Angola

 1. Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola

  Mto uligeuka na kuwa mwekundu mwezi uliopita
  Image caption: Mto uligeuka na kuwa mwekundu mwezi uliopita

  Karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, waziri wa mazingira anasema.

  Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia.

  Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.

  Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chchote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.

  Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.

 2. China 'kujenga' kambi za kijeshi Tanzania na Kenya

  Jeshi la China

  China inafikiria kujenga kambi za kijeshi katika nchi nne za Afrika, kwa mujibu wa ripoti ya idara ya ulinzi ya Marekani.

  Tanzania, Kenya, Ushelisheli na Angola zimetajwa kuwa miongoni mwa nchi kadhaa ambazo China inapania kujenga kambi za kijeshi.

  Serikali za nchi hizo nne za Afrika zilizotajwa na Marekani hazijatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

  Ripoti hiyo iliyochapishwa wiki iliyopita imeangaziwa sana na vyombo vya habari wikendi iliopita, huku baadhi ya nchi ambazo kambi hizo zitajengwa zikikanusha kufanya mazungumzo na China.

  "Kando na kambi yake ya sasa nchini Djibouti, Jamhuri ya watu wa China ina mpango wa kuongeza kambi zake za kijeshi ughaibuni kusaidia vikosi vya majini, angani na ardhini," sehemu ya ripoti hiyo ilisema.

  Pia imeongeza kuwa China huenda ameamua sehemu itakapojenga vituo vyake vya kijeshi nchini Myanmar, Thailand, Singapore, Indonesia, Pakistan, Sri Lanka, Umoja wa Falme za Kiarabu,(UAE), Kenya, Ushelisheli, Tanzania, Angola, na Tajikistan.