Muungano wa Afrika - AU

 1. Marekani yakaribisha uteuzi wa Obasanjo kuwa mwakilishi wa AU eneo la Upembe wa Afrika

  Obasanjo
  Image caption: Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo

  Marekani imeunga mkono uteuzi wa rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuwa Mawakilishi wa Muungano wa Afrika katika eneo la Upembe wa Afrika.

  Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema Marekani itatoa ushirikiano kuelekea majadiliano ya kumaliza mzozo nchini Ethiopia ambako maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya robo milioni kuishi katika mazingira ya njaa

  Uteuzi wa Olusegun Obasanjo unakuja katika kilele cha mzozo wa miezi 9 katika jimbo la Tigray ambapo Umoja wa Mataifa unasema uhalifu wa kivita umefanywa, na sasa maelfu wanaweza kufa na njaa.

  Utawala wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed uko chini ya shinikizo kujadiliana na Chama cha Tigray People’s Liberation Front, ambacho Ethiopia imetambua kama shirika la kigaidi.

 2. Chanjo ya Urusi inatarajiwa kupatikana kwa kipindi cha miezi 12 kuazia mwezi Mei 2021,

  Kikosi kazi cha Muungano wa Afrika (AU) kimesema kuwa Urusi imetoa dozi milioni 300 za chanjo yake ya Sputnik V COVID-19 pamoja na msaada wa kifedha kwa nchi zinazotaka kupata chanjo hiyo.

  Soma Zaidi
  next