Kombe la Mataifa ya Afrika

 1. Sadio Mane: Uwanja wapewa jina la nyota wa Liverpool Senegal

  Sadio Mane
  Image caption: Sadio Mane akiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika

  Uwanja umepewa jina la Sadio Mane katika mji wa kusini-magharibi wa Sedhiou baada ya kuisaidia Senegal kupata mafanikio yao ya kwanza.

  Mshambulizi huyo wa Liverpool alifunga penalti ya ushindi wakati Simba ya Teranga ilipoishinda Misri kwa mikwaju 4-2 ya penalti na kutwaa ushindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza, baada ya mchezo kumalizika bila bao kufuatia muda wa ziada.

  Mabao yake matatu na pasi mbili murua kwa taifa hilo la Afrika Magharibi yalimpa tuzo ya Mchezaji bora na sasa meya wa Sedhiou, Adboulaye Diop, anasema uwanja wa soka wa eneo hilo utapewa jina la mtoto wao kipenzi.

  "Ningependa, kupitia uamuzi huu wa kutoa jina la Sadio Mané kwa uwanja wa Sédhiou, kuelezea utambuzi wa watoto wote wa mkoa huo, kwa mtu anayejulikana kwa utu wake kwa ujumla, Bambali na mji mkuu wake wa kikanda, ambao ni Sédhiou," Diop, ambaye ni waziri wa utamaduni na mawasiliano wa Senegal, alinukuliwa

  "Sadio Mané anastahili heshima hii."

  "Mane anapendwa na mamilioni ya watu kufuatia misaada anayotoa katika mji wake wa nyumbani kwa kuahidi pesa za kujenga hospitali na shule, kuchangia ujenzi wa misikiti na kutoa pesa kusaidia mapambano dhidi ya Covid-19.

  Kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo Mei 2018, aliwazawadia jezi ya Liverpool, wenyeji wa mji aliozaliwa wa Bambali ili waweze kuzivaa wakati wa mchezo.

  “Kijijini wapo 2,000, nilinunua jezi 300 za Liverpool ili niwapelekee wananchi wa kijijini, ili mashabiki wavae kuangalia fainali,” alisema Mane.

  Bambali ni mahali ambapo Mane alitazama urejeo wa umaarufu wa Liverpool dhidi ya AC Milan na kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2005 - akiwa na umri wa miaka 13.

  Na nyumbani anapotokea hakujawahi kuwa mbali na mawazo yake.

  Kutoka kwa klabu ya Metz ya Ufaransa hadi Liverpool kupitia RB Salzburg ya Austria na Southampton, Mane ametoka mbali hadi kutambuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani.

  Na baada ya mafanikio ya timu yake nchini Cameroon, Mane alisema kushinda Senegal Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza ni jambo kuu katika maisha yake ya soka.

  Soma zaidi:

  Fahamu mambo sita usiyoyajua kuhusu Sadio Mane wa Senegal na Liverpool

  ‘Tumengoja ushindi huu kwa miaka 60’- Mane afunga penalti ya ushindi na kuipa Senegal taji la kwanza la Afcon

 2. Timu ya soka ya Senegal yazawadiwa mashamba na pesa taslimu

  Rais wa Senegal amlimbikizia sifa kocha wa timu ya taifa, Aliou Cissé
  Image caption: Rais wa Senegal amlimbikizia sifa kocha wa timu ya taifa, Aliou Cissé

  Senegal imemzawadia kila mchezaji wa timu ya taifa ya kandanda zawadi ya pesa taslimu na mashamba kufuatia ushindi wao katika Kombe la Mataifa ya Afrika.

  Kila mchezaji wa timu alipokea zaidi ya $87,000 (£64,000) na kiwanja katika mji mkuu, Dakar, na katika mji jirani wa Diamniadio wakati wa sherehe iliyofanyika ikulu ya rais.

  Rais Macky Sall pia aliteua timu hiyo katika Tuzo ya heshima kutoka kwa Rais ambayo ni maarufu nchini Senegal, huku mashabiki wakishangilia nje ya lango.

  Rais hapo awali aliishukuru timu hiyo kwa kufika “kilele cha dimba hilo la Afrika” na kuleta ”fahari na heshima ambayo inaashiria watu wa kipekee. ”

  Pia alimsifu kocha wa timu hiyo, Aliou Cissé.

  Senegal iliishinda Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2, na kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.

 3. Alfred Mushi

  BBC Swahili

  Sadio Mane, Mohamed Salah and the Nations Cup trophy

  Ni lala salama ya AFCON leo katika dimba la Olembe unaopatikana kwenye mji kuu wa Cameroon, Yaounde.Nyota wawili wa Anfield ya England watakutana kuoneshana ubabe katika mchezo unaotarajiwa kushuhudiwa na wapenda soka wengi ulimwenguni.

  Soma Zaidi
  next
 4. Malawi yainyuka Uganda kufika fainali za Kombe la Mataifa

  Mara ya mwisho Malawi ilifuzu kwa Kombe la Mataifa ilikuwa mwaka 1984 na 2010
  Image caption: Mara ya mwisho Malawi ilifuzu kwa Kombe la Mataifa ilikuwa mwaka 1984 na 2010

  Malawi imeinyuka Uganda 1-0 katika fainali ya kundi B ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika mwaka 2021 na kujikatia tikiti ya mashindano hayo na kuitupa Cranes nje.

  Uganda ilihitaji sare katika mechi ya Blantyre, lakini ndoto yao ikazimwa na bao la Richard Mbulu katika dakika ya 15.

  Malawi wanasherehekea kufika fainali ya mashindano hayo itakayofanyika Cameroon mwaka 2022 – Hii ikiwa mara ya tatu wanafuzu kwa mashindano hayo.

  Kuondolewa kwa Uganda kumedidimiza matumaini ya nchi za Afrika Mashariki kufuzi kwa AFCON, baada ya Kenya na Tanzaniapia kuondolewa kutoka mechi hizo .