Nigeria

 1. Davido: Nyota wa Afrobeats asema mashabiki walimtuma £300,000 baada ya wito kupitia twitter

  th

  Nyota wa Afrobeats Davido anasema mashabiki wamemtumia takriban pauni 300,000 baada ya kuwataka wamtumie pesa kwenye Twitter.

  Mwimbaji huyo aliomba mashabiki wanaoamini kuwa "nimekupa wimbo unaovuma" "nitumie pesa", kabla ya kuweka jina lake halisi, David Adeleke, na nambari ya akaunti ya benki.

  Picha za skrini alizotoa mtandaoni zinaonyesha kuwa amekusanya zaidi ya Naira milioni 170 za Nigeria (kama pauni 300,000).

  Newsbeat imemtaka Davido kutoa maoni yake lakini bado hajajibu.

  Davido - ambaye alitumbuiza katika chumba cha mapumziko cha 1Xtra mwezi Machi mwaka huu - anachukuliwa kuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa Kiafrika duniani

  View more on twitter

  Mwanamuziki huyo alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa lengo lake lilikuwa ni kutaka mashabiki wamtumie Naira milioni 100 ili kuondoa gari lake la Rolls Royce kutoka bandari ya Nigeria, ili aweze kulipa bili ambazo hazijalipwa ili kuachilia bidhaa iliyosafirishwa kutoka nje ya nchi.

  Abubakr mwenye umri wa miaka 23 ni shabiki mkubwa wa Davido na anasema kumtumia pesa "ni jambo lililokamilisha siku yake".

  "Nilifanya hivyo kwa upendo. Najua yeye ni tajiri zaidi yangu na watu wanasema kwa nini nifanye hivyo," anaiambia Radio 1 Newsbeat.

  "Inanifanya nijisikie mwenye furaha. Inahisi kama moja ya malengo yangu yamefikiwa. Ni nadra kwa shabiki kufanya miamala na mtu mashuhuri."

  Wakati baadhi ya mashabiki wake wamefurahi zaidi kutuma pesa wengine wamemkosoa mwimbaji huyo.

  Mtumiaji mmoja aliandika katika twitter: "Ulimwengu unaenda wazimu, Davido anawezaje kuwauliza mashabiki [pesa]?"

  Lakini wengine hawakukubali, huku mmoja akisema: "Anastahili zaidi... amekuwa baraka kwa wengi na ni wakati wa kumrudishia. Happy birthday in advance @davido."

  Wengi wameshiriki picha za skrini za uhamisho wa benki kwa nyota huyo wa Nigeria kujibu chapisho lake la kwanza.

  Davido mara nyingi hushiriki picha kwenye Instagram akiwa kwenye jeti binafsi, au akiwa na magari ya kifahari na vito vya bei ghali.

 2. Mashabiki washangilia kuungana tena kwa bendi ya P-Square Nigeria

  P -square

  Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii alisema kwenye Instagram: "Tafadhali acha upendo na upatanisho huu udumu milele. Amina."

  "Nimejawa na hisia. Kama pacha siwezi kufikiria kutokuwa na uhusiano mzuri na pacha wangu kwa muda mrefu," mwingine alisema.

  Pia walifanya ushirikiano wa kimziki na wanamuziki wengine kama vile Diamond Platinumz wa Tanzania na nyota wa Marekani Akon.

  Walisaini lebo ya Akon ya muziki -Konvict katika mwaka 2011 na mwaka mmoja baadaye wakapata mkataba wa kusambaza muziki wao na kampuni ya Universal Music Group.

  Pamoja na kutajwa kama kikundi cha msanii wa MTV Afrika wa muongo mwaka 2015 walishinda pia tuzo ya kikundi bora mara tatu.

  Mashabiki wa kundi maarufu la muziki la P-Square nchini Nigeria wanaelezea kufurahishwa kwao na taaarifa kwamba ndugu hao walianza kuimba pamoja karibu miongo miwili na kisha kutengana wamepatana.

  Wawili hao - wanaojumuisha mapacha Peter na Paul Okoye - walitofautiana miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, na bendi hiyo ikatengana mnamo 2017.

  Sababu hasa ya kutengena kwao haikuwahi kutangazwa wazi kwa umma hata hivyo majaribio ya awali ya kuwaleta pamoja, yalihusisha wanasiasa, viongozi wa kidini na watu wengine mashuhuri hayakufanikiwa.

  Jumbe za mitandao mbali mbali ya kijamii ambazo walituma tangu watengane kimuziki ziliashiaria kuwa ugomvi wao ulihusisha wake zao na kaka yao mkubwa, ambaye pia alikuwa meneja wao.

  Lakini katika ujumbe wa Instagram Peter na Paul walisema "vichwa 2 ni bora kuliko 1".

  View more on instagram

  Tayari kuna taarifa kuwa wawili hao huenda walimaliza mzozo wao baada ya kila mmoja kumfuata mwingine kwenye mtadao wa Instagram. Halafu video ya wawili hao wakikumbatiana ikasambaa sa a kwenye mitandao ya kijamii Jumatano.

  Baada ya kutengana kila mmoja wao alishuka kimziki kwani iwe Mr. P (Peter) na Rudeboy (Paul) hakuna aliyefikia kiwango cha mafanikio waliyoyapata walipokuwa pamoja kama -P-Square.

  Wakiwa wawiliwalitawala katika muziki wa Nigeria kwa miaka na walikuwa ni moja ya makundi ya kuwanza kuuza miziki ya Afrobeats katika maeneo mengine ya bara

  Waliuza matamasha yao ya maonyesho ya moja kwa moja yaliyotawaliwa na densi ya ukakamavu iliyokuwa na miondoko ya break-dance

  Wawili hao - wanaojumuisha mapacha Peter na Paul Okoye - walitofautiana miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, na bendi hiyo ikatengana mnamo 2017.

  Ndugu hao, ambao walitimiza miaka 40 siku ya Alhamisi, walitawala tasnia ya muziki ya Nigeria kwa miaka mingi na muziki wao ulivuma chini humo na kwingineko.

  Hivi majuzi walionekana wakikumbatiana katika video iliyosambazwa sana mitandaini.

  Pulse Nigeria imeshiriki video hiyo kwenye Twitter.

  Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii alisema kwenye Instagram: "Tafadhali acha upendo na upatanisho huu udumu milele. Amina."

  "Nimejawa na hisia. Kama pacha siwezi kufikiria kutokuwa na uhusiano mzuri na pacha wangu kwa muda mrefu," mwingine alisema.

  • Peter wa P-Square aomba radhi mashabiki
 3. Marekani yaiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini

  Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ya nchi zinazochukuliwa kukiuka uhuru wa kidini
  Image caption: Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ya nchi zinazochukuliwa kukiuka uhuru wa kidini

  Marekani imeiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini, kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken nchini humo.

  Serikali ya Marekani mwaka jana iliiweka Nigeria katika orodha yake maalum ya waangalizi wa mataifa ambayo yaliendekeza ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kidini.

  Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ambayo ina Myanmar, China, Eritrea, Iran, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Saudi Arabia, Tajikistan na Turkmenistan.

  Algeria, Comoro, Cuba, na Nicaragua pia zimo kwenye orodha maalum ya serikali ambazo zimekiuka uhuru wa kidini, kulingana na idara ya masuala ya kigeni ya Marekani.

  Hata hivyo, makundi ya kijihadi ya Boko Haram na Iswap linaloendesha shughuli zake kaskazini-mashariki mwa Nigeria, bado yanatia wasiwasi.

  Bw Blinken anazuru Nigeria siku ya Alhamisi katika awamu ya pili ya safari yake ya mataifa matatu ambayo ni pamoja na Kenya na Senegal.

  Anatarajiwa kukutana na Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari kujadili jinsi nchi zote mbili zinaweza kushirikiana zaidi katika afya ya kimataifa, usalama, kupanua upatikanaji wa nishati na ukuaji wa uchumi.

  Nigeria inapambana na vitisho vingi vya usalama, vikiwemo uasi wa muda mrefu wa Boko Haram, mapigano baina ya jamii na hivi karibuni, wimbi la utekaji nyara mkubwa shuleni unaofanywa na magenge yenye silaha.

  Soma:

  Fahamu dini mpya inayozua mjadala Mashariki ya kati

  Je waraabu wanaipuuza dini?

 4. Walimu wa chuo kikuu Abuja watekwa pamoja na watoto wao

  m

  Taarifa kutoka Nigeria zinasema wanaume wenye silaha wamekivamia chuo kikuu cha Abuja, kilichopo mji mkuu wa nchi hiyo.

  Wakazi wa chuo ambao hawakutaka majina yao kutajwa , wamethibitisha shambulio hilo katika eneo la chuo la Gwagwalada, kutokea majira ya saa saba usiku wa nchi hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwalimu mmoja, ni kuwa walimu watatu na watoto wao wawili walichukuliwa mateka.

  Taarifa zinasema wanaume hao wenye silaha waliwashinda nguvu walinzi wa chuo na kuweza kuingia katika nyumba za walimu na kuwateka.

 5. Jengo Nigeria laporomoka: Jitihada za kutafuta manusura zinaendelea

  Kifusi

  Waokoaji wanafanya kazi usiku kucha kutafuta manusura katika mji wa Lagos nchini Nigeria baada ya jengo la ghorofa 22 kuporomoka wakati wa ujenzi.

  Takribani watu wanne wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani walipo. Mchimbaji yuko eneo la tukio na waokoaji na baadhi ya wenyeji wanatafuta vifusi na chuma kilichosokotwa.

  Watu wanne walionusurika wamepatikana kufikia sasa.

  Hapo awali, picha kutoka kwenye tovuti zilionesha umati wa watu karibu na kilima kikubwa cha uchafu. Ni nini kilisababisha kuanguka na ni watu wangapi wamenaswa chini ya vifusi bado haijulikani.

  Wakati huo huo, mamlaka za mitaa zimeamuru uchunguzi kuhusu kuanguka na kuahidi kutoa ripoti ya mwisho kwa umma. Rais Buahari amezitaka mamlaka kuongeza juhudi za uokoaji.