Canada

 1. Mwanajeshi Canada akabiliwa na kifungo jela kwa kulisha wenzake keki zenye bangi

  Keki
  Image caption: Keki

  Mwanajeshi wa Canada ambaye alilisha wanajeshi wenzake keki yenye bangi wakati wa zoezi la silaha sasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano.

  Koplo Chelsea Cogswell alipatikana na hatia ya kuwapawanajeshi wanane, "kitu cheye dawa za kulevya" pamoja na kuonesha kitendo cha aibu.

  Wanajeshi hao walikuwa wameelezea kuhisi kulewa na kuchanganyikiwa wakati wameshika silaha baada ya kula keki alizowapa mnamo mwaka 2018. Uhalifu huo ulitokea miezi mitatu kabla ya bangi kuhalalishwa kote nchini Canada.

  Jaji wa Jeshi Cmdr Sandra Sukstorf alitangaza uamuzi huo Jumatano.

  Alisema waendesha mashtaka kwamba walithibitisha bila shaka yoyote kuwa wanajeshi walioathiriwa walikuwa wamekula bangi iliyochanganywa na keki, ambayo koplo aliwapa kwa kujua.

  Kesi hiyo ya kushangaza inatokana na tukio lililotokea katika Kituo cha Mafunzo ya Kupambana huko CFB Gagetown katika mkoa wa New Brunswick.

  Waendesha mashtaka katika kesi hiyo ya kijeshi walisema kwamba Cogswell aliongezea hatari zaidi kwa hali ambayo yenyewe ilikuwa tayari ni hatari wakati alipowapa keki za chokoleti alipokuwa akisimamia kantini wakati wa mazoezi ya silaha uwanjani.

  Wanajeshi waliokuwa wanatoa ushahidi walikiri kuhisi "kutojua kinachoendelea", "kuchanganyikiwa" na "kuwa katika tishio fulani" na kuwa "walegevu" baada ya kula keki hizo zilizotengenezwa nyumbani.

  Maafisa wa matibabu waliitwa kufanya uchunguzi baada ya wanajeshi kuripoti dalili zao.

  Licha ya kwamba ilikuwa siku ya joto, uchovu wa joto uliondolewa.

  Baadaye, watano walithibitishwa kuwa na chembechembe za bangi, kama ilivyokuwa kwa keki moja iliyokuwa imefungushwa vizuri kwenye eneo la tukio.

  Madhara ya Bangi

  • Unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na wasiwasi usio wa kawaida
  • Ikivutwa na tumbaku, inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa kama vile saratani ya mapafu
  • Matumizi ya mara kwa mara yamehusishwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya kiakili
  • Upungufu wa kudumu wa kiwango cha mtu kufikiria na kufahamu mambo, baada ya kutumia kwa muda mrefu

  Pia unaweza kusoma:

  Tanzania na Kenya zinaongoza kwa uvutaji wa bangi Afrika mashariki

 2. Familia ya Kiislamu yauawa katika shambulio la chuki 'ya kukusudia'

  wakaazi

  Watu wanne wa familia ya Kiislamu wameuawa "kimakusudi" katika shambulio la gari siku ya Jumapili, polisi wa Canada wanasema. Soma zaidi.

 3. Video content

  Video caption: 'Niliweka tattoo ili niwe na alama sawa na ya mwanangu'

  Derek Prue, kutoka Alberta nchini Canada, aliamua kwenda kuchora tatoo ambayo inafanana na alama ambayo mtoto wake wa kiume mwenye miaka nane anayo