugombea urais.

  Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine, ambaye aligombea urais mapema mwaka huu, amesema ushindi wa Bw. Hichilema haukuwa ushindi tu wa Zambia, bali ushindi kwa Afrika na demokrasia.

  Kiongozi mwingine mkongwe wa upinzani ambaye pia ni wa kutoka nchi ya Uganda Kizza Besigye alimpongeza rais mteule kwa ushindi wake.

  Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto Kabwe amesema Zambia “imeonyesha ulimwengu kiwango cha ukomavu wake wa kidemokrasia.

  Ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani unafanyika… ”.

  Nelson Chamisa, kiongozi wa upinzaji wa Zimbabwe, amesema "amefurahishwa" kupokea simu na yeye binafsi kumpongeza Bw. Hichilema.

  Raila Odinga wa Kenya naye pia amesema watu wa Zambia wamefanya bara la Afrika "lijivunie kwa kufanikisha uchaguzi" katikati ya janga la virusi vya corona.

  View more on twitter
 8. Hakainde Hichilema (14 July 2006)

  Hakainde Hichilema, mfanyabiashara aliyejitengenezea utajiri wake, ni kiongozi kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kupitia United Party for National Development (UPND).

  Soma Zaidi
  next