Islamic State

 1. Mashambulizi mapya ya wanamgambo yaripotiwa Msumbiji

  The insurgency has created a humanitarian crisis with many displaced from their homes

  Wanamgambo wa kijihadi wamehusika tena katika mashambulio mapya karibu mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, vyanzo vya habari vya jeshi vimeliambia shirika la habari la AFP.

  Shambulio hilo linakuja wakati ambapo nchi za kusini mwa Afrika zimeishinisha kupelekwa kwa kikosi maalum kusaidia Msumbijikukabiliana na wanamgambo hao.

  "Wanamgambo hao walijaribu kushambulia ngome za vikosi vya serikali mjini in Patacua, karibu na eneo la Afungi LNG lakini walirudishwa nyuma baada ya kupatikana kwa msaada kutoka angani," shirika la habari la AFP lilinukuu vyanzo vya habari vikisema.

  Mkoa wa kaskazini Cabo Delgado kwa muda mrefu umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa lakini uvamizi kutoka kwa wanamgambo wa kijihadi ulianza mwaka 2017.

  Mzozo huo umevuti ajamii ya kimataifa baada ya wanamgambo kuteka mji wa Palma mwezi April, kuua raia wa kigeni na kukwamisha mradi wa gesi asilia wa thamani ya dola bilioni 20 za Kimarekani.

  Mashambuilo ya wanamgambo yamesababisha mzozo mkubwa wakibinadamu, huku watu waliofurushwa makwaowakiishi katika kambi za wakimbizi karibu na mikoa inayozunguka Cabo Delgado.

 2. Kwanini ni vigumu kukabiliana na kundi la IS Msumbiji?

  Militants in the area

  Shambulizi la hivi karibuni lililosababisha wengi kupoteza maisha kutokana na shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa jihadi wa kundi la Islamic State kaskazini mwa Msumbiji limeshutua dunia. Mamia ya wapiganaji waliokuwa wamejihami walifanikiwa kudhibiti mji ulio karibu na mradi kubwa zaidi wa gesi Afrika. Waliwaua makumi ya watu, wenyeji na wataalamu huku wakiacha miili iliyokatwa vichwa mitaani. Lakini je hili lilitokea vipi, kwanini serikali ya Msumbiji imeshindwa kukabiliana na wanamgambo na je nini kinahitajika kushinda vita hivi?Soma zaidi

 3. Ureno kuwapeleka wanajeshi wake Msumbiji baada ya shambulio la kigaidi

  Ramani ya Msumbiji

  Ureno imesema itawapeleka wanajeshi wake katika koloni lake la zamani, Msumbiji, kufuatia mashambulio ya wanamgambo wa Kiislam dhidi ya mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo.

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno Augusto Santos Silva amesema karibu maaskari 60 wanajiandaa kuelekea Msumbiji kuwapa usaidizi majeshi ya nchi hiyo.

  Wiki iliyopita, mamia ya wanamgambo walivamia mji wa Palma katika mkoa wa Cabo Delgado, na kuwaua makumi ya raia.

  Maelfu ya watu wametoroka eneo hilo wakiwemo raia wa kigeni wanaofanya kazi katika sekta ya kawi inayohusisha mradi wa gesi asilia unaogharimu mabilioni ya dola.

  Wengi wao hawajulikani walipo.

  Msumbiji: Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?

  Cabo Delgado: Uhusiano uliopo kati ya mali asili,uasi na mapigano nchini Msumbiji

 4. Msumbiji

  Uasi unaoendelezwa na kundi moja la kiislamu katika kona ya juu ya taia la Msumbiji umegeuka na kuwa vita vya wazi ambavyo vimesababisha mauaji, watu kukatwa vichwa na kutekwa kwa miji kadhaa katika wiki za hivi karibuni katika Mkoa wa Cabo Delgado.

  Soma Zaidi
  next
 5. Wanamgambo wa Kiislamu 'wawakata vichwa watoto' Msumbiji

  msumbiji

  Shirika la kimataifa linasema watoto wadogo wa hadi miaka 11 wanauawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa Kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.

  Mwanamke mmoja ameliambia shirika la Save the Children kwamba alishuhudia mtoto wake aliyekua na umri wa miaka 12 akiuawa karibu na mahali alipokuwa amejificha na watoto wake wengine.

  "Baada ya mwanangu kuuawa, tulibaini hni hatari kuendelea kuishi katika kijiji chetu,"alisema.

  "Tulikimbili anyumbani kwa baba yangu katika kijiji kingine, lakini baada ya siku chache mashambulio yakaanza tena huko pia ."

  Zaidi ya watu 2,500 wameuawa na wengine 700,000 wametoroka makwao katika mkoa wa Cabo Delgado ulio na utajiri mkubwa wa gesi na mafuta tangu mashambulio ya wanamgambo yalipoanza mwaka 2017.

  Baadhi ya watu wamefariki wakijaribu kutoroka eneo hilo baada ya boti waliyokuwa wakisafiri kuzama.

  Mwezi Novemba, chombo cha habari cha kitaifa kiliripoti kwamba zaidi ya watu 50waliuawa kwa kuchinjwa katika uwanja wa mpira wa miguu huko Cabo Delgado.

  Na mwezi April mwaka jana, makumi ya watu walichinjwa na wengine kuuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji kimoja.

  ramani

  Makundi ya kutetea haki yanasema vikosi vya serikali vimekuwa vikitekeleza ukiiukwaji wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kukamtwa kiholepa, ukatili na mauaji wakati wa oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kijihadi.

  Serikali ya Msumbiji imeomba jamii ya kimataifa kuisaidia kukabiliana namashambulio ya wanamgambo.