Maalim Seif

 1. Video content

  Video caption: Zitto Kabwe amuomboleza Maalim Seif

  Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Maalim Seif amekuwa nguzo muhimu.

 2. Maalim Seif aapishwa kuwa makamu wa kwanza wa urais

  Maalim Seif

  Maalim Seif Sharif Hamad kutoka chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo amepishwa rasmi kuwa makamu wa rais wa kwanza wa Zanzibar.

  Wakati akila kiapo hicho, Maalim Seif amehaidi kushirikiana na rais wa Zanzibar kwa hali na mali ili kuijenga Zanzibar kwa usalama na amani.

  Maalim alitoa shukrani kwa wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa "imani ya wananchi wangu ndio wito mtakatifu unaonilazimisha kusimama kuwatumikia."

  Aidha ameeleza kuwa uamuzi wa yeye Maalim pamoja na chama chake kufikia uamuzi wa kukubali kuingia katika serikali shirikishi ulikuwa mgumu sana ila nia ya rais Dkt.Hassan Mwinyi ndio iliwafanya wafikie uamuzi huo na kuweka pembeni madhila yote yaliyotokea.

  Yeye amewakilisha chama kuja kutibu majeraha yaliokuepo.

  Soma pia: